Kutoka Taifa: Yanga Vs Toto African, vita ya ubingwa ama kushuka daraja!

Mkuu ila si kwa leo maana walikaza matak kweli leo nadhan wanahuzunika kukosa fungu walilokuwa wameahidiwa na mikia kupitia sportpesa kwakweli sijawahi kuwaona toto wakikomalia game kama hii ya leo ila kushuka daraja nako ni kubaya kwan rupurupu za vpl hupat nk.
 
Sijapenda mtoto wetu kushuka daraja!
Imebidi iwe hivyo ili kuiadhibu Mbao kwa kuwataka watuinamie na kutupigia makofi siku ya kukutana nao (Guard of Honour). Hiyo ni adabu tosha kwa kijana aliyedokoa mboga sahanini kwa mzee. Lakini adabu zaidi ataipata ndani ya kiwanja kwa kipigo ambacho huenda kitamnusuru mdogo wetu na kushuka daraja.
 
Mixed emotions, naumia timu ya nyumbani Toto Africa kufungwa, nashangilia chama langu Yanga kutwaa ubingwa
 
Mimi nimewashangaa sana,hata na mechi na Azam hawakukaza namna hii
 
Yanga nao kuanzia sasa hivi inabidi wajifunze,kipindi cha kwanza na kipindi cha pili mwanzoni wanacheza kwa ku relax sana utafikiri tayari wameshashinda.Hawajui wanavyotupa pressure zisizo za lazima sisi mashabiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…