Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Dogo anajitahidi

Ni kweli anajitahidi ingawaje takwimu hasa uzalishaji ajira ni kama kaweka kiwango cha juu. Mfano, kusema makampuni makubwa au viwanda viitakavyozalisha ajira 500 kwa mwaka watasamehewa baadhi ya kodi. Hii iko juu sana labda kama alikusudia ajira ambazo zitazalishwa na wanunuzi wa bidhaa vya viwandani kama maduka. Nayo hii ni ngumu sana kupata takwimu sahihi.
 
Lugha zote mbili za kufundishia kwa wakati mmoja how,January muongo sana
 
Changamoto za elimu zipo lukuki
Jambo la kufanya ni
Kuondoa mjadala wa dira wa elimu yetu kwa kuweka misingi inayochochea
Uweledi
Udadisi

Ubunifu
Uzalendo
Pamoja na kusisitizia katika lugha ya kufundishia tuna uwezo wa kutumia lugha zote mbili

Kama mwalimu hajatulia elimu haitosonga serikali yake itazingatia kuondoa changamoto zote zinazowakabili waalimu kuhakikisha elimu inapiga hatua
 
January Makamba atafanya maajabu wasiotarajia Watanzania mwaka huu.
 
At least umejitaidi kiasi flani Ku arrange hoja zako zinaeleweka.
 
Huu urais huu... mwaka huu viroja!

Kwa watu wa makamo yake, Kingwngala, Kigoma Malima, Ngeleja nk mpaka sasa hakuna aliyejenga hoja nikaona anaweza kuwatisha wapinzani, nadhani angekuwa Zitto Kabwe at least UKAWA wangeweza kupata shida kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Eti wavuvi watapewa Boti,jamani uongo mwingine huu.imeshindikana kununua Meli tu kwenye ziwa victoria ya kwenda Bukoba,Ziwa Tanganyika,ziwa Nyasa,leo tunadanganywa wavuvi watanunuliwa boti uongo huu,kuna cha bure hapa duniani?
katika wagombea wa ccm waliotangaza nia hakuna mgombea mwenye sera za uwongo kama huyu sijui anatuona sisi ni wajinga wa kudanganywa miaka yote
 
Eti wavuvi watapewa Boti,jamani uongo mwingine huu.imeshindikana kununua Meli tu kwenye ziwa victoria ya kwenda Bukoba,Ziwa Tanganyika,ziwa Nyasa,leo tunadanganywa wavuvi watanunuliwa boti uongo huu,kuna cha bure hapa duniani?
nimecheka sana ! unajua kitu kingine nilichogundua ni kwamba ukiacha rushwa silaha nyingine ya ccm ni uongo .
 
Lakini si ndio haya yalikuwa yamependekezwa katika rasimu ya katiba mpya ya mzee Warioba? Na hawa hawa akina Tanzania Mpya wakayapiga chini? Mimi nashindwa kuelewa hawa watia nia wa ccm wanataka tuwaeleweje?

Wanafiki hawa...ila nampongeza huyu kwa kuweza kupangilia uongo wake ukawa mzuri kuliko yule wa mtama
 
Baada ya mabilion ya kikwete sasa yanakuja mamilion ya makamba.
 
Back
Top Bottom