Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

January hizi pesa za haya yote uliyoyasema utatowa wapi?umesema utawezesha vyuo kukopesha wanafunzi how jamani?mana kwa sasa vyuo vinategemea ada ndo kama income zao?
 
Weng waliotangulia hawajatoa hoja za kueleweka lakini mwana kaya anazungumza uhalisia hapa.
 
hakika nimepata kitu kutoka kwako
miongoni mwa watia nia wachache wenye kujibu swali la "how"
 
Rushwa hili limezungumzwa na watu wengi zipo njia nyingi katika kuthibi rushwa zipo njia mbili
Kimfumo mamlaka, kitaasisi

Na mfumo wa kijamii

Kesi za wahujumu uchumi ziendeshwe kwa wazi na zieleweke
Kwa kushirikiana na viongozi wa dini kukemea na kuichukia rushwa kivitendo
 
Eti wavuvi watapewa Boti,jamani uongo mwingine huu.imeshindikana kununua Meli tu kwenye ziwa victoria ya kwenda Bukoba,Ziwa Tanganyika,ziwa Nyasa,leo tunadanganywa wavuvi watanunuliwa boti uongo huu,kuna cha bure hapa duniani?

Na wavuvi kukopeshwa majokofu ili wahifadhi samaki. Aisee!!! Kweli CCM Oyee!
 
Kijana anamwagika sera, yuko vizuri kisiasa.
 
Wanafiki hawa...ila nampongeza huyu kwa kuweza kupangilia uongo wake ukawa mzuri kuliko yule wa mtama

Na hapo ndo alipomshinda wa mtama kajipanga vizuri hata uzushi haushtukiwi kabisa. Hafu wanapigana madongo wao kwa wao sijui ili iweje.
 
January atatoa milioni hamsini kwa kila kijiji,jamani Tanzania tuna vijiji vingapi?January atawezesha vyuo viweze kukopesha wanafunzi,Huku akisema kunawili kwa nchi hakutegemei kodi za mapato,bali kunategemea kuwainua watanzania.sasa hizo pesa za kugawa kama pipi atattoa wapi kama hatokusanya kodi ipasavyo?
 
Eti wavuvi watapewa Boti,jamani uongo mwingine huu.imeshindikana kununua Meli tu kwenye ziwa victoria ya kwenda Bukoba,Ziwa Tanganyika,ziwa Nyasa,leo tunadanganywa wavuvi watanunuliwa boti uongo huu,kuna cha bure hapa duniani?

Khaaaa....huyu mtu namvulia kofia😕
 
Kaanza kumpopoa mtu kuhusu rushwa.Eti, adhabu ya kijamii kwa mtoa rushwa ni kugoma kwenda kwenye sherehe alizoalika watu.
 
Hivi Chadema lini wagombea wake wanatangaza nia zao kwa wananchi.
 
Aibu....aibu,aibu mpaka mwisho. Hivi ccm hawana akili kiasi hiki? Hivi hawajui....... Hapana huu ujinga mwisho October. Mungu wape ujasili Wa kuachia nchi kwa ustarabu vinginevyo nchi ilipofika imevimba itapasuka kwenye kutangaza matokeo.
 
Back
Top Bottom