Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Wakati wa maswali:
1. Kuhusu michezo: Ni kwa namna gani atatatua tatizo la michezo kusuasua?
2. Namna gani atatatua changamoto za foleni jijini Dar es salaam?
3. Mkakati gani wa kuwasaidia wanamama waweze kupata mikopo midogo midogo?
4. Landa speculators: Hili swali linahusu wale wenye kuhodhi ardhi kubwa huku hawaiendelezi. Je, ni namna gani atawashughulikia watu wa aina hiyo?
Mhe Januari anaanza kudondosha nondo kujibu maswali yote yaliyoelekezwa kwake!
1. Majibu ya swali la kwanza:
- Kuunda academy za michezo ili watoto wadogo wa miaka 6, 7, 8 waanze kufunzwa michezo katika umri huo mdogo.
- Kuwezesha kifedha timu za daraja la kwanza ili iwe motisha kwao na kuepusha mfumo wa sasa wa kutembeza bakuli ambao unawavunja moyo wana michezo.
2. Katoa nondo nyingi sana ila kubwa ni kwamba atajenga flyovers ili kutanua zaidi njia za kutoka katikati ya jiji na kwenda kwenye zile four ateries (njia nne kuu za kutoa Dar). Hili linafanyika kwa miaka chini ya 10 tu, ila amegoma la kuweka foleni kwa sababu itahitaji miaka 50 ili mradi kukamilika. Hivyo kwa uharaka wa tatizo la foleni, njia ya flyovers ndio nzuri zaidi.
4. Majibu kwa swali la nne:
- Ataweka gharama kubwa kwa speculators. Hili ni jambo la muhimu sana na kiukweli dogo huyu ni kichwa! Ameni-impress.
Majibu ya maswali hayo niliyobold yanaonyesha kuwa ama ni mbabaishaji au anawajua watu wake kwa hiyo anasema lolote la kuwafurahisha.
(1) Kuhusu michezo na hizo academy zake sijui ni nini na wapi. Elimu ya sekondari yenyewe ni tatizo halafu mtu anaahidi kujenga academy zenye vifaa vya michezo, sasa sijui hizo zitajengwa Dar es Salaam tu au zitajengwa kila Kata? Majibu kama haya yanaonyesha viongozi wetu ni watu wa namna gani. Vipaji vya michezo huanzia mashuleni; zamani sana tulikuwa na utaratibu wa kitaifa wa wa kuhimiza michezo mashuleni kuanzia shule za msingi (UMISHUMITA) hadi sekondari (UMISETA) ambapo wachezaji wengi wa kitaifa walitoka huko: Binafsi ninawafahamu akina Daud Salum, Hussein Masha, Ibrahim Malekano na Lawrence Mwalusako- wapo wengi sana. Marekani wana utaratibu kama huo huo tuliokuwa nao Tanzania zamani hizo. Kuna ngazi kama tatu za michezo; ngazi ya HIGH School, ngazi ya College na ngazi ya Professional. Kila mwaka vyombo vinavyosimamia michezo ya professional huchukua wachezaji wapya kutoka kwenye ngazi ya College. Ingawa serikali haichangii kukuza michezo ngazi yoyote, lakini ile ngazi ya high school ni sehemu inayopiwa na kusimamiwa na kodi ya wanachi. Wanafunzi wanaofanya vizuri HIGH school hupata skolaship za kwende College ambako kila college ina mpanago wake wa kuendesha michezo yao lakini wakiwa wanasimamiwa na chombo kimoja cha National Collegiate Athletic Association NCAA.
Kwa hiyo hiyo ahadi ya mpango wa kujenga Academies ni maneno matamu kwa wasikilzaji ambao wakitoka hapo mkutanoni wanasahau, lakini siyo ahadi inayotoka mdomoni mwa mtu serious. Ni sawa na maneno ya nwaka 2010 ya kuleta meli mpya huko Bukoba, Kigoma na Mbaba Bay ambapo leo hata zile mbovu zilizokuwapo hazifanyi kazi tena na hakuna anayefuatilia.
(2) Kuwezehsa kifedha timu za daraja la kwanza ni maneno yasiokuwa na mbele wala nyuma unless aseme kuwa zitakuwa zinapata ruzuku ya serikali. Kila timu ya daraja la kwaza leo hii hupewa sehemu ya mapato yatokanayo ni mechi zao lakini fedha hizo hazitoshi timu kujiendesha. Kwa vile timu za daraja la kwanza ni biashara serikali haitakiwa kujiingiza kwenye vilabu bali ishughulikie timu ya Taifa tu. Kila kilabu kiachiwe namna ya kujiendesha chenyewe kwa faida. Kuna njia nyingi sana kwa vilabu kujiendesha kwa faida ikiwa ni pamoja na uuzaji wa matangazo, uuzaji wa jezi zao kwa mashabiki, ujengaji wa vitega uchumi vya michezo.
(3) Kujenga Flyovers Dar es Salaam yote ndio uwongo mweninge ambao kiongozi anaweza kusema. Utajenga Flyover ngapi na utabomboa nyumba ngapi ili upanue barabara za jiji la Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaama lilianza kuharibika mwaka 1988 baada ya ujenzi holela kuanza; master plan ya mwisho ambayo ilikuwa itumiwe kujenga Sinza haikufuatwa tena. Kiongozi siriasi angesema tu kuwa Da tuna tatizo ila itabidi tupange upya huduma za jiji kusudi szisiwe za kuelekea sehemu moja tu. Huduma muhimu zinatakwa ziwe decentralized kiasi kuwa mtu halazimiki kwenda City center kupata mahitaji yake. Iwapo m,tu aliyeko Kimara anaweza kupata kila kitu huko huko basi msongamano wa Morogoro road utapungua sana. Upanuzi wa baadhi ya barabara na ujenzi wa barabara mpya ni idea ambayo ningekubali kwa mfano upanuzi wa barabara zilizoko kwa mfano upanuzi wa barabara inyotoka Sinza kijiweni hadi Magomeni, upanuzi wa barabara inayotoka Ubungo Maziwa hadi viwanja vya jangwanai. Vile vile ujenzi barabara nyingine mpya kabisa kwa mfano kutoka Kinondoni kwenda United Nations kwa kupita katikati ya Muhimbili na Azania, na kutoka Tabata hadi Jangwani kwa kupitia ile barabara ya Ubungo Maziwa. Kuna plani nyingi zinazowezekana ila viongozi wetu wanataka majibu mkato wa Flyover tu kwa vile hayo ndiyo wasikilazji wanataka kusikia bila kuangalia kuwa flyover zinasaidia kwenye intersection ya barabara mbili tu lakini hazipunguzi traffic density kwenye barabara yoyote