Muhongo ana Kiburi jeuri na dharau, aende akafanye kazi za taaluma Urais hauhitaji wataalam. Kafieni mbele huko na njaa zenu.
Kikwete ni mchumi na ni Rais je uchumi wetu unapaa?
Haha.
Muhongo kwenye gesi sio mtu mzuri wa kubishana nae kwa wanasiasa wa Tanzania, ataisia kukuabisha tu na kukung'ong'a ukose pozi. Give credit where credit is due, he is the most capable among the candidates when it comes to gas vision and knowledge, kwengine it's up for debate.
Wasichoelewa watanzania ni kuwa unaweza kuwa na PhD level knowledge kwenye gesi, halafu ukawa na Kindergarten knowledge level kwenye other public policies and social issues. Kwa upande wangu Muhongo uelewa wake wa social issues, uko around grade six at the very best.
Huyu Makamba kwenye Gesi kumlinganisha na Muhongo ni kutaka kumdhalilisha Makamba, kwani ingawa kwenye social issues Makamba anamzidi Muhongo kwa mbali sana, he can't even qualify to be Muhongo's student if we were to enroll Makamba in an Oil and Gas Major at a higher learning institution.
Nilichokiona kwa wanasiasa wetu ni muendelezo wa kudharau wasomi na tafiti kwenye ku-present mada zao. Hivi wanashindwa nini kuunda research team, hata kwa kukusanya interns kutoka UDSM? wanashindwa nini kusema kuwa nimekusanya maoni haya na haya ya wataalamu husika kwenye hili na hili, na nime-comeup with best possible scenario hii na hii kwa tatizo hili na hili?
We need such kind of politician,wanaoweza kutumia resources tulizonazo kuweza kuja na majibu ya matatizo yetu. Hatuhitaji Mr. Know-it-all mwenye muarubaini wa matatizo yetu yote. Tukiendelea kumtafuta huyu mtu tusubiri kuendelea kudanganywa mpaka basi.