Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Muhongo ana Kiburi jeuri na dharau, aende akafanye kazi za taaluma Urais hauhitaji wataalam. Kafieni mbele huko na njaa zenu.

Kikwete ni mchumi na ni Rais je uchumi wetu unapaa?

Haha.

Muhongo kwenye gesi sio mtu mzuri wa kubishana nae kwa wanasiasa wa Tanzania, ataisia kukuabisha tu na kukung'ong'a ukose pozi. Give credit where credit is due, he is the most capable among the candidates when it comes to gas vision and knowledge, kwengine it's up for debate.
Wasichoelewa watanzania ni kuwa unaweza kuwa na PhD level knowledge kwenye gesi, halafu ukawa na Kindergarten knowledge level kwenye other public policies and social issues. Kwa upande wangu Muhongo uelewa wake wa social issues, uko around grade six at the very best.
Huyu Makamba kwenye Gesi kumlinganisha na Muhongo ni kutaka kumdhalilisha Makamba, kwani ingawa kwenye social issues Makamba anamzidi Muhongo kwa mbali sana, he can't even qualify to be Muhongo's student if we were to enroll Makamba in an Oil and Gas Major at a higher learning institution.

Nilichokiona kwa wanasiasa wetu ni muendelezo wa kudharau wasomi na tafiti kwenye ku-present mada zao. Hivi wanashindwa nini kuunda research team, hata kwa kukusanya interns kutoka UDSM? wanashindwa nini kusema kuwa nimekusanya maoni haya na haya ya wataalamu husika kwenye hili na hili, na nime-comeup with best possible scenario hii na hii kwa tatizo hili na hili?

We need such kind of politician,wanaoweza kutumia resources tulizonazo kuweza kuja na majibu ya matatizo yetu. Hatuhitaji Mr. Know-it-all mwenye muarubaini wa matatizo yetu yote. Tukiendelea kumtafuta huyu mtu tusubiri kuendelea kudanganywa mpaka basi.
 
Mama kwaiyo hiyo ya songo songo siyo gas??
na inakotumika ina tumika bure!!?
Mama au unamanisha shilingi siyo pesa ni sarafu!!?

Kijana, ni kidogo sana hiyo uzalishwaji wake huwezi kuiuza nje na hauna miundo mbinu ya Gas ya kujaza mimeli ya tanker mikubwa, ambayo inataka ikitia nanga inajazwa masaa machache inaondoka, si rahisi na si mchezzo miundo mbinu yake, kuna kazi kubwa sana itafanyika, subiri usiwe na haraka utaiona.

Hebu tumia fursa ya google, google kidogo Qatar Gas Port au terminal Ujionee.
 
hakuna sera iliyokuwa bora tangu kujitawala kuliko MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ingawaje imeshindikana
 
Nimemsikiliza kwa makini sana bwana january jana wakati wa kutoa hotuba yake.
Ametuvutia wengi kuonyesha nia yake ya kujenga Tanzania Mpya, lakini amenipa maswali kadhaa:
1. Ni kweli TZ ya sasa haina mifumo mizuri ya kusimamia na kuendeleza uchumi wa nchi??
2. Hivi yeye si sehemu ya Tatizo kweli?
3. Hivi historia gani inambeba kumfanya tuamini kweli atafanya anayoyaongea??
4. Je aliyoyasema na wanayosema vyama vya upinzani kuna tofauti gani? kwanini asiseme sasa tuiondoe ccm madarakani?
5. kwanini kakiacha kilimo kama sehemu kubwa ya muajiri kwa watanzania badala yake anasema ujenzi wa nyumba unaweza kuajili watu zaidi ya milioni 5 bila kutambua juhudi za NHC and kuahidi kulisupport shirika hilo badala yake ataweka kitu kingine? anajua kasoro ziko wapi??
6. Hivi vyuo vinazalisha kitu gani mpaka avijengee uwezo wa kukopesha wanafunzi?? kuanzisha mfuko wa mikopo ya wanafunzi tofauti na kubioresha uiliopo kweli ni suluhisho??

nahisi alichofanya january ni sawa na KUMCHUKUA MWANAFUNZI WA CHUO ALIYEMALIZA CHUO AU SHULE BILA KUAJILIWA UMUAMBIE JE UKIWA RAISI UTAFNYA NINI?
maelezo yake ilikuwa ni hadithi za kusadikika.....

la mwisho huwa najiuliza hizi gharama za kufanya haya wanatoa wapi??
hotuba ya january makamba
Ndugu Watanzania wenzangu,
Naomba sasa nifafanue majawabu mapya ambayo Serikali yangu itayatekeleza kwa changamoto mahsusi:
Naomba nianze na suala la ajira. Kwasasa, wapo zaidi ya Watanzania milioni 23 kwenye soko la ajira leo hii. Kila mwaka wanaongezeka vijana zaidi ya laki tisa kwenye soko la ajira.
Hawa ni watu wengi sana. Viongozi wengi wa siasa wameliita tatizo la ajira kuwa ni bomu. Lakini kulielezea tatizo sio kulitatua.
Serikali yangu itafanya nini?
Watanzania wengi wanajishughulisha na biashara ndogo na za kati. Karibu zote zinaajiri mtu mmoja au wawili na nyingi zinasuasua. Watalaamu wanatuambia, asilimia 20 tu ya biashara na kampuni ndogo nchini zikiongeza mfanyakazi mmoja kwa mwaka, ajira 400,000 za kudumu zitazalishwa kwa mwaka. Je asilimia 80 za biashara hizi zikiongeza watu wawili wawili tu kwa mwaka? Tutakuwa tumepunguza sana kama sio kumaliza tatizo la ajira.
Kwahiyo, jawabu letu la kwanza litakuwa ni maendeleo ya biashara ndogo na za kati. Zilizopo zifanye vizuri na kuongeza waajiriwa na wale wanaotaka kuanzisha biashara, iwe rahisi kufanya hivyo.
Ziko namna kadhaa za kufanya hivi. Kwa mfano, katika nchi yetu, Serikali bado ndio mnunuzi mkuu. KIla siku, Serikali yetu inanunua bidhaa nyingi - kuanzia kuni, karatasi, matofali, mabati, vyakula na huduma nyingine nyingi. Katika kuzijengea uwezo kampuni ndogo na za kati, Serikali yangu itaweka Sheria ya kuwezesha asilimia 30 ya thamani ya manunuzi ya umma kupewa makampuni madogo na ya kati yatakayokidhi vigezo rahisi yanayomilikiwa na vijana na wanawake. Jambo hili litawezesha biashara nyingi ndogo kujenga uwezo, kupanuka na kuajiri watu wengi zaidi.
Lakini, ili hili litokee, lazima tuwe na taasisi madhubuti ambayo itashughulika na ustawi wa biashara na makampuni madogo na ya kati.
Kwahiyo, nitaanzisha Mamlaka mahsusi ya Maendeleo ya Biashara Ndogo na za Kati. Pamoja na mambo mengine, Mamlaka hii itapewa majukumu ya kuwezesha, kurahisisha na kusimamia biashara ndogo kuanzishwa kwa urahisi, kuendeshwa bila bughudha, na kupata fursa ya kukua.
Ndugu Wananchi,
Viwanda bado ni tegemeo kubwa la ajira. Kwa viwanda vikubwa vilivyopo sasa, tutaweka motisha ya kikodi kwa yoyote ambaye ataweza kuongeza ajira mpya angalau 500 au zaidi za kudumu kwa mwaka. Haipaswi kumgharimu kikodi mtu mwenye biashara kuongeza wafanyakazi.
Kwa waajiri ambao ni biashara au kampuni mpya ndogo na za kati, yaani SMEs, Serikali yangu itatoa motisha ya kupunguziwa kodi hizi kwa kila kazi mpya tano au zaidi kwa mwaka. Ukweli hapa ni kwamba kunawiri kwa uchumi hakutokani na kodi inayokusanywa na Serikali bali kunatokana na kipato na uwezo wa manunuzi walionao wananchi na kipato cha wafanyabiashara kuweza kukuza biashara zao na kutoa ajira nyingi zaidi.
Vilevile, katika kukabiliana na tatizo hili la ajira, tutawezesha sekta binafsi kujenga na kufufua viwanda vya nguo, katani na korosho nchini. Huko nyuma tulishawahi kuwa na viwanda vingi vya aina hii, vikichangia asilimia 25 ya pato la Taifa na kuajiri asilimia 25 ya wafanyakazi wote nchini. Kwa sasa, ni asilimia 30 tu ya pamba yetu ndio inayotumika nchini. Pamba tunayo ya kutosha kukidhi mahitaji ya viwanda vikubwa zaidi ya hamsini. Ndani ya miaka mitano ijayo tutahakikisha tunajenga na kufufua viwanda 11 vya nguo vitakavyotoa ajira mpya zaidi 100,000 viwandani tu, huku asilimia zaidi ya 80 ya wafanyakazi hawa wakiwa ni wanawake. Lengo ni sekta nzima ya pamba kuajiri walau asilimia 10 ya nguvu kazi (kazi milioni 2.5).
Katika kuwezesha hili, Serikali nitakayoiongoza itachukua hatua za muda mfupi za kikodi na kiushuru ili kuwezesha viwanda hivi kukabiliana na ushindani wa kanga, vitenge, mitumba na vitambaa kutoka nje ya nchi.
ni wazi kabisa january Makamba ndo rais ajayee katika kuijenga tanzania mpya
 
Uyu muongo na hutuba yake haina reality
Jambo jingine kubwa ambalo ningependa kulizungumzia ni tatizo la rushwa. Limezungumzwa na wengi. Lakini kulizungumzia na kulipigia kelele suala la rushwa pekee hakulimalizi. Ziko namna mbili tutakazozitumia kukabiliana na hili tatizo: njia ya kwanza ni kisheria, kimfumo na kitaasisi; njia ya pili ni kijamii.

Kuhusu kimfumo, nitafanya mabadiliko makubwa mawili. Kwanza, ni kuiwezesha TAKUKURU kuwa na mamlaka kisheria ya kuwashitaki watuhumiwa wa rushwa moja kwa moja mahakamani. Pia, tuanzishe Mahakama Maalum ya Uhujumu Uchumi ambayo itahusika na makosa ya rushwa; ubadhirifu wa mali ya umma; ukwepaji kodi; kuiba, kunufaika au kutaka kuiba au kutaka kunufaika na mali ya umma; na makosa mengine ya aina hii.

Mahakama ambayo itakuwa na jopo maalum la majaji ambalo litafanya kazi mwaka mzima na kusikiliza na kuhukumu kesi hizi haraka. Kesi za uhujumu uchumi ziendeshwe wazi na mfululizo na adhabu ziwe kali sana, kwa mfano ya kifungo cha maisha. Pia tutaanzisha Kurugenzi ya Uchunguzi na Mashtaka ya Uhujumu Uchumi. Tutaiwezesha Mahakama hii na Kurugenzi hii bila ukomo wa kirasilimali kuifanya kazi hii vizuri.

Kuhusu kijamii, kwa kushirikiana na viongozi wa dini na wengine wa kijamii, nitaanzisha na kuwezesha mjadala mpana kwenye jamii yetu kuhusu maadili ya jamii. Jamii yetu ijengwe kwenye misingi ya kuchukia rushwa, ulaghai na njia za mkato za kupata mali. Inapofika mahala jamii inasheherekea mali ambazo hazina maelezo, inapofika mahali ambapo jamii inawatukuza wachache ambao wametumia ujanja kufanikiwa, inapofika mahala ambapo jamii inakuita mjinga unapostaafu ukiwa hujilimbikizia mali, hapo lipo tatizo ndani ya jamii. Lazima kujenga jamii tofauti, ambayo wala rushwa wanajiona kama wanatembea uchi, jamii ambayo inatoa adhabu za kijamii, yaani social sanctions, ikiwemo kutengwa, ambazo ni kali kuliko adhabu za kisheria. Mwalimu Nyerere alijaribu kujenga jamii ya aina hii: jamii ambayo kiongozi wa umma hapaswi kungoja mahakama itamke kwamba ni mla rushwa. Tunapaswa kuendelea kujenga jamii ya aina hii. Viongozi wa dini wana nafasi kubwa
 
Huyo January ni muongo, gas itaanza kuinufaisha Tanzania kuanzia kwenye umeme kwanza, halaf itumike viwandani na majumbani, halaf ndo ije kuuzwa, ni process, na kila process ina manufaa yake. Jamani msikilizeni muhongo, ndo maana alisema achaguliwe yeye kwa sababu wengine hawajui na watawadanganya kama huyu

mawazo ya january ni more practical kwa sabb anaongea kitu ambacho anaamini kitawezekana after a certain period of tym kama ni matumizi ya gesi ya uhakika ni baada ya miaka kumi na huo ndo ukweli wenyewe not oherwise....
pili muhongo ndo mwenye sera za uongo coz hakitekelezeki

we need Tanzaniampya na raisi ambaye atatusikiliza wananchi waake
 
Watu wa bumbuli wanashangaa mnavyomshangilia huyo kilaza
kilaza ni wewe usiyeweza kupembua safi na chafu utaatapika tuu unga wa ndere soon nginingi mpya inakuja na itajengwa kwa imani yetu na chaguo sahii january Makamba
 
kilaza ni wewe usiyeweza kupembua safi na chafu utaatapika tuu unga wa ndere soon nginingi mpya inakuja na itajengwa kwa imani yetu na chaguo sahii january Makamba

chaguo sahihi ndo huyu January makamba mpiga chabo maarufu aliyefutiwa mitihani??
 
mawazo ya january ni more practical kwa sabb anaongea kitu ambacho anaamini kitawezekana after a certain period of tym kama ni matumizi ya gesi ya uhakika ni baada ya miaka kumi na huo ndo ukweli wenyewe not oherwise....
pili muhongo ndo mwenye sera za uongo coz hakitekelezeki

we need Tanzaniampya na raisi ambaye atatusikiliza wananchi waake
Ndugu yangu najua unamkubali sana January ila tujadiliane basi sera ipi ya Muhongo uliyoisikiliza ni uongo na haitekelezeki kivipi?
 
kwa nini wanatumia hela nyingi sana kwa zoezi la kutangaza nia? mbona ukiitisha press conference inatosha tu! lakini mbwembwe nyingi utafikiri chama kimeshawateua!
 
MAKAMBA ATAJA KIPAUMBELE CHAKE KATIKA URAIS
Mbunge wa jimbo la bumbuli, JANUARY MAKAMBA Ametangaza rasmi nia yake ya kugombea urais kwa tiketi ya chama chake cha CCM , Iwapo kitampitisha kugombea nafasi hiyo ambayo binafsi amesemma hapambani na mtu bali ni kwa ajili ya kupambana na na changamoto za watu.
hali kadhalika alisema hana shaka ya kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa ndani wa taifa kuwa hana deni lolote hivyo kwa ujasiri mkubwa atapambana nchini iondokane na hangamoto ya rushwa.
Mkamba aliyabainisha hayo Dar es salaam jana wakati akizungumza na watanzania kupitia vyombo vya habari alipokuwa anatangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya uraikizungumza na wananchi alisema kama atapata nafasi ya kuongoza nchini atahakikisha anaondoa changamoto zilizopo kwenye sekta mbalimbali kama aridhi ,elimu na huduma za kijamii
ELIMU
Makamba aloisema sekta ya elimu inachangamoto nyingi sana hivyo serikali yake itahahakikisha inamaliza matatizo hayo.
alisema atahakikisha elimu ya Tanzania inaongozwa na dira ya vijana kujiajiri kudadisi pamoja na kuwepo kwa mitaala mipya
pia alisema serikali yake itahakikisha inamaliza matatizo ya waalimu kwani bila kufanya hivyo elimu bora haiwezi kupatikana
"elimu bora haiwezi kupatikana saikolojia ya waalimu haipo vizuri na hii inatokan na walimu hao kuwa na changamoto mbalimbali za maisha ,kama nikiingia madarakani nitahakikisha mazingira ya waalimu ya kufanyia kazi yanaboreshwa , kuongeza mishahara kupandishwa madaraja na kujengewa nyumba" alisema
mmbunge huyo alisema kila wilaya inakuwa na chuo kimoja cha ufundi ili kuondokana na tatizo la ajira nchini
Alibaiinisha kuwa serikali yake itatoa mfumo mpya ya utoaji mikopo kuwa ya wazi kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kila mtu aweze kupata kupata mkopo unaostahili.
RUSHWA
Watu wengi wanazungumzia rushwa lakini hawzungumzi namna ya kupambana nayo .
Alisema kama akiingia madarakani atapambana na rushwa kisheria , kijamii na kimfumo.
Alibainisha kuwa kimfumo atahakikisha kuwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) inapewa nguvu katika kuwafichua watu wanaojihusisha na rushwa pamoja na kuwachukulia hatua.
kisheria alisema atahakikisha serikali yake inaweka adhabu kali kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo.
vilevile alifafanua kuwa viongozi wa dini , sekta mbalimbali na familia zina haki ya kuwaelimisha wananchi kuhusu athari za Rushwa ili kuondoa jamii ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.
aliweka wazi kuwa kiongozi yeyote anayetaka kuacha historia nzuri anatakiwa kupambana na rushwa
"namna viongozi wanavyotafuta uongozi ndivyo watakavyo tawala hivyo ni vyema wananchi kuwa ,makini katika kuchagua viongozi" alisema makamba.
ARIDHI
Alisema aridhi ni rasilimali kubwa katika kila nchi hivyo atahakikisha kuwa umiliki na matumizi ya aridhi yaanaweka katika mfumo bora .
makamba alisema watu wanatabia ya kuhodhi aridhi kwa matumizi yao . hivyo alisema serikali lazima waanze kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima na maeneo ya hifadhi kwa kuipa hifadhi thamani na kuweka mipika ya aridhi.
HUDUMA ZA JAMII
Aidha alisema kuna changamoto kubwa za huduma ya afya hivyo serikali yake itahakikisha inaendelea kusogeza huduma hizo karibu na wanajamii hasa walio maeneo ya vijijini . sanjari na hayo alisema kila mtanzania anakuwa na bima ya afyab bila kujali uwezo wake
"mimi na serikali yangu tutahakikisha tunaondoa ukiritimba na urasimu wa kusambaza dwa katika kilavituo vyote vya Afya vya serikali " alisema.
MAJI
Kuhusu maji tatizo hilo ni changamoto ni changamoto kubwa katika maeneo ya vijijini hivyo alisema yeye na serikali yake wataanzisha mfuko na wakala wa maji vijijini ili kuondoa tatizo hilo.
UCHUMI
Kuhusu uchumi alisema atahakikisha misingi ya barabara inakuwa imara pia ujenzi wa reli utakamilika ilikurahisisha usafiri utakaokuza uchumi wa taifa .
hata hivyo alisema hayo yote yanaweza kutekelezwa kwa kuondoa misamaha ya kodi ambayo inaweza kuwapata kiasi cha shilingi billioni 860.
alisema ataongeza ufanisi wa kazi kwa asilimia 10 kutoka mamlaka ya mapato TANZANIA (TRA), Ambao utawez kukusanya sh.billion 620 .Kwa upande mwingine alisema kama ardhi itapimwa vizuri na kuhakikisha kila anayemiliki analipa kodi stahiki serikali itaweza kukusanya sh.bilioni 520.Makamba alisema kuna miradi mingi ambayo inaweza kuiingizia serikali fedha nyingi ambazo zinaweza kutatua changamoto izo bila kutegemea fedha kutoka mataifa ya nje
mbali ya hayo alisema pia akiingii madarakani serikali yake itafumua mfumo wote ulliopo na utumishi ilikuondoa urasimu uliokithiri katika sekta ya umma.Alifafanua kuwa mfumo huo utarudisha nidhamu ya kazi ambayo itasaidia kutekeleza mambo yote aliyoyataja .......

Source jambo leo.
 
sikuelewi unachoongea maana kufaidika kwa gesi hakutokani na uzalishaji tu ambapo naona nawe umejikita huko kumbuka uzalishaji ni moja tu ya hatua kuna zingine ambazo kama nchi ilibidi tumeshajipanga kuvuna lakini kwa sababu tuna wanasiasa wasio na vision hii ndio hasara yake. mimi naongea kama mtaalam wa energy maana ndio kazi yangu nitaanza na exploration hapa kuna pesa nyingi kama tungekuwa tumejipanga ktk seismic survey na air transportation, kuna appraisal hapa tungeweza kutengeneza pesa kwy drilling kwa kutumia vijana wetu kufanya core analysis both lab and physical, halafu kwy well completion pia kazi ni nyingi na vile vile stage ya pre development na development hapa ndipo almost 60% of CAPEX inapoishia. Makamba is wrong kwa sababu ameichukua Tanzania more like consumers badala ya participant wa Process nzima.
Mkuu, kwanza nakushauri kanisome hapa, Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- Watanzania Tunaibiwa Mchana Kweupe!....

Kwenye process nzima ya uchumi wa gesi mpaka hapa ninapozungumza Watanzania ni watazamaji tuu na sio players hata kidogo, apart from manual labor!. Nenda Lindi na Mtwara, wenye tenders za supply ya consumables na foodstufs ni Wakenya hadi maji ya kunywa ni kutoka Kenya!. Wenye tender za ulinzi ni makampuni ya Afrika Kusini, sisi tumeelezewa kampuni zetu za ulinzi hazina che capacity!. Kila kitu kingine kinafanywa na wataalamu wao!. Hata kazi tuu ya ku draft hiyo mikataba ya PSA angalau wangepewa wanasheria wetu!, hakuna hata mmoja!, hadi PSA wanatu draftia na kutuletea sisi kazi yetu ni kusaini tuu!.

Tuje kwenye bomba la gesi, kanisome hapa,
[h=3] Bomba la Gesi Mtwara:Kumbe ile "20 -Year Grace Period" ni Kiini Macho Tuu!
[/h]wakati mabomba yanaletwa, wametafuta madereva 100 kutoka Lindi na ,Mtwara wenye class c!, huwezi amini walipatikana wawili tuu!, the rest walitoka Dar kwa malipo kiduchu ajabu!.

All and all kila kitakachopatikana kwenye gesi kujumlisha na muliplied effects yake, hakitakuwa na impact yoyote kwa yule Mtanzania masikini anayeishi kwa less than a dollar a day!. January was very right, tusiandikie mate, tupo tuendelee kukumbushana kuhusu hizi neema za gesi asili!.

Pasco.

 
Rushwa hili limezungumzwa na watu wengi zipo njia nyingi katika kuthibi rushwa zipo njia mbili
Kimfumo mamlaka, kitaasisi

Na mfumo wa kijamii

Kesi za wahujumu uchumi ziendeshwe kwa wazi na zieleweke
Kwa kushirikiana na viongozi wa dini kukemea na kuichukia rushwa kivitendo

Swali kuu walikuwa wapi kuishauri serikali ambayo na wao pia ni sehemu yake? Why tomorrow and not today? Naogopa sana mtu ambaye anakuja kuomba msaada huku akiwa hajafanya chochote in advance. Amefanya nini katika hayo hayo anayoyazungumza wakati akiwa katika nafasi yake ya uwaziri? Nasikitika sana nikikumbuka MB8 na jinsi ilivyokuwa implemented bila hata kutushirikisha watumiaji wa mtandao.
 
hawana akili wapo mirembe au ????
CCM ndo chama mama kwahy hata babu zetu hawakuwa na akili????
watanzania tupunguze uvivu wa kuwapongeza watu wakifanya vyema

CCM ya sasa sio ile ya baba na babu zetu, believe me
 
Alikuwa anasoma kwa kutumia TelePrompter.

Hata hivyo CCM ni waongo tu

Mkuu haya maswala ni mageni sana kwa nchi yetu ndio maana utaona wengi walijua jamaa kameza nondo, lakini kwa nchi zilizoendelea TelePromper imeanzishwa na muigizaji Fred Barton miaka ya 1950, ikatumika kwa mara ya kwanzA 1952 Marekani katika kampeni za kuwania urais na Dwight Eisenhower, kwa msingi huu ndio maana watu wamejikita katika kujadili jamaa amekariri hotuba badala ya kile anachokisema!
 
Wakuu
Sikupata nafasi ya kumsikiliza Mh January makamba wakati anatangaza nia. Watu mbalimbali wanasena aliongea vizuri hivyo na mm nashawishika kuitafuta hotuba yake nisikilize alichokiongea.
Tafadhari naombeni kwa yeyote aliyenayo anisaidie.
 
We kama unaweza kuwa humu jf si utafute youtube au hutaki kuhangaisha akili yako,basi tafuta boyfriend ili awe anakusaidia usituchoshe sie
 
Back
Top Bottom