Kutokana na kupanda kwa gharama za vifurushi, napumzika rasmi kununua vocha na kujiunga na vifurushi kwa muda usiojulikana

Kutokana na kupanda kwa gharama za vifurushi, napumzika rasmi kununua vocha na kujiunga na vifurushi kwa muda usiojulikana

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Moja kwa Moja.

Nina line tatu kila nikichungulia hakuna uafadhali, nilikuwa najiunga halotel kufushi cha Halotel Royal 5K kwa mwezi napata dakika na Mb ambazo zilikuwa zinanifaa kusongesha maisha lakini cha ajabu leo nimekuta wameondoa na cha bei ya chini sio elfu tano tena bali ni elfu Kumi.

IMG_20221104_090503.jpg


Tokea utawala wa awamu ya sita vifurushi vinapanda hovyo sidhani kama imetokea kupita miezi miwili bila kukuta mabadiliko na bei ya vifurushi kuwa ghali, na hali hii imesababisha nishindwe kuchukua maarifa mitandaoni na kupunguza matumizi ili kuendana na hali.

Kutokana na serikali kushindwa kuzuia hali hii nimeamua nipumzike kwa muda kidogo ili kubana matumizi maana mwisho wa siku najikuta natumia gharama kubwa kujiunga mabando.

Nitakuwa naingia mtandaoni nikiwa sehemu ya Free Wi-Fi au nikipata chimbo la Free data Vpn ,dakika na sms bahati nzuri ninazo kutumia mwezi kupitia kifurushi kilichoisha Mb hivyo ni muda muafaka sasa kupumzika kuendana na haki.

Bye bye Jf,Quora , YouTube ,Gugo na chimbo zangu za kuchukua madini.

#UziTayari
 
Mi nimeamua nijiunge na voda supa kasi
 
Wiki ya pili inakaribia sasa nipo ,sio kama sina hela hapana ila sipendi kupandishiwa gharama muda wowote wanaojisikia wao .Ukikaa muda kidogo unakuta vifurushi vimepanda .

Nipo kwenye mgomo mwendo wa kuvizia free Wi-Fi na kutafuta machimbo ya Free VpN
IMG_20221114_175553.jpg
 
Back
Top Bottom