Kutokana na kuwepo kwa taarifa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Mwenyekiti wa Tlp Taifa Augostino Mrema ,hatimaye Mkewe Halima amevunja ukimya kuhusu ndoa yake na Mwenyekiti huyo.
Kwamba hana ugomvi na familia yake na watu waache uzushi wa kumzushia kwamba mumewe huyo mtarajiwa amepata upinzani mkubwa kumuoa yeye .
Amesema kuwa,hana mgogoro wowote na mpenzi wake mtarajiwa wananchi wapuuze maneno yanayosambazwa mtandaoni kwamba yeye na mzee wana mgogoro sio kweli,
Bali familia wanaishi nao vizuri na wala hakuna neno na ameshapewa baraka zote amsaidie baba yao.
Halima amesema suala la ndoa yake kufungwa siku ya alhamisi bado ni mapema sana kusema kwani kipindi hiki ni cha kwaresma hivyo muda ukifika watasema jambo lao ni lini lakini kwa sasa hayupo tayari kusema mambo mengi isitoshe yeye sio mwanasiasa .
Mmoja wa watoto wa mzee Mrema ambaye jina limehifadhiwa amesema kuwa , hawana mgogoro wowote na baba yao kuhusu kuoa kwani mzee Mrema ni mtu mwenye akili timamu na anafanya maamuzi yake vizuri na kama wangeona hayuko sawa wangemshauri kwamba sio jambo jema lakini kuhusu suala la baba yao kufunga ndoa kwa kuoa mwanamke familia imelibariki kwani ni mzee na anahitaji uangalizi wa karibu zaidi.
Hakuna ajabu kwa mzee Mrema, na wazee wengine kama yeye, waliofiwa na wake zai na kuamua kuupiga mwingi na kuoa wake wengine katika maisha yao ya uzeeni. Maamuzi kama haya yanatajwa hata katika maandiko matakatifu. Pengine nukuu yenye kumhusu baba wa imani Ibrahimu inaweza kutufikirisha zaidi;
MWANZO 25
1 Abrahamu alioa mke mwingine, jina lake Ketura.
2 Ketura alimzalia Abrahamu watoto: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.
3 Yokshani alimzaa Sheba na Dedani; wazawa wa Dedani walikuwa Waashuru, Waletushi na Waleumi.
4 Watoto wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Henoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wazawa wa Ketura.
5 Abrahamu alimrithisha Isaka mali yake yote.
6 Lakini watoto wa kiume wa masuria wake akawapa zawadi, na wakati alipokuwa bado hai, aliwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka mwanawe.
7 Abrahamu aliishi miaka 175.
8 Alifariki baada ya marefu na ya fanaka, akajiunga na wazee wake waliomtangulia.
9 Isaka na Ishmaeli, wanawe Abrahamu, wakamzika baba yao katika pango la Makpela, mashariki ya Mamre kwenye shamba lililokuwa la Efroni, mwana wa Sohari, Mhiti.
10 Abrahamu alikuwa amenunua shamba hilo kwa Wahiti. Huko ndiko alikozikwa Abrahamu na mkewe Sara.
Kwa kupitia andiko hilo, tunajifuna ya kuwa mke pekee kwa Ibrahimu alikuwa ni Sara, wengine ijapokuwa aliwaoa nje yake wanatajwa kama ni masuria (concubines), yaani kwa lugha ya kitaa huitwa mahawala.