Je, ni Muongozo wa dini yao unaotokana na maamrisho ya mwenyezimungu yaliyomo kwenye Quran Tukufu,
Nimegundua kuwa wewe huna lengo la kujifunza. Nyuzi zako za zamani nilikuwa nadhani unataka kujifunza, lakini nimegundua hutaki kujifunza. Ulishawahi kuanzisha uzi (upo Jukwaa la Dini) ukauliza kuhusu Sunnah na ukajibiwa. Ila sijui why unauliza swali kama hili tena.
Je, picha za video na mitandao ya kijamii haiwezi kumfanya mwanamke wa Kiislamu kujua nini huwa kinafanyika kwenye maziko ya Kiislamu?
Wanawake kutokwenda kuzika sio kwa sababu walikuwa hawajui/hawajawahi kujua mazishi ya Kiislam. Unafikiri wanawake hawaendi kuzika kwa sababu hawajui mazishi ya Kiislam? Wanawake katika Uislam wanalazimika kuisoma Dini yao kama wanaume. Wanawake wanatakiwa kuisoma Dini yao, hakunaga kauli za "mwanamke hana Dini" katika Uislam. Wanawake pia wanakalifishwa na Shariah za Allah, na kuitekeleza Dini kunahitajika Elimu/kusoma, hivyo nao lazima wasome.
Ila hukmu hutofautiana baina ya wanaume na wanawake katika baadhi ya mambo ya Kishari'ah kwa Hikma ya Allah ambaye kawaumba wanawake na wanaume na anawajua vizuri zaidi. Mfano wote wanapaswa kuswali (wanawake na wanaume) ila kuna hukmu wanatofautiana.
Sio kwamba wanaonewa au kukandamizwa.
Na sio kwamba hawafanyi mambo fulani kwa sababu tu hawajui/hawawezi kujua. Kama unavyotaka kuashiria.
Kukutaarifu tu;
Wanawake wanaosha maiti za wanawake wenzao, bali Mwanamke anaruhusiwa kuiosha maiti ya mumewe, wanawake wanaweza kukafini wanawake wenzao (kuwavika sanda). Wanawake wanaswalia maiti (ya mwanamume au mwanamke), hawaendi tu kuzika makaburini.
Kutokwenda makaburini kuzika isikupe tabu. Kukatazwa wanawake kufanya jambo fulani wala sio ajabu. Hili hata kwa wanaume, kuna mambo wanakatazwa ila wanawake wanaruhusiwa. Mfano ni haramu mwanaume kuvaa dhahabu (hapa duniani) ila ni halali kwa wanawake, ni haramu wanaume kuvaa hariri (hapa duniani) ila ni halal kwa wanawake.
Kuna mambo wanaume wanalazimishwa ila kwa wanawake wamepewa hiari, mfano ni ni LAZIMA mwanaume kuswali Swala ya Ijumaa, ila mwanamke anaweza kuswali Swala ya Ijumaa au akitaka akaswali Dhuhr nyumbani kwake badala ya Swala ya Ijumaa, hiari hiyo hajapewa mwanaume, LAZIMA kwa mwanaume (labda awe na udhuru wa kishari'ah). Ni lazima mwanaume kuswali Swala za Faradhi Msikitini katika Jamaa (isipokuwa anapokuwa na udhuru wa kishari'ah utakaomfanya asiswali Jamaa msikitini) ila sio lazima kwa mwanamke kuswali Jamaa msikitini, ila anaweza kuswali msikitini.
Na mifano mengine mingi.
Hukumu zinaweza kubadilika si kwa jinsia tu, hata mtu mmoja huyo huyo, hukmu katika mambo ya Ibadah zinaweza kubadilika kwake kulingana na hali, mfano; mtu anawajibika kuswali Swala tano za Faradhi, ila anavyoswali akiwa katika hali ya kawaida (mzima na afya) ni tofauti kidogo na atakavyoswali katika hali za dharura kama ugonjwa na safari (kuna tahfifu kapewa), hukmu zinabadilika kulingana na hali yake atakayokuwa nayo na Shari'ah ishaweka bayana katika kila hali.
Uislam sio Dini ya Usawa. Ni Dini ya UADILIFU. Hakuna usawa katika Uislam, kuna Uadilifu.
So usitake kutaka kuleta mambo ya "usawa" yaliyotokana na fikra za watu nje ya Uislam (ambazo ni uongo mtupu na uharibifu).
Tunaridhia Shari'ah kutoka kwa Mola wetu. Na tunasikia na tunatii.
Na Allah ni Mjuzi zaidi.