1gb
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 2,199
- 2,859
I nashangaza mkuu ikiwa kile wanachokatazwa Kwao wana kifanya Kwetu.Hii ndio maana ya kuheshimiana sio kitu cha kushangaa , ukiwa Roma utafanya ya Roma, ukiwa Saudia utafanya ya Saudia
Na hakuna lolote lile linalowapata kwa kusudi la katazo la kwao,we hushangai?
Tukatae tukubali kuna bonde kubwa sana linalo(tu/wa)tenganisha kati ya dini na wenye dini.
BONDE LA WAKATI.
BONDE LA TAMADUNI.
B LA WAKATI.
Wakati ule zamani hizo teknolojia,maarfa,elimu ilikuwa hafifu sana kiasi ambacho kwa kila jambo ambalo wangelifanya lingekuwa chini ya kiwango ukilinganisha na sasa,
Mfano Wakati wao mtu akifariki waislamu ilipaswa maiti asicheleweshwe kuzikwa.
Kwanini,kwa sababu hakukuwa na namna iliyofaa sana kutunza mwili usiharibike kwa muda mrefu.
Na hasa ukizingatia mazingira yao ya Jangwani Joto ni kali sana.
Sasa ukilinganisha na miaka hii unaweza ukaona hakuna sabb ya kukimbizana kuzika ikiwa mwili unaweza kuhifadhiwa kwa siku za kutosha.
Lkn Waislam wanafuata kwa sabb dini imeamuru tayari hapo kuna athari ya bonde la wakati.
Mm naamini laiti kama aliyeamuru maiti asicheleweshwe kuzikwa angezaliwa na kuishi miakahii /zama hizi.
Asinge sema hivi.
B LA TAMADUNI.
Tamaduni za kale kipindi Chao kwa hakika zilikuwa tofauti kabisa na hizi za sasa tulizo nazo.
Utamaduni wa mashariki ya kati ni tofauti kabisa na utamaduni wa Afrika.
Katazo la wanawake kushiriki ktk shughuli za mazishi bila shaka walioandikiwa kwanza ni wanawake wa jamii hiyo ambapo kwa namna moja ama nyingine Kulikuwa na athari kwa mwanamke wa kipindi hicho.
Ndio maana mwanamke wa zama hizi ,kilekile alichokatazwa katika Uislam akija kwenye ukristo kwa kubadili dini au kushiriki mazishi ya jirani yake Mkristo hakuna linalompata/linalomuathiri huyo mwanamke.
Kwa Hivyo washika Dini tunatunza dini, tamaduni ,miiko ya wenzetu na siyo yetu.