Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 6,585
- 10,363
Habari za muda huu wakuu,
Mimi dhehebu langu ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kumekua na utaratibu wetu wa kufuata taratibu na kalenda ya kanisa inavyotaka, ni kitu kizuri sana, lakini naona kuna haja ya kuendana na mabadilko ya technology ilikua kuokoa muda
Mfano
1) Matangazo ya week,
Kwa Dunia ya sasa sidhani kuna umuhimu wa kusoma matangazo wakati kuna namna nyingi ya kuwafikia watu, unakuta baada msomajI matangazo kumaliza kusoma matangazo, Mchungaji naye anakuja tena kutolea ufafanuzi matangazo yale yale (anakazia) hii inachangia muda mwingi kupotea,
2) Usomaji wa lutrujia,
Ifike mahali ibada zetu zisitufunge tushindwe kwenda out of box, kwa dunia ya leo ingepaswa ibada itawaliwe zaidi na kusifu, kuabudu na kujifunza neno la Mungu
3) ibada binafsi zetengewe siku maalumu,
Mfano ibada ya ubatizo wa watoto,ingefaa ziwe nje ya ratiba ya kawaida ya ibada ya jumapili, kama ilivyo ibada ya Ndoa n.k
Lengo la kutoa mapendekezo haya ni kuleta balance katika ibada, tuna amini watu wote wamekuja kwa ajili ya kuabudu na kupata chakula cha kiroho (Neno la Mungu)
Muingiliano wa ratiba nyingi katikati ya Ibada za Jumapili kumepelekea waumini wengi kutoroka ibada, hali inayopelekea baada ya mchungaji kumaliza neno, watu kuanza kuondoka kwa speed, hii hali inaashiria ibada zinakua ndefu kutokana na kuwa na mambo mengi nje ya msingi mkuu wa ibada yani kusifu,kuabudu na kuskiliza neno la Mungu