Si bure, kuna kitu kinachoendelea ndani ya chama hiki kikongwe cha siasa kilichojizolea umaarufu mkubwa wa kisiasa miaka ya nyuma.
Vyombo vya kiuchunguzi wana kila sababu ya kukifanyia uchunguzi wa kina wa kiusalama chama hiki cha siasa, viongozi wake waandamizi na wananchama wake mashuhuri dhidi ya kuhusika kwao kwenye mambo haya, na vyanzo vya taarifa za kihalifu walizonazo hususani kwenye hili la watu kupotea na baadae kukutwa wakiwa wafu. kwa hakika uchunguzi huo unaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutuliza hali ya taharuki wanazoibua chadema kwa jamii na tashwishwi za kiusalama kwa wananchi.
Je, ni kweli wao kama chadema hawahusiki na utekaji huo?
ni vizuri kijiridhisha isije ikatokea Shakahola ya kisiasa ndani ya chadema Tanazania? are these not stage managed political schemes of silencing challengers in party elections?
Pia soma: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Ndani ya chama hicho cha siasa hakuko salama na hakuana utulivu wa kisiasa, joto la uchaguzi ni kali lipo juu mno, taharuki na hali ya kutoaminiani imetanda pakubwa.
Je, hii haiwezi kuwa sababu ya kunyamazishana katika jitihada za kugombania nafasi za uongozi kwa ambao wamekosa uhalali, hoja na hawataki changamoto kwenye sanduku la kura?
Kwa maoni yangu na bilashaka yoyote uchunguzi wa kiusalama ukifanyika ndani ya chama hiki, taharuki hizi zote wanazoibua wenyewe zitakoma, kwasababu kuna wasiwasi na viashiria vya moja kwa moja kwa chama hiki kuhusika, lakini ili kujiridhisha ni muhimu sana kuchunguza.
Mungu Ibariki Tanzania.
Matukio mengine ya utekaji yakihusisha watu wasiyojulikama soma Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana