Kutokea Dar to Mwanza ipi njia fupi kati ya kupita Dodoma au Arusha

Wewe huna hata google map ukaangalia kabla ya kuuliza JF? Hiyo smartphone ni ya kazi gani kama kitu kidogo kama hicho umeshindwa kupata jibu... unakera mno.
 
Kama ni adventure pitia arusha, babati, singida. njia iko poa sana na utapata view nzuri. ila kama ni pilikapilika we pita zako moro, dodoma singida.
 
Inahusiana nini? Ndo maana umelambwa ban
 
Habari wanaJF, naomba kuuliza kama natokea Dar kwa Gari ndogo kuelekea Mwanza ipi njia fupi kati ya kupita Dodoma au Arusha, japo njia ya Dodoma niliishapita mara kadhaa ila Arusha bado

Nategemea michango yenu wakuu
Panda ndege.
 
Tabora-Nzega hakuna magari kabisa,nimepita mwaka jana ila lami siyo smooth kama zingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…