Kutokutunzwa kwa kumbukumbu za nchi ndiko kunakosababisha Magufuli aonekane Shujaa kuliko wenziwe

Ukimtoa Mwl Nyerere, JPM is the best President kuliko yoyote kwenye kuanzisha miradi mikubwa. Tunaweza hapa kuweka one on one uone! Alafu msisahau katawala awamu moja tu [emoji4]
Nitajie miradi mikubwa mitano aliyoianzisha.
 
Kwani wangapi wanamuombea mabaya magufuli unadhani wao hawajui tutakufa? Mm nimesema kwa mtazamo wangu na sijaona kibaya hapo
Vyeti feki, walamba asali, majizi, mafisadi, wafanyabiashara wa siasa wanajitafutia kipato kwa njia ya halali na isiyo halali,wamefurahia kifo cha Magufuli na bado wanaendelea kumchafua kama wao kifo hakiwahusu
 
Nchi imeendelzwa na wote. Kila.Rais kwa kuwango chake. Wengine hawakulalamikiwa kuja, kutesa, kumpoteza n.k. Mtukuze tu.
Wapumbavu kama nyie ni laana kwa nchi. Waliochota pesa ya escrow walikuwa wanaendeleza nchi?! Swaini jinga wewe.
 
Mradi Gani mkubwa kuliko wote?
JK pekee tu UDOM, Mloganzila, Terminal 3 Airport ya DSM, Bomba la Gesi, Kinyerezi 1 and 2, Mwendokasi, mradi wa kuhamisha Maji ya ziwa Victoria kwenda kati ya nchi, Taasisi ya moyo JKCI, Shule za kata, Lami nchi nzima, Madaraja kama Kigamboni na malagarasi duh hizo za haraka haraka kichwani!!

Hayo angefanya JPM mngemjengea Sanamu!! Mind you JK alifanya hayo yote makusanyo yakiwa chini ya billion 800 kwa mwezi, kukiwa na wafanyakazi hewa na ufisadi wa kutisha!! Imagine Sasa angekua na makusanyo kama ya JPM ya almost trillion 2 kwa mwezi!!!
Bahati nzuri Sana JK anakuwa underrated lakini mzee wa watu hana kisirani. Anatabasanu tu...

Mungu aendelee kumtunza mzee wetu...
 
Magufuli kama McKenzie Kwa kweli
Huwaambii kitu wafuasi wake...
Akitokea mtu akasema wafuasi wa Magufuli wasile chakula mwaka mzima ili afufuke ...mbona tutabaki mdomo wazi...
Ni kama Kibwetere pia. Akiwaambia watu waache mavi yao nyumbani watu wanampigia makofi. Akitaka kumuoza mama yake kwa mahari ya jogoo wanashangilia... Akiwaambia wakinamama kama wanataka kupanuliwa wanaitikia ndioooo....
 
Gagnija ingia kwenye website ya National Beural of statistics kwenye Preliminary results halafu angalia Population Pyramid.

Na takiwmu hizi pia kwamba vijana chini ya miaka 35 ni asilimia 75 ya watanzania wote zimetolewa na Waziri Ummy Mwalimu wakati akielezea ni kwa nini wamempa Diamond ubalozi wa Kupambana na Malaria.
 
Alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, John Pombe Magufuli alitamani kila mradi uitwe kwa jina la Julius Kambarage Nyerere. Ni kama vile aliamini kuwa hakuna aliye bora kati ya Marais watatu wengine waliomtangulia, yaani Ally Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa au Jakaya Mrisho Kikwete.

Hakuna anayebisha kwamba Magufuli alipokuwa Rais wetu, kuna mambo aliyafanya kwa ufanisi na lakini pia isibishiwe kuwa kuna uhalifu pia alifanya. Magufuli alikuwa ni fundi wa kuzuga (Manipulate) akili za baadhi ya watu kiasi kwamba hao watu mpaka sasa wanaamini ni yeye tu aliyekuwa Rais bora kuliko wenziwe wote waliomtangulia.

Nimeona tatizo ni kwamba kwa Mujibu wa takwimu za Sensa za mwaka 2022, wanzania walio chini ya miaka 35 ni sawa na 75%. Kwa maana nyingine wengi wa watu waliopo sasa ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 1987 kuja 2022 wakati sensa inafanyika.

Kwa tafsiri ya Takwimu hizo (HIvi ile sheria ya takwimu ya zama za Magufuli bado iko?) ni kwamba wakati Kikwete anatoka mdarakani mwaka 2015 wengi wa waliozaliwa mwaka 1987 walikuwa wana miaka 28 kushuka chini. Au kwa maana nyingine wao ndiyo walikuwa wapiga kura wa mara ya kwanza mwaka 2005 wakati kikwete anagombea Urais.

Kundi hili kubwa la watanzania (75%) halijawahi kushuhudia Wakati Nyerere, Mwinyi, ama Mkapa wakiwa madarakani. Hawa ndiyo kina johnthebaptist huwafanya mateka kwa kuwaambia kwamba watangulizi wa Magufuli hakuna walichowafanyia watanzania zaidi ya kufilisi nchi.

Kwa kuwa historia imekusudiwa kupotoshwa na kina Countrywide Stroke na wenzao, nchi inakuwa imekwama kwenye kubishana kama Magufuli alikuwa bora kulliko wenziwe na hatatokea tena mwingine kama yeye ama alikuwa sawa tu na wenziwe.

Kutokutunzwa kwa kumbukumbu za nchi yetu, kunasababisha wapiga porojo wa Lumumba ambao walikuwa waimba pambio enzi za Magufuli ambao sasa wamejigeuza kuwa chawa wa Samia Suluhu Hassan, kusema uongo bila ya hofu ya kuumbuliwa.

Ukweli ni kwamba, mpaka Leo hii, mpaka muda huu, Magu ndie the best President, na mama Samia ndie best vice President

Chukua vice wote, hakuna kama mama Samia na chukua marais wote, hakuna kama magufuli huu ndio ukweli

Yule jamaa alikuwa na udhubutu ambao vitu vinaonekana na sio udhubutu wa kwenye makaratasi tu

Jamaa alikuwa na udhubutu wa kuwatoa wafanyabiashara hewa na ambao hawana vigezo vya kufanya kazi wanazofanya kitu ambacho Marais wote walishindwa

Jamaa alikuwa na udhubutu wa kila jambo,
 
Unadhani waliomtangulia walikuwa hawana uthubutu?? Yeye alikuta watu wanaishi maporini? Shule na vyuo alivyosoma alijenga yeye??
 
Kaacha madeni makubwa vile vile na kuvuruga mfumo wa Hifadhi ya jamii. Miradi mingi aliiacha haijakamilika na inakamilishwa sasa. Kwa ivo ukiweka mradi kumbuka weka uliokamilika.

Ubungo interchange ulianza kutekelezwa tangu zama ya Kikwete na ndiyo maana zile nyumba za Ubungo zilibomolewa wakati Kikwete akiwa Rais.

Zama za kikwete ni kwenye makaratasi, ni sawa na daraja la kwenda mafia, lipo kwenye makaratasi tu

Huo mfumo wa hifadhi ulikuwa ni wizi Tu, just emagine ela zako za kustaafu zinaenda kujenga appartment ambazo hakuna mtu anaenda kukaa na zinakuwa magofu je hiyo ni akili?

Ndio maana magu aliwaambia why msijenge viwanda? Nssf wanajenga ghorofa 30 then no wapangaji hiko ndio unataka?

Madeni Kwa serikali za Africa ni kawaida
 
Alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, John Pombe Magufuli alitamani kila mradi uitwe kwa jina la Julius Kambarage Nyerere. Ni kama vile aliamini kuwa hakuna aliye bora kati ya Marais watatu wengine waliomtangulia, yaani Ally Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa au Jakaya Mrisho Kikwete.

Hakuna anayebisha kwamba Magufuli alipokuwa Rais wetu, kuna mambo aliyafanya kwa ufanisi na lakini pia isibishiwe kuwa kuna uhalifu pia alifanya. Magufuli alikuwa ni fundi wa kuzuga (Manipulate) akili za baadhi ya watu kiasi kwamba hao watu mpaka sasa wanaamini ni yeye tu aliyekuwa Rais bora kuliko wenziwe wote waliomtangulia.

Nimeona tatizo ni kwamba kwa Mujibu wa takwimu za Sensa za mwaka 2022, wanzania walio chini ya miaka 35 ni sawa na 75%. Kwa maana nyingine wengi wa watu waliopo sasa ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 1987 kuja 2022 wakati sensa inafanyika.

Kwa tafsiri ya Takwimu hizo (HIvi ile sheria ya takwimu ya zama za Magufuli bado iko?) ni kwamba wakati Kikwete anatoka mdarakani mwaka 2015 wengi wa waliozaliwa mwaka 1987 walikuwa wana miaka 28 kushuka chini. Au kwa maana nyingine wao ndiyo walikuwa wapiga kura wa mara ya kwanza mwaka 2005 wakati kikwete anagombea Urais.

Kundi hili kubwa la watanzania (75%) halijawahi kushuhudia Wakati Nyerere, Mwinyi, ama Mkapa wakiwa madarakani. Hawa ndiyo kina johnthebaptist huwafanya mateka kwa kuwaambia kwamba watangulizi wa Magufuli hakuna walichowafanyia watanzania zaidi ya kufilisi nchi.

Kwa kuwa historia imekusudiwa kupotoshwa na kina Countrywide Stroke na wenzao, nchi inakuwa imekwama kwenye kubishana kama Magufuli alikuwa bora kulliko wenziwe na hatatokea tena mwingine kama yeye ama alikuwa sawa tu na wenziwe.

Kutokutunzwa kwa kumbukumbu za nchi yetu, kunasababisha wapiga porojo wa Lumumba ambao walikuwa waimba pambio enzi za Magufuli ambao sasa wamejigeuza kuwa chawa wa Samia Suluhu Hassan, kusema uongo bila ya hofu ya kuumbuliwa.
Wakili ku manipulate ni kuzuga? Hebu kuwa serious
 
Zama za kikwete ni kwenye makaratasi, ni sawa na daraja la kwenda mafia, lipo kwenye makaratasi tu
Kuna kitu cha serikali hakianzii makaratasini??
Kwani hela za kujenga ile Interchange zilitoka wapi?? Maana mnasifia sana kama vile alitoa hela zake kujengea ile Interchange wakati ni mkopo tutakaoulipa sisi na watoto wetu!!
 
Back
Top Bottom