Kutokutunzwa kwa kumbukumbu za nchi ndiko kunakosababisha Magufuli aonekane Shujaa kuliko wenziwe

Kuna kitu cha serikali hakianzii makaratasini??
Kwani hela za kujenga ile Interchange zilitoka wapi?? Maana mnasifia sana kama vile alitoa hela zake kujengea ile Interchange wakati ni mkopo tutakaoulipa sisi na watoto wetu!!

Huo sasa ndio udhubutu,

Ela ngapi za miradi zimeliwa? Si Bora hata yy amejenga Leo folen ya Kimara imepungua?

Kwani angeamua si angekula Tu kama wengine walivyokula
 
Ukimtoa Mwl Nyerere, JPM is the best President kuliko yoyote kwenye kuanzisha miradi mikubwa. Tunaweza hapa kuweka one on one uone! Alafu msisahau katawala awamu moja tu [emoji4]
Urais si kuanzisha miradi tu , ni pamoja na kuweka usawa ,Haki na kulinda Katiba , Urais si utekaji wala uuaji wala udikteta .

Unapompima kiongozi gusa yote haya

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Nyerere ametawala miaka mingapi? Na magu miaka mingapi?
Na Nyerere katawala kwenye mazingira gani na Magufuli katawala kwenye mazingira gani?

Yaani unataka kumlinganisha mtu ambaye anapokea nchi 90% ya wananchi wa Tanganyika walikuwa hawajui kusoma wala kuandika na mtu aliyekuta nchi ina vyuo vikuu zaidi ya kumi??
 
Kwani angeamua si angekula Tu kama wengine walivyokula
Hebu tueleze hao watangulizi wake walikula nini na yeye hajala nini??

Mambo aliyoyafanya kwa kutumia urais kwa manufaa yake binafsi kuna Rais aliyetangulia anamfikia??

Hivi hela alizokuwa anatapanya angeziingiza kwenye Kilimo ama viwanda leo hii nchi yetu ingekuwa imepiga hatua kiasi gani??
 

Why not?
 

Kula ni kawaida, hakuna rais Africa asiekula ela

But kuna mwingine anakula na kufanya mambo yaende
 
Wewe nawe muongo kama nini,mtu aliyesimamia ujenzi wa barabara nchi nzima katika awamu tatu zote akitekeleza utendaji wa viwango vya juu vya uwaziri katika awamu mbili Kwa miaka 20 unataka kuwa mchoyo .

Wewe unachuki sana tena sana lakini kamwe Kwa Tanzania hii ukimtoa Nyerere Hakuna kiongozi aliyafanya Kwa vitendo Kazi ya uwaziri kumzidi JPM, husimfananishe na wajinga wajinga hata kidogo.


Wewe ebu fikilia miaka mitano tu, ameweza kusomesha wanafunzi bila ada,JNHP,MFUGALE,KIJAZI,NJIA NANE,TANZANITE,JPM BRIDGE,MASOKO ya MADINI,UKUTA MERELANI,ZAHANATI kila Kijiji, ,STAND kila mkoa,umeme vijijini, ndege,mapato kuongezeka kutoka 800b Mpaka 1.5t,uanzishwaji wa viwanda vya uchenjuaji Dhahabu,mapato ya madini yamepanda,tanzanite inauziwa Tanzania na Tanzania ndio kinara sio India au Kenya,barabara kwenye Miji midogo yote,taa barabarani Miji yote, ujenzi wa vivuko nchini Ni Tanzania ni vitu vingi sana siwezi kumaliza.
 
Kaka JK Nyerere alifanya Kwa miaka mingapi?
Swali zuri.

Nyerere alikaa Madarakani kwa miaka 23.

Sasa unapotaka kuwalinganisha si lazima uwa na kigezo cha katikati (median factor) lazima iwe ni usawaziko (Ratio) inayohusu mambo ya msingi.

Kwa mfano unapompima Mwalimu aliyetoka kwenye Urais mwaka 1995 na Magufuli aliyeingia Madarakani miaka 30 (2015) baadaye ni lazima uwe na kigezo cha katikati, ambacho kwa msingi huu ni jinsi walivyotatua matatizo ya wananchi na matatizo hayo waliyatatua katika mazingira gani.

Kwa ivo huo utofauti tu wa miaka toka Mwalimu atoke madarakani mpaka Magufuli kuwa Rais, unaweza kukupa picha kwamba hawa watu wawili kimantiki hawawezi kufananishwa kuwa mazingira na zama zao za kiuongozi hazifanani kabisa!!
 
Wewe nawe muongo kama nini,mtu aliyesimamia ujenzi wa barabara nchi nzima katika awamu tatu zote akitekeleza utendaji wa viwango vya juu vya uwaziri katika awamu mbili Kwa miaka 20 unataka kuwa mchoyo .
Kwa nini hizo barabara zilizojengwa enzi Mkapa na Kikwete wakiwa Marais hamuwataji wao badala yake mnamtaja aliyekuwa Waziri ila yeye alipokuwa Rais hamuwataji mawaziri wake??

Yaani madaraja yaliyojengwa wakati Magufuli akiwa Rais mnasema kuwa "Bila yeye" yasingejengwa, ila hamtaki kusema bila Mkapa na Kikwete hizo barabara zisingejengwa. KWA NINI??
 
Kwa Sababu yeye alisimamua kikamilifu ndio maana watu tunaamini yeye ndiye alifanya vikawa ,ndio maana enzi hizo uwezi Kuta magufuli akifokewa au kuulizwa kama ambavyo yeye alikuwa akiwafokea mbarawa na Yule Mzee Wa mpanda.
 
Kwa Sababu yeye alisimamua kikamilifu ndio maana watu tunaamini yeye ndiye alifanya vikawa ,ndio maana enzi hizo uwezi Kuta magufuli akifokewa au kuulizwa kama ambavyo yeye alikuwa akiwafokea mbarawa na Yule Mzee Wa mpanda.
Atafokewaje wakati waliokuwa Marais hawakuwa na tabia ya kufokea watu hadharani. Yale mambo ya kufokeana uliyaona kafanyiwa nani wakati Mkapa na Kikwete wakiwa Marais!!??

Kwa ivo kwa Magufuli kutokufokewa ni kwa sababu waliokuwa marais walikuwa ni watu waungwana wenye kuheshimu utu wa wasaidizi wao na siyo kwamba alikuwa hakosei au alikuwa bora zaidi ya Marais wake.
 
Unafikiri kwa

Unafikiri kwa nini kutokutunzwa hizo kumbukumbu za nchi kusingemfanya mwingine yeyote(mkapa,kikwete ama mwinyi) kuonekana shujaa na badala yake awe yeye JPM?
 
Unamlinganisha mtu aliyejenga viwanda nchi nzima vikaja kuuzwa na Mkapa, na huyu mnayetaja kwa mambo ya daraja na miradi ambayo hakuna alioacha umekamilika na sasa inakamilishwa na Samia Suluhu.
Kimsingi magufuli alitaka watanzania wafanye mambo mengi wenyewe ili kujikomboa kuwa tegemezi wa ujuzi ndio maana alikuwa anasisitiza kufanya Kazi na miladi mingi ilijaa wazawa na akawa anawaandaa watanzania kujitegemea.
 
Unafikiri kwa


Unafikiri kwa nini kutokutunzwa hizo kumbukumbu za nchi kusingemfanya mwingine yeyote(mkapa,kikwete ama mwinyi) kuonekana shujaa na badala yake awe yeye JPM?
Kwa mfano tulikuwepo wakati Mkapa anapokea nchi toka kwa Mwinyi tulimuona kuna mambo makubwa sana kayabadilisha kwenye utumishi wa Umma kama ambayo Mwinyi alivyobadilisha mambo mengi sana kwenye uchumi au Mkapa ambaye alileta nidhamu ya ukusanyaji fedha za umma kwa kuunda TRA.
 
Wewe ukatae au ukubali hakuna wa kumfikia na inaeleweka wazi mara zote watu wanaopenda matokeo hawapendi michezo kazini fuatilia hata kazini kwako JPM alikuwa mpenda matokeo ndio maana aliamua na ikawa wewe endelea na roho mbaya yako na tunamjua mwingine ambaye anapenda matokeo yupo Zanzibar Ila yeye anahuruma kidogo,akimaliza mama najua atafika TU.
 
Wannaomponda magufuli huwa siwaelewi kabisa mm nimeshuhudia vizuri utawala wa mwinyi na nlianza kupiga kura yangu kipindi cha pili cha mkapa. Kipindi cha nyerere pia nlikishuhudia japo sikuwa na akili ya kuelewa vitu. Kwangu mm magu alikuwa bora kuliko wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…