Kutokuungwa mkono Bashiru, Polepole, Ndugai na wengine, tujitathmini

Ni kweli watanzania ni waoga na hawaungi mkono harakati za ukombozi. Lakini ni mwendawazimu tu ndio anaweza kuwaunga mkono hawa wanasiasa wa kitanzania!

Wote hao uliowataja, walikua kimya wakati dola iko upande wao. Bashiru na Polepole ilifikia hatua wakajiona kama miungu watu hapa Tanzania. Hawakukemea uovu, bali waliunga mkono na kusifia uovu. Pia wakajitokeza hadharani kuwakemea wale walioonekana kuupinga huo uovu.

Leo hii wanageuka kua wanaharakati kwakua dola haiko upande wao tena. Ni mahasimu wao ndio wanaofaidi keki ya taifa. Harakati zao zimejengwa juu ya msingi wa kinyongo na visasi. Hawako hapo kutetea maslahi ya nchi, wako hapo kuwapinga waliowapora ulaji!

Unaanza vipi kumuunga mkono mtu wa aina hii?
 

Kenya wanaweza vipi ku focus kwenye agenda wala si watu?

Siasa za chuki: Tanzania tunakwama wapi?

Tungali na safari ndefu sana.

Elimu kwa watu kuhusu agenda ingali sana.
 
Unanisikitisha kwa kuona Ndugai, Polepole na Bashiru ndio wa maana. Chaguzi za magumashi na katiba mbovu ujashangaa kuona watz wameyakalia kimya?
 
Unanisikitisha kwa kuona Ndugai, Polepole na Bashiru ndio wa maana. Chaguzi za magumashi na katiba mbovu ujashangaa kuona watz wameyakalia kimya?

Tunayo safari ndefu sana kuwa na mliojawa chuki hivi ati kwamba nanyi mko upande wa kupigania katiba mpya. Ikumbukwe CCM wanafurahishwa mno na mawazo kama yako. Au nawe ni mmoja wao na hii ni janja ya nyani tu?

Kama ni furaha kuu mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja akitubu, kwanini isiwe furaha kwetu kama uliowataja wakijua walipopotoka?

Kwani wewe na yule mwana mwema aliyechukizwa na mwana mpotevu kurejea nyumbani kwa babaye mna tofauti gani?

NInakazia:

Katiba Mpya haitakuja kwa Maneno Matupu
 
Kuwa na akili hata kidogo. Hao wanayaongea hayo kwasababu wamekatwa mikia. Wangekuwa ni watu wakweli na safi, wangeyaongea hayo wanayoyaongea sasahivi hata ktk kipindi kile ambacho walikuwepo madarakani
 
Pole sana sukuma gang maana sasahivi mmejikuta mmekuwa wapinzani ambao hawana mshiko

Umesikika sukuma genge. Kwani ni nadra kwa mwizi kupiga ukelele wa mwizi kila anapoitishwa wizi wake?

Kwa taarifa yako hatudanganyiki!
 
Mandela alishirikiana Hadi na kina Buthelezi.

Kenya nao ndiyo hao. Siasa zetu za chuki Zina tija gani?

Siasa za chuki: Tanzania tunakwama wapi?
Ila mkuu ukizungumzia siasa za chuki naona hata wewe mkuu unatakiwa ujitoe kwenye hizo siasa za chuki, nikijaribu kukumbuka wakati ule wa Magufuli hasa kipindi kile cha corona naona kabisa ilikuwa ni zaidi ya kukosoa.
 
Ukikumbuka ya mwendakuzimu na jinsi walivyokuwa wanayachekelea na walivyokuwa wanajimwambafai kwa kweli kuwaunga mkono inakuwa ngumu mno hata kama wakisema kipi cha maana
Kwahiyo una kinyongo?
 
Naamini Dr. Bashiru ataendelea kubaki na msimamo wake, hii itafaa sana kuweka rekodi sahihi mbele ya safari, na hata hao wenye ubinafsi, wanaoiwekea demokrasia masharti, naamimi nao iko siku wataamka.
Dr Bashiru ana msimamo gani? Au kuna Dr Bashiru Wawili?

Huyu chawa wa Magufuli ana msimamo upi?
 
Dr Bashiru ana msimamo gani? Au kuna Dr Bashiru Wawili?

Huyu chawa wa Magufuli ana msimamo upi?

Kama nawaona ma CCM yanavyochekelea kwa kuicheza ngoma yao bila hata kuchezeshwa. Mungu ayape nini?
 
Hatuwezi kuwaunga mkono machawa wa Magufuli.

Wasulubiwe.

Misahafu inaandikab dhambi nyekundu kama bendera zaweza kusafishwa kuwa nyeupe kama theluji.

Kabila gani wewe? Huko kwenu hakunaga toba?

Zingatia kuwa una msimamo kama wa ma CCM. Bado hujishangai?
 
Hakuna alioomba toba kati ya hao sanasana kinachoonekana wanasumbuliwa na njaa

Maneno ya huyu nguli yana maana yoyote kwako?

Your browser is not able to display this video.


Au nguli ni wewe sasa na huyu mwamba anatwanga maji kwenye kinu tu?
 
Misahafu inaandikab dhambi nyekundu kama bendera zaweza kusafishwa kuwa nyeupe kama theluji.

Kabila gani wewe? Huko kwenu hakunaga toba?

Zingatia kuwa una msimamo kama wa ma CCM. Bado hujishangai?
Huyu chawa wa Magufuli aliomba Toba lini? Ipo siku mtaanza kumtetea mpaka Makonda.

Hawa watu wameumiza sana watu na wamewasababishia madhira makubwa.

Hawa ndio kwa hakika wanamjuwa nani alimpiga risasi za kikatili vile Tundu Lisu.

Ni utaratibu wa dunia nzima utawala wowote wa kifashisti kama wa hawa washamba wa kihutu unapoangushwa wale viherehere wote ni lazima watiwe adabu.

Soma historia ya utawala wa kifashisti wa Bolshevik ulipoangushwa wale machawa wote walifanywa nini? Au angalia utawala wa Saddam Hussein ulipoangushwa ni nini kilifuata?

Sisi tunatumia sheria za Musa za torati ni jino kwa jino ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…