Kutokuungwa mkono Bashiru, Polepole, Ndugai na wengine, tujitathmini

Kutokuungwa mkono Bashiru, Polepole, Ndugai na wengine, tujitathmini

Ni kweli watanzania ni waoga na hawaungi mkono harakati za ukombozi. Lakini ni mwendawazimu tu ndio anaweza kuwaunga mkono hawa wanasiasa wa kitanzania!

Wote hao uliowataja, walikua kimya wakati dola iko upande wao. Bashiru na Polepole ilifikia hatua wakajiona kama miungu watu hapa Tanzania. Hawakukemea uovu, bali waliunga mkono na kusifia uovu. Pia wakajitokeza hadharani kuwakemea wale walioonekana kuupinga huo uovu.

Leo hii wanageuka kua wanaharakati kwakua dola haiko upande wao tena. Ni mahasimu wao ndio wanaofaidi keki ya taifa. Harakati zao zimejengwa juu ya msingi wa kinyongo na visasi. Hawako hapo kutetea maslahi ya nchi, wako hapo kuwapinga waliowapora ulaji!

Unaanza vipi kumuunga mkono mtu wa aina hii?
 
Kenya wanaweza vipi ku focus kwenye agenda wala si watu?

Siasa za chuki: Tanzania tunakwama wapi?

Tungali na safari ndefu sana.

Elimu kwa watu kuhusu agenda ingali sana.
 
Haki ni haki bila kujali maslahi binafsi ya awaye yote. Kwa bahati mbaya tumekuwa wabinafsi tusiotaka kuwa sehemu ya kupigania haki hizo.

Tumekuwa kama wapenzi watazanaji wengine wanapojaribu kuuwasha moto.

Imekuwa fulani kasema hivi, fulani kasema vile. Sisi tumesema nini fulani anaposema la maana hata kama hatumpendi? Hatuna hata kauli za mshikamano?

Izingatiwe zimekuwapo kauli nzito za maaskofu kama Mwingira, Shoo na hata mzee wa Upako au Sheikh Ponda. Kwani kulikuwa matamshi hata ya mshikamano tu kutokea wapi?

Kwa hakika kama watanzania tuna matatizo mtambuka tena yaliyo endelevu:

1. Siasa za Chuki, Tanzania tunakwama Wapi?

2. Tuungane mkono dhidi ya Kunyamazishwa

3.Msamaha kubutuliwa, Ndugai aungwe mkono

4.Kujiuzulu kwa Ndugai: Hongereni CHADEMA na NCCR japo haikutosha

5.Aungwe Mkono Askofu Mwingira kukemea Maovu

7. Mizengo Pinda: Tuanze mchakato wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi

8.Katiba Mpya haitakuja kwa Maneno Matupu

Hawakuungwa mkono kina Ndugai, Polepole, Pinda, Kitila Mkumbo na leo tunayaona kwa Bashiru.

Ukombozi ni jitihada za wote waliokuwamo na hata wasiokuwamo.

Ukombozi si suala binafsi au watu fulani ati kwamba ni hao tu from the scratch.
Unanisikitisha kwa kuona Ndugai, Polepole na Bashiru ndio wa maana. Chaguzi za magumashi na katiba mbovu ujashangaa kuona watz wameyakalia kimya?
 
Unanisikitisha kwa kuona Ndugai, Polepole na Bashiru ndio wa maana. Chaguzi za magumashi na katiba mbovu ujashangaa kuona watz wameyakalia kimya?

Tunayo safari ndefu sana kuwa na mliojawa chuki hivi ati kwamba nanyi mko upande wa kupigania katiba mpya. Ikumbukwe CCM wanafurahishwa mno na mawazo kama yako. Au nawe ni mmoja wao na hii ni janja ya nyani tu?

Kama ni furaha kuu mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja akitubu, kwanini isiwe furaha kwetu kama uliowataja wakijua walipopotoka?

Kwani wewe na yule mwana mwema aliyechukizwa na mwana mpotevu kurejea nyumbani kwa babaye mna tofauti gani?

NInakazia:

Katiba Mpya haitakuja kwa Maneno Matupu
 
Tunayo safari ndefu sana kuwa na mliojawa chuki hivi ati kwamba nanyi mko upande wa kupigania katiba mpya. Ikumbukwe CCM wanafurahishwa mno na mawazo kama yako. Au nawe ni mmoja wao na hii ni janja ya nyani tu?

Kama ni furaha kuu mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja akitubu, kwanini isiwe furaha kwetu kama uliowataja wakijua walipopotoka?

Kwani wewe na yule mwana mwema aliyechukizwa na mwana mpotevu kurejea nyumbani mna tofauti gani?

NInakazia:

Katiba Mpya haitakuja kwa Maneno Matupu
Kuwa na akili hata kidogo. Hao wanayaongea hayo kwasababu wamekatwa mikia. Wangekuwa ni watu wakweli na safi, wangeyaongea hayo wanayoyaongea sasahivi hata ktk kipindi kile ambacho walikuwepo madarakani
 
Pole sana sukuma gang maana sasahivi mmejikuta mmekuwa wapinzani ambao hawana mshiko

Umesikika sukuma genge. Kwani ni nadra kwa mwizi kupiga ukelele wa mwizi kila anapoitishwa wizi wake?

Kwa taarifa yako hatudanganyiki!
 
Ukikumbuka ya mwendakuzimu na jinsi walivyokuwa wanayachekelea na walivyokuwa wanajimwambafai kwa kweli kuwaunga mkono inakuwa ngumu mno hata kama wakisema kipi cha maana
Kwahiyo una kinyongo?
 
Naamini Dr. Bashiru ataendelea kubaki na msimamo wake, hii itafaa sana kuweka rekodi sahihi mbele ya safari, na hata hao wenye ubinafsi, wanaoiwekea demokrasia masharti, naamimi nao iko siku wataamka.
Dr Bashiru ana msimamo gani? Au kuna Dr Bashiru Wawili?

Huyu chawa wa Magufuli ana msimamo upi?
 
Dr Bashiru ana msimamo gani? Au kuna Dr Bashiru Wawili?

Huyu chawa wa Magufuli ana msimamo upi?

Kama nawaona ma CCM yanavyochekelea kwa kuicheza ngoma yao bila hata kuchezeshwa. Mungu ayape nini?
 
Hatuwezi kuwaunga mkono machawa wa Magufuli.

Wasulubiwe.

Misahafu inaandikab dhambi nyekundu kama bendera zaweza kusafishwa kuwa nyeupe kama theluji.

Kabila gani wewe? Huko kwenu hakunaga toba?

Zingatia kuwa una msimamo kama wa ma CCM. Bado hujishangai?
 
Hakuna alioomba toba kati ya hao sanasana kinachoonekana wanasumbuliwa na njaa

Maneno ya huyu nguli yana maana yoyote kwako?

Au nguli ni wewe sasa na huyu mwamba anatwanga maji kwenye kinu tu?
 
Misahafu inaandikab dhambi nyekundu kama bendera zaweza kusafishwa kuwa nyeupe kama theluji.

Kabila gani wewe? Huko kwenu hakunaga toba?

Zingatia kuwa una msimamo kama wa ma CCM. Bado hujishangai?
Huyu chawa wa Magufuli aliomba Toba lini? Ipo siku mtaanza kumtetea mpaka Makonda.

Hawa watu wameumiza sana watu na wamewasababishia madhira makubwa.

Hawa ndio kwa hakika wanamjuwa nani alimpiga risasi za kikatili vile Tundu Lisu.

Ni utaratibu wa dunia nzima utawala wowote wa kifashisti kama wa hawa washamba wa kihutu unapoangushwa wale viherehere wote ni lazima watiwe adabu.

Soma historia ya utawala wa kifashisti wa Bolshevik ulipoangushwa wale machawa wote walifanywa nini? Au angalia utawala wa Saddam Hussein ulipoangushwa ni nini kilifuata?

Sisi tunatumia sheria za Musa za torati ni jino kwa jino ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Back
Top Bottom