Kutokuwepo kwa Mabalozi wa US, UK, Sweden, Norway, Denmark, EU, Japan na South Korea leo Dodoma, kuna nini kinaendelea jikoni?

Naona mmeanzisha uzi wa kujifariji! Hivi TL wenu si yupo ubelgiji kaunganeni nae huko sisi ni Nchi huru!.Hivi kwa akili zenu mnategemea hao mabeberu wenu watawasaidia? ,kutokuudhuria kwao si kitu kwetu!.Haizui sisi kuendelea na mambo yetu!.
Payuka tu, kesho Kabudi anaanza ruti za kwenda huko kuomba misaada.
 
Ndivyo walivyo lelewa bila ya vitisho wanaona ujumbe hautofika

Haya ndio matatizo ya kufikisha ujumbe kwa kumpiga mtoto..

Mungu tusaidie Waafrika chini ya jangwa la Sahara..
 
Kwani hao wazungu mnaowasifu na kuwasujudu kila siku humu ndani jf ni akina nani hapa duniani. Msituchoshe hebu .
 
Magu aliwatangazia,aliwahakikishia kuwa Uchaguzi utakuwa huru na wa haki..

Kawatia changa la macho,wamemkasitikia
Hawawezi kuzuia sisi kuendelea na mambo yetu! Kutumia fedha za ndani katika Uchaguzi nu kielelezo kuwa sisi ni Nchi huru!
 
Kwa ukilaza wako unadhani pesa ya umeme vijijini ni ya kwetu???
Wewe unadhani ya nani jinga wewe,
Pesa ni zetu na ndio maana ulisikia siku ila hata raisi alimwambia karemani aonane na waziri pesa itoke umeme uwekwe kwani ulisikia anaomba kwa jirani?
Jitambue
Hii dunia hakuna cha bure
 
Hawawezi kuzuia sisi kuendelea na mambo yetu! Kutumia fedha za ndani katika uchaguzi nu kielelezo kuwa sisi ni Nchi huru!
Kweli,sisi ni nchi huru,yenye uchumi wa kati..

Yenye kuiba kura wakati wa Uchaguzi,yenye kuonea watu wake,kuwanyima Uhuru wa kuamua ...NK

Mkuu,bado hatuko huru,bado hatujitambui, bado hatujaweza kujitawala..
 
Hafla muhimu zaidi kwa balozi kuhudhuria kuonesha ishara ya urafiki na ushirikiano na serikali iliyoingia madarakani ni ile ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais. Balozi zote zilihudhuria hafla hiyo. Hili la ufunguzi wa Bunge halina kipaumbele kikubwa kidiplomasia
 
Achana na watu kama hawa. Sikio la kufa halisikii dawa.
 
Usiseme Wazungu,sema Mabeberu!
 
Huyo amejiunga oct 2020. Anajua amejiunga kwa lengo gani. Acha kumpaisha. Just bonyeza ignore
 
Kuna kitu nahisi kinakuja, na si cha kawaida kwa kweli. Sie tulioibiwa Uchaguzi nafikiri huu ni muda sahihi kuchukua popcorn na kuangalia huu mchezo unavyozidi kuwa mtamu
Utasubiri sana na hio popcorn yako hutapata chochote.

Fanya mambo yako tu.

#PoleniUpinzani


#LoserLissu
 
Hayo ndio mambo yamelichelewesha bara la Africa kujiamlia mambo yake na kujitegemea!!

Misaada misaada, hata kwangu binafsi siitaki, kubebwa bebwa kumelifanya hata soka letu liwe la hovyo hovyo, tunakuwa na timu nzuri ndani Tu kwa sababu ya kubebwa bebwa tu! Ni wakati wa kuonyesha uwezo wetu sasa bila kuwategemea hao ambao mpaka leo wao wanaliwa na Corona

Tanzania bila wazungu, inawezekana bhana, Isipokuwa, Tanzania bila Mungu, haiwezekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…