Ni swali muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
Amani iwe nanyi wadau!
Usiku wa Jana, Wakili Robert Amsterdam ameitaarifu dunia kupitia Twitter yake kuwa amefikia hatua nzuri kupeleka mashtaka katika mahakama ya ICC Uholanzi dhidi ya Magufuli na Serikali yake.
Leo alfajiri, Magufuli akateua mawaziri wawili -- wa Mambo ya Nje, na wa Fedha.
Muda mchache uliopita kwa mara ya kwanza, wawakilishi wa nchi zinazoisadia zaidi Tanzania kifedha na kimisaada yaani Marekani, Uingereza, Sweden, Norway, Japan, Ujerumani, Finland, Korea ya Kusini na Umoja wa Ulaya hawajaudhuria hotuba ya Rais Magufuli Bungeni.
Naomba mnaojua mtuelezee humu, kuna nini kinaendelea jikoni? Au ndo mambo yashakuwa mambo?
Naomba michango yenu!