Kutokuwepo kwa Mabalozi wa US, UK, Sweden, Norway, Denmark, EU, Japan na South Korea leo Dodoma, kuna nini kinaendelea jikoni?

CHADEMA achen uoga.......Tanzania ni nchi huru
Shida ni kuwa kuna watu wanaodhani bila wao tanzania itaanguka, itakufa, haiwezekani, haitaenda, itapigana, itatengwa, haitajulikana, nk. Huu ni puuzi sawa na upuuzi mwingine tu.

Nchi itakwenda kwa kupokezana vyama, mwingine akikosea mwingine anarekebisha kama vile Democratics na Republican, labour na conservative, nk
 
Ni swali muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu.

Amani iwe nanyi wadau!

Usiku wa Jana, Wakili Robert Amsterdam ameitaarifu dunia kupitia Twitter yake kuwa amefikia hatua nzuri kupeleka mashtaka katika mahakama ya ICC Uholanzi dhidi ya Magufuli na Serikali yake.

Leo alfajiri, Magufuli akateua mawaziri wawili -- wa Mambo ya Nje, na wa Fedha.

Muda mchache uliopita kwa mara ya kwanza, wawakilishi wa nchi zinazoisadia zaidi Tanzania kifedha na kimisaada yaani Marekani, Uingereza, Sweden, Norway, Japan, Ujerumani, Finland, Korea ya Kusini na Umoja wa Ulaya hawajaudhuria hotuba ya Rais Magufuli Bungeni.

Naomba mnaojua mtuelezee humu, kuna nini kinaendelea jikoni? Au ndo mambo yashakuwa mambo?

Naomba michango yenu!
Yani bado kuna wapuuzi wanaamini wazungu ndo suluhisho ya maisha ya waafrika...kama wanajali sana kwanini wasiende kumshtaki Trump ambaye kagoma kutoka Ikulu
 
Nachojua bado kuna korona,hivyo wamezingatia usalama wa afya zao. Hotuba wameitazama luningani.

Subiri tweets zao kuonesha wanaunga mkono harakati za serikali hii.
 
Wakati anahutubia na baada ya hotuba,mkulu hakuwa na uso wa bashasha,alionekana hana raha na mwenye feelings nyingi,japo mzee wa mjengoni na gwajboy walichombeza vijembe vingi kwa upande ule ulioshindwa lakini mkulu alikunja viganja vya mikono na kuonekana anaomba Mungu amsaidie kwa magumu yajayo.Kwa kweli politocal strategic iliyotumika kupata ushindi wa kimbunga dhamiri zao zinawahukumu mpaka wanakosa furaha na matokeo ya ushindi mnono

You can fool some people for sometime but you can't fool all the people all the time.
Nimeanza na msemo huu wa Kiingereza kutaka kuweka msistizo wa kile ninachosema. CCM na Magufuli wanadhani wanaweza kuendelea kuwadanganya Watz na dunia nzima kwa siku zote...jambo ambalo halitawezekana asilan!
Huwezi kushinda kwa asilimia 84.4 Urais na Ubunge zaidi ya 95%!
Unless utuambie hii ni nchi yenye kufuata mfumo wa chama kimoja!!!!!
 
Ndugu mie ni mpambanaji kweli. Pamoja na kuwa mwanasheria na Wakili , ni mwekezaji mzuri wa kilimo huku Ruvuma na kule Katavi. Sitegemei ndugu ila sina shida na vikwazo kwa sababu watanzania tukipigwa vikwazo wajinga walio wengi wataamka na kuacha kuwa misukule ya Ccm.
Unamaanisha mwanasheria usie na muhuri au?
 
You can fool some people for sometime but you can't fool all the people all the time.
Nimeanza na msemo huu wa Kiingereza kutaka kuweka msistizo wa kile ninachosema. CCM na Magufuli wanadhani wanaweza kuendelea kuwadanganya Watz na dunia nzima kwa siku zote...jambo ambalo halitawezekana asilan!
Huwezi kushinda kwa asilimia 84.4 Urais na Ubunge zaidi ya 95%!
Unless utuambie hii ni nchi yenye kufuata mfumo wa chama kimoja!!!!!
You nailed it mkuu.
 
Ni swali muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu.

Amani iwe nanyi wadau!

Usiku wa Jana, Wakili Robert Amsterdam ameitaarifu dunia kupitia Twitter yake kuwa amefikia hatua nzuri kupeleka mashtaka katika mahakama ya ICC Uholanzi dhidi ya Magufuli na Serikali yake.

Leo alfajiri, Magufuli akateua mawaziri wawili -- wa Mambo ya Nje, na wa Fedha.

Muda mchache uliopita kwa mara ya kwanza, wawakilishi wa nchi zinazoisadia zaidi Tanzania kifedha na kimisaada yaani Marekani, Uingereza, Sweden, Norway, Japan, Ujerumani, Finland, Korea ya Kusini na Umoja wa Ulaya hawajaudhuria hotuba ya Rais Magufuli Bungeni.

Naomba mnaojua mtuelezee humu, kuna nini kinaendelea jikoni? Au ndo mambo yashakuwa mambo?

Naomba michango yenu!
Balozi wa Somalia alikuwepo?
 
You can fool some people for sometime but you can't fool all the people all the time.
Nimeanza na msemo huu wa Kiingereza kutaka kuweka msistizo wa kile ninachosema. CCM na Magufuli wanadhani wanaweza kuendelea kuwadanganya Watz na dunia nzima kwa siku zote...jambo ambalo halitawezekana asilan!
Huwezi kushinda kwa asilimia 84.4 Urais na Ubunge zaidi ya 95%!
Unless utuambie hii ni nchi yenye kufuata mfumo wa chama kimoja!!!!!
Na uongo unapofika kilele chake hujidhihirisha wenyewe,huleta fadhaa na majuto kwa alioufanya.Uongo una tabia ya kuvuruga rekodi nzuri iliyofikiwa na mtunga uongo na madhara yake ni makubwa
 
Hayo maneno yako ni propaganda za miaka ya 70 ambazo hazifanyi kazi kwenye dunia ya leo. Mzungu akuonee wivu wewe ambae anakujengea hadi vyoo wakati yeye anawaza kwenda kuanzisha maisha sayari ya Mars huko???😂😂😂

Embu kajipange upya
Bado unaendelea kujikomba. Maisha yanaendelea kama kawaida baada ya wakala wa mabeberu kushindwa.
 
Yaani pamoja na matamko yote yale ya kutoridhishwa na namna Uchaguzi ulivyofanyika, ulitegemea waende pale kufanya nini?!

Nakuhakikishia, japo jiwe amejitutumua pale Bungeni, lakini "deep inside" anajua ameharibu, na sijui ataanzia wapi kuwatongoza wale Wazungu.
Wewe unadhani wazungu hao tunahitaji vya kwao sana kuliko wao wanavyo hitaji vya kwetu? Ujinga wetu waafrika upo hapo. Hao wazungu wako ukiwachekea tuu utaambulia mabua;lazima uwakazie waje kwa ustaarabu. Subiri uone mabalozi wanapishana ikulu kujipendekeza.
 
Wanahitaji nini cha kwako ambacho hawana au hawawezi pata sehemu nyingine?
 
Magufuli atumie akili, akijifanya mtemi ataumia hadi hata hao walinzi wake wanaomlinda ataanza kuwaogopa.

Awaombe radhi wapinzani wa kweli kwa hujuma na uhuni aliowafanyia na awaambie walete ankara za gharama zote walizoingia kutokana na huo anaoita uchaguzi kisha awalipe fedha zote walizotumia.

Aache wananchi watunge katiba mpya wanayohitaji bila kuingiliwa na serikali katika mchakato huo. Sheria zote za kijinga alizotunga ili kumsaidia kutawala kiimla zitenguliwe mara moja.

Ianzishwe uchunguzi huru kuhusiana na vitendo vinavyofanywa na genge linalojiita watu wasiojulikana na kuhusika kwao katika shambulizi dhidi ya Lissu na kutoweka kwa watu mbalimbali.

Angalau akifanya hayo ataweza kwa kiasi kikubwa kukwepa balaa la vikwazo ambazo akiwekewa itakuwa ni ndoto kwake kumaliza miaka yake hii mitano akiwa kama rais.
 
Huyu jamaa anajifanya anakiburi sana, sasa acha wenye dunia yao wamfundishe ndo atie akili. Huku ICC inamuhusu, huku vikwazo vinamuhusu. Sasa akae ikulu huku akiwa anawaza anachunguzwa na anaweza kukamatwa muda wowote ili ajue hoe it feels kama anavyonyanyasa wapinzani wake kwa kuwaweka roho juu kila wiki wanaripoti polisi.
 
watubane hadi wajinga waumie
Na hii ndo itaoendeza kweli. Unamkuta mtu anaishi uswahilini mvua ikinyesha hapapitiki kwa sababu ya sera mbovu za Ccm huku hata kipato chake anakipata kwa kudanga kwa sababu hana ajira alafu anasema sijui Ccm mbele kwa mbele. Lazima wajinga wote wapate akili safari hii!!
 
Je walialikwa? Kama ndio, walijibu nini?
He siku ya kuapishwa walihudhuria, walijibu nini officially?
 
Ni swali muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu.

Amani iwe nanyi wadau!

Usiku wa Jana, Wakili Robert Amsterdam ameitaarifu dunia kupitia Twitter yake kuwa amefikia hatua nzuri kupeleka mashtaka katika mahakama ya ICC Uholanzi dhidi ya Magufuli na Serikali yake.

Leo alfajiri, Magufuli akateua mawaziri wawili -- wa Mambo ya Nje, na wa Fedha.

Muda mchache uliopita kwa mara ya kwanza, wawakilishi wa nchi zinazoisadia zaidi Tanzania kifedha na kimisaada yaani Marekani, Uingereza, Sweden, Norway, Japan, Ujerumani, Finland, Korea ya Kusini na Umoja wa Ulaya hawajaudhuria hotuba ya Rais Magufuli Bungeni.

Naomba mnaojua mtuelezee humu, kuna nini kinaendelea jikoni? Au ndo mambo yashakuwa mambo?

Naomba michango yenu!
Kamuulize mumeo Robert Amsterdam
 
Back
Top Bottom