Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Je, ni tatizo gani hili?

Mkuu unahitaji kufanyiwa vipimo vya maabara ili kujua tatizo. Fanya ufike kwenye kituo cha afya kilichokuwa karibu nawe.
 
Wakuu habari, sijaweza kuuweka huu uzi/hoja huko JF doctors,

Naombeni maoni yenu, nina kama saa 46 hivi ninaona damu kwenye choo.

Wala si kuharisha, yani mwishoni mwa choo/haja kubwa, ninaona damu fresh kabisa, yani damu mbichi kabisa.

Ninahofu, naombeni msaada.

Miaka miwili mfululizo nilipimwa hospital tatu tofauti kwa nyakati tofauti tofauti na kukutikana na Hectobacter paylor, na nilikua nikipewa dawa lkini nashindwa kumaliza kutokana na dawaa kama Tinidazole kuninyima apetit ya chakula Na kinywa kuwa kichungu.

Mara ya mwisho nilipima Choo na damu katika hospitali moja na Kuambiwa sina H-pylor.

Naombeni ushauri Nikiwa nachukua hatua za kwenda hospitali kwamba.:-

Nini kinaweza pelekea mtu kuona du kama bleed kwenye choo.

Nini madhara enedelevu.

Naombeni msaada.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kapime choo kikubwa.
Yawezekana Amoeba...Miongoni mwa viashiria ni kinyesi kuchanganyika na damu
 
goodfool, Hilo tatizo nilikuwa nalo mimi mwishoni mwa 2019, kuna janki mmoja tu wa zahanati ya serikali akaniambia kuna bacteria wanaitwa "shigella" ndo husababisha kutokwa fresh blood baada ya haja. Wala hutasikia tumbo kuuma wala nini.

Bwaana aliniandikia dawa fulani hivi nikaenda kuzinunua famasi. Aisee dozi ya wiki moja lakini siku tatu tu dam ilikata nikawa najisaidia fresh kabisa hadi leo sijaona tena. Ila hizo dawa nimezisahau aisee, ningekujuza.

Nilienda dispensary moja hivi wakaanza kuniletea habari ya sijui mara tukipime choo, nikaona wananiyeyusha tu ndo nikamchek huyo jamaa yangu, aliniponya hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kunywa maji mengi pia huenda unapata choo kigumu sana na hivyo kutumia nguvu kukitoa mpk kinakuchana
 
Hiyo ni dalili ya ulcerative colitis, au bawasiri.wahi hospital ujue Nini chanjo ili upate tiba stahili
 
Wakuu habari, sijaweza kuuweka huu uzi/hoja huko JF doctors,

Naombeni maoni yenu, nina kama saa 46 hivi ninaona damu kwenye choo.

Wala si kuharisha, yani mwishoni mwa choo/haja kubwa, ninaona damu fresh kabisa, yani damu mbichi kabisa.

Ninahofu, naombeni msaada.

Miaka miwili mfululizo nilipimwa hospital tatu tofauti kwa nyakati tofauti tofauti na kukutikana na Hectobacter paylor, na nilikua nikipewa dawa lkini nashindwa kumaliza kutokana na dawaa kama Tinidazole kuninyima apetit ya chakula Na kinywa kuwa kichungu.

Mara ya mwisho nilipima Choo na damu katika hospitali moja na Kuambiwa sina H-pylor.

Naombeni ushauri Nikiwa nachukua hatua za kwenda hospitali kwamba.:-

Nini kinaweza pelekea mtu kuona du kama bleed kwenye choo.

Nini madhara enedelevu.

Naombeni msaada.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app

Habari yako Ndugu,
Pole sana na tatizo linalo kusumbua. Kutokana na maelezo yako ni kwamba unasumbuliwa na kutokwa kwa damu kutoka sehemu ya chini ya njia ya chakula kwa kitaalamu Lower Gastrointestinal Bleeding (LGIB)

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha tatizo hili, nitaeleza kwa ufupi :

  1. Magonjwa ya uvimbe(Inflammation): Uvimbe huu unaweza kusababishwa na maambukizi(infection) mfano Amoeba(amoebiasis), Typhoid(salmonellosis), Shigella(Shigellosis) au uvimbe usio wa maambukizi(Inflammatory Bowel Diseases)
  2. Saratani(Neoplasm)
  3. Kupasuka mishipa ya damu(Vascular) mfano Bawasili
  4. Uoto wa vinyama (Diverticulosis)
Kwa maelezo yako umesema hupati homa kwa hiyo tunaweza kutoa maambukizi kama sababu ingawa vipimo vinaweza kuthibitisha vinginevyo. Pia damu fresh inamaanisha damu inatoka karibu sana na njia ya haja kubwa(rectum) yaani haijasafiri kwa muda mrefu. Nakushauri ukamwone daktari bingwa wa magonjwa ya ndani na njia ya chakula(Gastroenterologist) ili afanye uchunguzi wa sababu na eneo linalotoka damu hiyo.

NB. Usitumie experience ya mtu mwingine kutibu ugonjwa wako kabla hujasibitisha kwa daktari shida hasa inayokusumbua. Maelezo haya yasitumike kama tiba kabla ya kumuona daktari bali ni kwa ajili ya kutoa elimu.
 
Mtoa mada,
Kama uko sehemu ambayo unaweza kupata huduma ya daktari tajwa hapo juu huu ndio utaratibu mwafaka kwa tatizo lako.
Nenda kamwone daktari.
Kama huwezi kufika kwa daktari aliyetajwa hapo juu badi fika kwenye hospitali yoyote ili uweze kupata tiba mwafaka.
 
Humu ndani kuna wajinga na wapuuzi kama ilivyo ndani ya jamii zetu na ili jamii ikamilike lazima hao watu wawepo.ni kama vile kwenye msafara wa mamba hua kenge nao hawakosekani ila hapa kenge wamekua wengi kuliko mamba.watu wanatoa hoja nzuri ili kusaidia wasiojua lakini wengine wanapotosha kwa makusudi kutokana na pengine mikwamo yao yakimaisha inawachochea kufanya ivo.mwingine analeta mpaka darubini.sasa huyu ni kenge shoga kabisa.kama huna cha kuchangia si ukae zako kimya tu? Ficha ujinga wako kwa kukaa kimya inatosha acha ujuaji mob.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom