Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Je, ni tatizo gani hili?

Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Je, ni tatizo gani hili?

Tumia sana High fiber diet kama ulivyoelezwa hapo juu pia fika hospital maana hapo naguess yaweza kuwa Hemmorhoids
 
hili ni jambo ambalo sana sana huwatokea wanaojihusisha na ajira ngumu(hard labour).kama upo kwenye hilo kundi basi ni jambo la kawaida sana kutokwa na damu wakati ama baada ya haja kubwa.another possibility yaweza ikawa una hemorrhoids.hivi ni vinyama ambavyo huota kule ila ukiwahi hospital utapata usaidizi.ni vema ukala maboga na matunda na unywe maji mengi na yawe safi.hii itasaidia kuongezea fibre content ndani ya mwili wako ili kuiwezesha digestion kuenda sawa.anyway,pole kwa yalokufika
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
sawa nitafanya kama ulivyonishauri yani huwa navusha hadi siku mbili au tatu bila kupata choo me huwa naenda mpaka yakibana na pia huwa najitahidi kunywa maji mengi
Vipi Shida yako ya kutokwa na damu wakati kujisaidia haja kubwa umepona? Hujaleta mrejesho
 
Habari kwa wote wakuu! Hope mpo njema

TATIZO...

Ni sku chacbe zilizopita ndo niligundua tatizo

Ni ile tu baada ya kumaliza kujisaidia haja kubwa (kunya) zile dakika za mwisho baada y kuangaza macho kwny ile sink nyeupe nilishangaa kuona imetapakaa damu y nyingi sana tena ile damu mbichi

Baada y kujichunguza kwa makini niligundua ile damu inadondoka kwa matone kutoka kwny njia y haja kubwa though sikuwa na maumivu yoyote ndio maana nilishndwa hata kuelewa ile damu ilitoka wap na nadhan bila kuichungulia ile sink hata nisingeweza kujua km nina hilo tatizo

Next time nilikuwa makn kujichungua km ile damu itatoka tena na inaanzia wap...

Soon baada y kuchuchumaa na kuanza kusukuma mzigo niliona matone ya damu yanatoka kwa kasi sana mpaka sink yote ilitapakaa damu, na hata nilipomaliza kushusha mzigo kile kitendo cha kuendelea kuchuchumaa pale kwny sinkvitome vya damu mbichi viliendelea kutoka but hakuna maumivu yoyote Yale

MSAADA...

Kabla cjafikia hatua ya kwenda hospital naamin humu ndan kuna madaktari, wataalamu kibao was afya wenye experience na changamoto tofauti za kiafya

Yoyote ambye ana experience na hili tatizo naomba aje anisaidie kunpa maelezo ya hili tatizo yan
-ugonjwa gan huu?
-chanzo?
-tiba ni nin?

Msaada plz
 
Hali hiyo ishanitokea kitambo,huwa ni kupasuka kwa mishipa midogo ya damu pia minyoo ikishambulia sana utumbo inaweza sababisha kinyesi kuchanganyikana na damu na hali hiyo ilikoma yenyewe hata kabla sijaenda hospital. Haina tofauti na kutokwa damu puani. NB: Nenda hospital
 
Kuna sababu nyingi zinazosababisha kutoka damu na haja kubwa. Ikitokea usidharau lazima Union mtaalamu wa afya.

1. Haemorrhoids

2. Kuchanika kwa ngozi hasa kama unapata choo kigumu.

3. Dalili za cancer ya colon (utumbo mkubwa).
No cyo kama haja kubwa inatoka na damu hapana

Damu inavuja tofauti ndio maana hata kabla mzigo hujaanza kushuka kile kitendo cha kuchuctama 2 na kupush hapo damu ndo inaanza kuvuja na hata nikimaliza haja nikiendelea kukaa pale kwny sink damu pia inaendelea kuvuja mpaka ntaposimama
 
Hali hiyo ishanitokea kitambo,huwa ni kupasuka kwa mishipa midogo ya damu pia minyoo ikishambulia sana utumbo inaweza sababisha kinyesi kuchanganyikana na damu na hali hiyo ilikoma yenyewe hata kabla sijaenda hospital. Haina tofauti na kutokwa damu puani. NB: Nenda hospital
Shukhran kwa ushauri mkuu
 
Hiyo ni LOWER GASTROINTESTINAL BLEEDING ambayo ina a lot of differential diagnoses.

Cha msingi wahi hospitali asubuhi na mapema kabla hali haijawa mbaya.

Unforgetable
 
Habari kwa wote wakuu! Hope mpo njema

TATIZO...

Ni sku chacbe zilizopita ndo niligundua tatizo

Ni ile tu baada ya kumaliza kujisaidia haja kubwa (kunya) zile dakika za mwisho baada y kuangaza macho kwny ile sink nyeupe nilishangaa kuona imetapakaa damu y nyingi sana tena ile damu mbichi

Baada y kujichunguza kwa makini niligundua ile damu inadondoka kwa matone kutoka kwny njia y haja kubwa though sikuwa na maumivu yoyote ndio maana nilishndwa hata kuelewa ile damu ilitoka wap na nadhan bila kuichungulia ile sink hata nisingeweza kujua km nina hilo tatizo

Next time nilikuwa makn kujichungua km ile damu itatoka tena na inaanzia wap...

Soon baada y kuchuchumaa na kuanza kusukuma mzigo niliona matone ya damu yanatoka kwa kasi sana mpaka sink yote ilitapakaa damu, na hata nilipomaliza kushusha mzigo kile kitendo cha kuendelea kuchuchumaa pale kwny sinkvitome vya damu mbichi viliendelea kutoka but hakuna maumivu yoyote Yale

MSAADA...

Kabla cjafikia hatua ya kwenda hospital naamin humu ndan kuna madaktari, wataalamu kibao was afya wenye experience na changamoto tofauti za kiafya

Yoyote ambye ana experience na hili tatizo naomba aje anisaidie kunpa maelezo ya hili tatizo yan
-ugonjwa gan huu?
-chanzo?
-tiba ni nin?

Msaada plz
You cant be serious man
Vipi udai umemwagika Damu MPK IMETAPAKAA SANA kisha Uje JF kuuliza kabla ya kwenda Hospital?
Are you joking?
Kumwagika damu ulikokuelezea kunaweza sababisha very serious complications including DEATH!
Wacha kabisa utani wa namna hii.
Na kama uko serious ktk Uzi huu nenda Hospital haraka sana. Tena ikiwezekana sasa hivi.
 
Mambo ni mengi ila cha msingi fanya ivi vipimo

1: stool occult blood.

2: CEA hichi upima colon cancer.

3: H.pylory

4: ya wezekana bawasari.

Kupona kwako kuna tegemea diagnosis izo.
 
Kuna mshkaji wangu tunafanya naye kazi jana amekuja analalamika kuwa wakati akijisaidia haja kubwa anatokwa na damu. Sasa ameanza kupata wasiwasi kuwa anaweza kuwa na kansa ya njia ya haja kubwa.

Mimi kama mdau wa hapa ninapopaaminia naomba tumshauri huyu mshkaji wangu ili aepukane na janga hili. Yuko kwenye tension kwa kweli

Big Up Jf members kwa ushirikiano wenu

Kuwa makini na kutokwa damu njia ya haja kubwa
By Dk Christopher Peterson
Unaweza kuhisi una uvimbe umejitokeza nje ya njia ya haja kubwa wenye muwasho, maumivu na wakati mwingine ukiwa unajisaidia haja inatoka kwa tabu na kadri unavyotumia nguvu kuisukuma unahisi maumivu, ikitoka inakuwa na damu. Hili ni tatizo la afya ambalo kitabibu linaitwa Hemorrhoids.
Cha kusikitisha, wagonjwa wengi hawapati tiba sahihi kwa ama kuogopa, au kuona aibu kupata ushauri wa daktari kutokana na namna tatizo lenyewe lilivyo. Wachache huishia kununua dawa kutoka kwenye maduka yaliyopo mtaani bila ushauri wowote wa mtaalamu.
Jambo muhimu la kufahamu kwa kila mmoja ni kwamba, kutokwa damu sehemu za siri kunahitaji msaada wa daktari kuliko kutumia dawa bila kujua chanzo cha tatizo. Wanawake wanakuwa hatarini zaidi kupata ugonjwa huu hasa wanapokuwa wajawazito.
Inaelezwa, kadri mimba inavyokua, mfuko wa uzazi hupanuka na kuongezeka ukubwa hivyo kusababisha mkandamizo kwenye utumbo mpana.
Pia, wazee wapo kwenye kundi la hatari kwa sababu mfumo wao wa kinga mwilini dhidi ya magonjwa unapungua.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha kuwa idadi ya wazee wanaopata tatizo hili duniani ni kubwa kuliko vijana na watoto, ingawa bado ni muhimu kuchukua taadhari
Wanaonyanyua vitu vizito ni waathirika pia, kwani kwa kufanya hivyo nguvu nyingi hutumika na kusababisha misuli kukaza hasa ya njia ya haja kubwa hivyo kuidhoofisha na kuvimba.
Wanaofanya zinaa kinyume na maumbile ni kundi jingine.
Mtu anapopatwa na tatizo hili, mara nyingi sehemu ya ndani ya ngozi kwenye njia ya haja kubwa inavimba na kutokeza nje. Huwa linatibika na kuzuilika kirahisi mgonjwa akimuona daktari mapema.
Tatizo hili linatokea wakati mishipa midogomidogo kwenye njia ya haja kubwa inatanuka na kusababisha ngozi ya sehemu ya ndani ya haja kubwa kutokeza nje, kutokana na maambukizi mbalilmbali.
Zipo dalili ambazo kila mmoja anapaswa kuwa makini nazo kukabiliana na ugonjwa huu, ambazo ni kutokwa na damu kusikoambatana na maumivu au maumivu ya kawaida, muwasho au maumivu ndani au nje ya sehemu ya kutolea haja kubwa.
Dalili nyingine ni uvimbe kwenye njia ya haja kubwa na ngozi ya ndani ya sehemu hiyo kutokeza nje. Yeyote mwenye moja ya dalili hizi anapaswa kumuona daktari haraka.
Baadhi ya maradhi kama vile saratani ya utumbo au ya njia ya haja kubwa, zinasababisha kutoka damu sehemu ya haja kubwa hivyo ni kosa kudhani kuwa ni tatizo tu la kawaida na kupuuzia kumuona daktari kwa msaada.
Kuharisha na uzito uliopitiliza, kukohoa kupita kiasi na mwili kukosa maji ya kutosha pia husababisha tatizo hili. Mwili unahitaji maji ili chakula kumeng’enywe vizuri hivyo upungufu wake husababisha ukosefu wa haja kubwa na inapotokea huwa ngumu kiasi cha kuleta msuguano unaosababisha michubuko, ambayo hurahisisha maambukizi kwenye njia ya haja kubwa.
Mgonjwa anayechelewa kupata matibabu hulazimika kufanyiwa upasuaji mdogo kumaliza tatizo alilonalo.
Kunywa maji ya kutosha ni njia rahisi ya kusaidia kuzuia ugumu wa kinyesi utakaoathiri kuchubua njia ya haja kubwa wakati wa kujisaidia. Namna nyingine ya kujiweka salama dhidi ya ugonjwa huu, ni kuhakikisha unapata mlo kamili utakaosaidia kujikinga au kuliondoa kama unalo.
Ulaji wa vyakula vyenye nyuzilishe kwa wingi; mboga za majani, matunda na vyakula visivyokobolewa mfano ugali wa dona kunarahisisha mmeng’enyo wa chakula na kuzuia utaoji wa kinyesi kigumu.
 
Back
Top Bottom