Kutolewa kwa Azam kwenye Mashindano ya Caf ni ujumbe tosha

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Azam complex ni uwanja wa Azam, kama uchawi unacheza mpira Azam walikuwa na muda wa kufanya kafara zote kama Popoma mkuu anavyoamini uchawi unacheza mpira.

Wakati Yanga wametulia kimya Avic town kuna wazururaji wa Msimbazi na Chamanzi walini kwenda kuzurura nje ya Tanzania ndio kuandaa timu.

Sasa pumba na mchele vinaanza kujitenga wazuraji na waliokaa kambini Avic town kuandaa timu nani ameandaa timu?

Simba wanashindwa mechi zao lakini hawana furaha wakiangalia moto wa Yanga na kambi ya Avic town.

Simba imepigwa 3 bila na Raja Casablanca hapo kwa Mkapa hatoki mtu, je hamkuroga?

Majibu ni kuandaa timu kisayansi tu na si vinginevyo.

Nilipenda sana leo Azam wavuke hii hatua lakini uwezo wao umeishia hapo, tujipe pole Watanzania naamini wapenda mpira wote leo tulikuwa upande wa Azam ila uwezo umeamuwa matokeo.
 
Ww nae kama huna hela usipangie wanaume wenzako matumizi..mbona unaumia sana watu kwenda kubadili upepo nchi zingine..nyie hamna hela tuliaaa.....
Taratibu mtani, punguza hasira!

Hivi visenti ambavyo Mwamedi akitoa, lazima aje kuwasimanga mitandaoni ndivyo vya kukufanya uje kututambia? Usitufanyie hivyo bana.

Kwanza sponsor mwenyewe kila siku anasusa. Gubu kama mama wa kambo. Hiyo jeuri ya kuongelea pesa hamna mtani!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
WacheZaji wa Azam Ni misukule hawana Ari ya kupambana kutafuta kitu wanachokitaka,pia timu haina viongozi sahihi Sasa Kama huyo Popat Ana mafanikio gani hapo Azam miaka na miaka anakula hela za Buree....wanatumia gharama nyingi lakini matokeo sifuri.....hawana Malengo zaidi ya miaka 10,Namungo aliingia Cafcc Mara moja akaingia makundi,jiulize Azam Wana kila kitu lakini hawajawahi kuandika historia katika haya Mashindano...utajiri upo wapi au nguvu ya pesa iko wapi?
 
Azam complex ni uwanja wa Azam, kama uchawi unacheza mpira Azam walikuwa na muda wa kufanya kafara zote kama Popoma mkuu anavyoamini uchawi unacheza mpira.

Wakati Yanga wametulia kimya Avic town kuna wazururaji wa Msimbazi na Chamanzi walini kwenda kuzurura nje ya Tanzania ndio kuandaa timu.

Sasa pumba na mchele vinaanza kujitenga wazuraji na waliokaa kambini Avic town kuandaa timu nani ameandaa timu?

Simba wanashindwa mechi zao lakini hawana furaha wakiangalia moto wa Yanga na kambi ya Avic town.

Simba imepigwa 3 bila na Raja Casablanca hapo kwa Mkapa hatoki mtu, je hamkuroga?

Majibu ni kuandaa timu kisayansi tu na si vinginevyo.

Nilipenda sana leo Azam wavuke hii hatua lakini uwezo wao umeishia hapo, tujipe pole Watanzania naamini wapenda mpira wote leo tulikuwa upande wa Azam ila uwezo umeamuwa matokeo.
Punguza maneno. Yanga alikutana na Zalan mechi zote wakacheza hapa hapa Tanzania na walipokutana na Al Hilal habari yao ikaishia hapo hapo.
Kumbuka mchezo ni ule ule, juzi mlikuwa Djibout mnacheza mechi na Asas.
Usijitape sana ukajua kuifungua KMC na Asas basi meshamaliza mchezo.
Kumbuka upo club bingwa.
Kwani Yanga walizuiliwa kwenda kuweka kambi nje ya nchi?
 
Azam awakucheza vibaya ila Gesi ilikata dk ya 60/65 Gauge ilikua haisomi.
Mbaya zaidi ile timu 90% ni wazawa.
Muda unao tumiwa na izi timu kuweka kambi nje ya nchi ni bora timu ijikite apa ndani ya nchi na kujifua ili kupata utimamu wa mwili unaonendana na vigezo vya mashindano husika.
 
Yanga bana, kucheza confederation fainali matambo kama yote. Je, mngejecheza Champion league na African super cup?
Kuifunga KMC na Asas tayari wao wanajiona wanajua ni bora sana kuliko wengine.
Mpunguze maneno, mtakuja aibika mpk mshangae. Kumbuka mpo Champion league, mecheza na Asas (km mlivyojitapa kwa zalan).
Mkitoka hapo sijui mtakutana na nani? Hiyo ni club bingwa.
Unamcheka Azam wakati Yanga Champion league alicheza mechi mbili tu.
Asas hawana uwanja km alivyo Zalan. Kwahiyo muweke maneno ya akiba
 
Kujifua nje au ndani haikupi nafasi ya kushinda. Ni sehemu wao walivyoamua tu.
Ingekuwa kuweka kambi ndani ndiyo kushinda.
Mbona Yanga champion league alicheza mechi mbili tu ya Zalan na Al hilal akatolewa Champion league?
 
Yanga imepata muda wa kutosha wa maandalizi ndiomaana wachezaji wao wako fit kwa dk 90'

Timu zinazo kwenda kuweka kambi nje nyingi huishia kupata wiki 2 tu za maandalizi mwishoe katikakati ya mechi za kimashindano zinakata moto.
 
Yanga bana, kucheza confederation fainali matambo kama yote. Je, mngejecheza Champion league na African super cup?
Kuifunga KMC na Asas tayari wao wanajiona wanajua ni bora sana kuliko wengine.
Mpunguze maneno, mtakuja aibika mpk mshangae. Kumbuka mpo Champion league, mecheza na Asas (km mlivyojitapa kwa zalan).
Mkitoka hapo sijui mtakutana na nani? Hiyo ni club bingwa.
Unamcheka Azam wakati Yanga Champion league alicheza mechi mbili tu.
Asas hawana uwanja km alivyo Zalan. Kwahiyo muweke maneno ya akiba
Usiwashtue waache tutawakumbusha maneno yao wenyewe
 
Back
Top Bottom