KERO Kutolipwa na serikali kwa wakulima wa mahindi Kanda ya Songea

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakulima waliouza mahindi Hifadhi ya Taifa ya Chakula kanda ya Songea hatujalipwa fedha zetu tangu September 2025 Hadi Sasa kimyaa.

Wakulima wameshindwa kurudi shambani wengine mahindi yanaharibika shambani kwa kukosa pembejeo hasa mbolea.

Tunaomba Waziri wa kilimo aingilie kati, hasa sisi wakulima wa Jimbo la Peramiho na Mbinga tunateseka sana. Mahindi sokoni yamefikia Bei zaidi ya Bei ya Serikali na ni cash, lakini Serikali imekaa na Hela ya mkulima kwa miezi zaidi ya minne bila majibu ya kueleweka.
 
Kwanni hawataki kuwalipa sababu zao ni zipi ama wameamua tu!?
 
shida ya hawa wanaokua "anonymous" wakishabandika ndo wamebandika

moderators wangeangalia namna ya hawa jamaa kupata access ya kujibu follow-up questions
 
Hawana hata mpango, hata kuzungumtia tu, hata kutoa ufafanuzi kuwapa matumaini wakulima. Hapo ndiyo mtamkumbuka Bashe na janjajanja zake lakini alitufaa,
 
Kwanni hawataki kuwalipa sababu zao ni zipi ama wameamua tu!?
Sasa utamuuliza nani ndugu? Maafisa wa NFRA watakwambia hawajaletewa pesa, wanasiasa watakujibu kiasiasa, kikubwa ni kwamba toka mwezi wa tisa mwaka jana kuna wakulima hawajalipwa pesa zao. Wengi wamepata hasara mashambani sababu pesa ya pembejeo iko NFRA.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
shida ya hawa wanaokua "anonymous" wakishabandika ndo wamebandika

moderators wangeangalia namna ya hawa jamaa kupata access ya kujibu follow-up questions
Watu wanaogopa, usije kujikuta matatani kwa sababu ya kudai kimilioni kumi chako.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Watu wanaogopa, usije kujikuta matatani kwa sababu ya kudai kimilioni kumi chako.
changamoto sana mkuu, wakulima wengi wanalalamika msimu huu wameshindwa kurudi shamba kwasababu pesa bado haijaingia ,
 
Mkuu, bora hata huyo ambaye hakurudi kabisa. Shida ni kwa yule ambaye alijichanga akaamua kurudi kwa matumaini kwamba pesa itamkuta kwenye hatua labda ya palizi au ya mbolea. Mtu anajikusanya kwa nguvu zote ananunua mbegu, analima, anapanda, anapalialia....hapo kwenye mbolea ndiyo keshaanza kuishiwa anabaki analitazama shamba lake analia kimyakimya. Mimi najiuliza, kwanini walikuwa wananunua kiasi cha mahindi ambacho hawakuwa na pesa ya kulipa? Na kwanini waliamua kukaa kimya wasiwatahadharishe wakulima kwamba pesa ya kulipa haijapatikana wawe makini na maamuzi yao? Kwanini mamlaka ziko kimya kana kwamba hakuna kinachoendelea, kwanini wameamua kuwadharau wakulima kiasi hicho na bado waapata nguvu ya kuonesha wana akiba kubwa ya chakula ilhali wenye mzigo hawajalipwa?!! Hili jambo nina mashaka kama serikali ngazi ya juu wana taarifa nalo, sidhani!
 
hatari sana mkuu, yani unachosema kama nikikumbuka vizuri kilijadiliwa kipindi watu wanaanza maandalizi, wengine wakasema hawaingii shambani wengine wakasema wanaingia fedha zikitoka zitawakuta katikati ya safari wao lazima waanze kuwahi msimu.

huko juu taarifa wanazo mkuu, hata kama sio rasmi, juzi kati hapa kama sikosei ni ITV wale walienda kwenye ghala moja maana kulikua na malalamiko kwamba watu wanadai pesa wanaambiwa hawajulikani, muhusika akapiga blah blah za hapa na pale tu.

watu watazidi kugomea mambo ya shamba na mwisho wa siku tupigwe na njaa

ni uzembe wa mikakati tu kwa walioko ofisini humo
 
Mimi nadhani haya ni matokeo ya kisiasa yasiyo na tija kwa mkulima . Kuendekeza sera za ujamaa kwa mkulima na katika dunia ya kibepari ni kuwatia umaskini wakulima. Sasa hivi kilimo ni biashara, hata mazao ya chakula ni biashara pia. Kufunga masoko ya nje ili kulinda "mlaji" wa ndani ni kumtukana mkulima ambaye anafanya kilimo biashara. Soko la mahindi lipo kubwa sana Kenya, Sudani ya Kusini na DRC lakini masharti mengi na maelewano duni ya kidiplomasia kati yetu na majirani ni kikwazo kikubwa kinachosababisha mkulima asifaidike moja kwa moja na uwepo wa masoko ya mazao katika nchi jirani. Yote sawa, tuffanye mamlaka zipo sahihi, walipeni basi pesa zao kukaa na pesa zao miezi mitano ni kuwadidimiza na kuwaongezea umaskini.

Hata kama serikali ina upungufu wa fedha, kama kweli mamlaka zinathamini kilimo walitakiwa kuona ni njia zipi watu wanaodai watapata pembejeo. Mfano TFC ingeweza kuwapatia mbolea wakulima wanaodai, au risiti ya NFRA kutumika kama dhamana kwa mikopo ya dharura ya haraka benki. Haya yote yangewezekana kama tungekuwa na watu considerate kwenye mamlaka. Kuziba masikio na kufunika kombe mwanaharamu apite siyo sahihi na ni dharau kwa wakulima.
 
hayo unayoyasema wanayaona wakulima tu na wanasema , wahusika wao sidhani kama hata wanaelewa hizo hoja au kama wanauwezo wa kutolea maamuzi, na mbaya zaidi mkulima taarifa hapewi
 
Back
Top Bottom