Kutomuamini Mungu ni ujasiri?

NAISIKITIKIA AFRIKA YANGU

Sijui nani atakuja kutukomboa
Tumejiharibu na kuharibu vizazi vyetu karne hadi karne kwa kuaminishwa stori za kufikirika tena za mataifa ya mbali ambazo zimejazwa hofu,vitisho,chuki na ahadi kwa wafuasi wake
Ni kwa Waafrika pekee ambapo maisha bora yanapatikana baada ya kufa eti dunian sio lolote sio chochote kwao, jambo ambalo limetufanya kuwa kituko kwa dunia nzima

Watu wanakesha kufanya maisha bora duniani mfn china,marekani,korea nk waafrika tuko bize kutafuta maisha bora baada ya kufa the same bullshit we have inherited to our generations for years

Ukweli ambao watu wanagoma kuukubali ni kuwa Mungu mnaelezewa kwenye vitabu vya dini hayupo zaidi ya fictious stories kama zingine tu, mmejazana hofu,chuki ahadi za uongo na kweli , na limited beliefs systems ambazo zinawazuia kufunguka kwenye ukweli

Jiulize maswali yafuatayo kabla hujaanza kulinda dini unayoitetea.

1.Kwanini taarifa za Mungu uletewe na watu kutoka nje ya bara lako,watu ambao sio wa asili yako? Au kwanini unatakiwa kuambiwa habari za Mungu na sio kwamba ulitakiwa mjue naturally? Kwa jinsi ambavyo Mungu anaelezewa kwenye vitabu vya dini na ukuu wake wote ,nikweli anahitaji mawakala ili mjue?

2.Kwanini Mungu amuumbe shetani ambae badae wanaanza kugombea waumini tena muda mwingine wanashirikiana kabisa ,?
Kwa kifupi shetani ni mtaji wa Mungu wa kwenye vitabu vya dini

3.Kwanini Hutakiwi kutumia akili ya kibinadamu ili kumuelewa ilihali amekuumba na akili hiyo hiyo ili iwe utambuzi kwako? Ogopa sana elimu unayopewa afu unaambiwa hupaswi kuhoji

4.Kwanini waafrika sehemu zao tukufu (holy places) zipo nje ya Afrika mfano macca,roma italy Israel nk unlike china,india,korea nk

5.Kwanini maisha bora yapo baada ya kufa lakini tunayaanda duniani,kwan haya tuyaoshi saizi tuliyaanda wapi?

6.Kwanini elimu pekee tunayoipata kikamilifu kwa lugha zetu ni elimu za dini, hakuna vitabu vya sciences, engineering, economics, hata politics vilivyopo kwa lugha zetu?
Nadhani mnaelewa lengo la kusoma elimu fulani kwa lugha yako

7.kwanini tunatakiwa kuwachukia wale wasio amini kama sisi,kama tuna adui mmoja kwanini tusiungane kumshinda adui,? Kwanini mtaji wa dini ni wapinzani wao?

8.Kwann vitabu vya dini vina mikangaiko mingi sana ambayo haiingii akilini isipokuwa kwa nguvu ya vitisho?

Mwisho.
Ubaya ni ubaya bila kujali kafanya nani as long as kitu fulani huwezi kujifanyia na haupo tajari kufanyiwa kutokana na madhara yake kwako basi usimfanyie mwingine.
Huitaji kutishiwa moto ili kujua hili
 
Duh! hivi unaelewa unachokiongea kweli?
Sitaki niingie deep zaidi,... ngoja nikuulize.

Nipe tofauti ya kutetemeka kwa ardhi na Kuyumba kwa ardhi.

Maana unaonekana umekariri.

Tuanzie hapo.
 
Kuna Power kubwa iliyoumba ulimwengu na kuvipa uhai vyote vilivyo hai,lakini sio hiyo miungu ya kwenye vitabu vyenu,hiyo ni miungu mliyojitengenezea kwa malengo na matakwa yenu ya upumbafu na ujinga.
Nguvu ipi hiyo?
 
Vipi kuhusu milima kutengeneza stability dunia isiyumbishwe?

Vipi kuhusu nyota kuwa ni mapambo?
1. Milima kutengeneza stability dunia isiyumbishwe, hiyo ni Geological fact pia,.. do you have any doubts?

2. Nyota kuwa mapambo(kuipamba anga ya karibu ya Dunia), ipo wazi... You can prove it with your naked eyes. Na kukuthibitishia hilo kuna baadhi ya nchi wameweka siku maalumu kabisa kwa ajili ya kusherehekea Beauty of the Sky ambayo imepambwa na Nyota! ⤵️

there are a few regions in the world that have a specific date to put off lights to celebrate the beauty of the sky. One example is Dark Sky Week, which is an annual event that takes place in February. During Dark Sky Week, people around the world are encouraged to turn off their lights and enjoy the night sky. Another example is Earth Hour which is organized by the World Wide Fund for Nature (WWF), which is a global movement that takes place every year on the last Saturday of March.


NB:- Nakusihi usichukie kitu au mtu yoyote mpaka ukajipa upofu wa kutofautisha ukweli na uongo toka kwa kitu au mtu unaemchukia.... "Be a free person, take what's good from anyone, don't hate anyone... Am I making myself clear? Is it loud enough for the people in the back to hear? ☠️🔥"
 
Unalazimisha Mungu awepo tu, hyo ni hypothesis tu kwenye mambo ya asili usiyoyaelewa.

Wewe umeyatungia hadithi na unayaforce yawe kweli.

Tunaprove vipi hiyo hypothesis yako ili tuthibitishe pasina shaka!?

Unaweza thibitisha Mungu yupo!?
Hakuna mtu analazimishwa kuamini uwepo wa Mungu, na kama kungekuwepo huo mlazimisho basi huu mjadala usingekuwepo.
Hypothesis ya mambo ya asili nisiyoyaelewa? Hebu nieleweshe unayoyaelewa wewe?
Jinsi gani ninavyoweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo ni kuwa katika ulimwengu ni lazima kupatikane na nguvu(uwezo) mkuu nje na hizi nguvu/uwezo uliyokuwepo wenye kutuwezesha/kiviwezesha ili kusudio fulani litokee kwa nidhamu iliyowekwa na nguvu hiyo kuu.
Kama utakuwa na wakati jaribu kumsikiliza huyu mwanazuoni kupitia link ya hapo chini.

View: https://www.youtube.com/watch?v=Hw7DG7L6GswVilevile unaweza kuona hoja za Ibn Sina kuhusu hoja za uwepo wa Mungu.
Shukran.
 
Uzembe ni kuumba ulimwengu mbovu unaoweza kuruhusu watu kufanya maovu ilihali uwezo wa kuumba ulimwengu ulio bora alikuwa nao.
Tafuta katika kamusi zote za lugha zote hakuna maana ya uzembe hii au hiki unachokiita wewe ni uzembe si uzembe.

Kingine tamko "Ubovu" au "mbovu" haliingii kwenye "Ulimwengu". Kila kitu ambacho kipo katika ulimwengu kimepangiliwa na kinatokea kwa sababu maalumu aidha unazijua au huzijui.

Ulimwengu kwa wenyewe hauruhusu mbaya kutokea, hilo unakosea kila muda. Sahihisha kwanza kauli yako.
 
Bado hujaonyesha uzembe sababu, haya yote anataka yeye yatokee na asingetaka yatokee yasingetokea pia.

Bado hujaonyesha uzembe na hakuna maana ya uzembe ambayo unajaribu wewe kuelezea, hapa ni wewe unaonyesha ya kuwa humjui Mola.

Ulimwengu kuuhusiaha na udhaifu ni udhaifu wa akili yako, mwanadamu kuwa mdhaifu ndio ukamilifu wenyewe sababu amewekewa vitu na mazingira ambayo yanaleta ukamilifu.

Bado hujaonyesha uzembe unao dai.
 
Uzembe wa Mungu ni yeye kuona jambo rahisi kwa binadamu ambaye ni dhaifu kuweza kuishi bila kufanya ubaya, ilihali yeye mwenyewe ambaye ni mkamilifu anafanya ubaya kwa kulete mafuriko yanayoua hadi watoto wasio na hatia

Ubaya wake uko wapi ? Wakati huu ni utaratibu ameuweka ya kwamba ili ufikie hapa lazima upitie hapa.

Mwanadamu ni dhaifu ila amewekewa mazingira ya kufikia ukamilifu ambayo yako wazi, kwamba akikosea akiomba msamaha anasamehewa, akifanya juhudi anapata akifanya wema analipwa wema na amepewa uhuru wa kuchagua, huu ndio ukamilifu wenyewe.

Nakuuliza swali, kwani kufa ni kitu kibaya ? Mpaka useme watoto hawana hatia ? Hao wanao kufa ni muda wao umefika na rizki yao imekatika. Mafuriko ni sababu ya kifo Chao.

Unatumia nini kupima uzuri na ubaya wa kitu ?
 
Kama kuweza kila kitu ni pamoja na kufanya mabaya, vipi bado ataendelea kuhesabika kuwa ni mwenye upendo wote?
Onyesha hayo mabaya na utuambie umetumia nini kupima huo ubaya ?

Allah hafanyi ubaya na amejiharamishia hilo, lolote analo lifanya ni sahihi na halina makosa.
 
Siku yake imefika na mbakaji ana kosa sababu amekuwa sababu ya kifo cha mtoto husika.
 
Kwani ni watoyo wangapi wamezaliwa na wakafa siku hiyo hiyo?

Kwanini asiwasaidie hao kwanza?

Wengine wanafia tumboni hata fursa ya kuiona dunia hawaipati, huyo Mungu anakuwa wapi wakati hayo yanafanyika?
Ndio maana nikasema hivi hao kufa kwao siku hiyo hiyo ndio ilikuwa haki yao na stahiki yao.

Kwahiyo ilipangwa wakizaliwa tu wafe ndio maana wamekufa.

Mungu ndio anakuwa ametaka iwe hivyo ndio maana imekuwa. Kijana mngemjua kwanza huyu Mungu msingekuwa mnauliza maswali ya kitoto namna hii.
 
Kama umeona uwepo wa Mungu ni wewe. Kuna watu wanapitia magumu kwenye maisha hadi wanafikia uamuzi wa kusema hivyo.

Kifupi kila mtu na imani yake. Na matokeo ya hiyo imani yake ni yake. Aheshimiwe kadri ya imani yake.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kama ndivyo, watu wanasali kwa Mamposya wote wangekuwa na magari. Mbona wengine ni maskinoi wa kutupwa huku akina mwamposya wenyewe wakiwa matajiri wa kutisha.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Pagani asikutese. Hata hivyo mafundisho ya dini yanasema TUPENDANE. Hayajasema tuwapende wa imani zetu tu, kwa hiyo ni tuvumiliane.
Cha ajabu wapendwa wanajitambulisha kwa salamu. Utadhani wameiona mbingu.

Wanajiona wako tofauti sana na sisi tusiookoka.

Kwa bahati mbaya huwa wanakuja kukopa kwa sisi wapagani.

Dunia nenda nayo hivyohivyo. Mheshimu kila mmoja kama alivyo. Hutasumbuka wala kugombana na watu. Ukijionesha upande wako usidharau upande wa pili, mtagombana.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Reactions: Tsh

Mfano sio halisi sababu una muongelea Muumba kwa kumlinganisha na kiumbe.

Sahihisha kwanza hapo.

Kwa minajili hiyo ulicho kiandika chote bado hakina uhalisia na ni makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…