Kutomuamini Mungu ni ujasiri?

Unaelewa mantiki ya uhuru haiambatani na adhabu?
Amekwambia nani ? Unapo muadhibu mwanao baada ya kukosea (hapa napo Kuna uhuru) huwa anakuwa hayuko huru ? Huwezi kuutenganisha uhuru na kupatia au kukosea.

Kijana hata hili dogo linakushinda kuling'amua ?
 
Unampa mtoto uhuru wa kuchagua kula Biriani au Pizza, huo ndio uhuru.
Ndio maana hata wewe Leo hii unamkana aliye kuumba na anakupa pumzi, huu ndio uhuru kamili sasa.
 
Nilikuuliza ututajie sifa za kitu kilicho jificha ni zipi ? Hukujibu hili swali.
Okay

Kilichojificha huwa kina sifa ya kuogopa

Kina sifa ya kutojiamini
 
Kumuambia mwanamke unaye mtongoza achague kati ya kukupenda wewe au kutokupenda halafu ukasema akichagua kutokupenda wewe utamuua. Huo sio uhuru wa kuchagua

Hiyo ni amri.
Sasa huu mfano wako si kamili na huwezi kuuweka au kuulinganisha na uhuru alio tupa Allah.

Allah alipo tuumba akatupa uhuru wa kuchagua, bali akatupa na natija ya kila chaguzi kwa maana, ukichagua hili hatima yake ni hii na ukichagua lile hatima ni Ile. Ili ukija kuhukumiwa ukosee cha kujitetea, sababu usingebainishiwa napo ungelalamika.

Allah anaumba na ni Mjuzi, ndio maana wewe akili yako imeishia katika mfano huu.

Hujui amri kijana, amri haifungamani na natija, jifunze lugha walau kidogo. Amri ni hii "Simama haraka" au "Njoo". Hii ndio amri.
 
Okay

Kilichojificha huwa kina sifa ya kuogopa

Kina sifa ya kutojiamini
Sasa kwanini umesema Mola amejificha na Hana sifa hizo ulizo zitaja hapa ?

Ndio maana huwa napenda muwe mnajibi maswali, sababu ujinga wenu huzidi kuonekana.
 
Na ukichagua mema unaenda peponi, kwahiyo ni hiari yako wewe tena ukawekewa wazi kabisa. Ili usije kusema hukuambiwa.

Hakuna amri ya namna hiyo, huo ni uhuru kamili. Ili ukosee cha kujitetea.

Sasa unafiki nao ni kitu kibaya, na Allah hataki mtu mnafikiria, Sasa ukifanya unafiki ni wewe.

Lakini, vile vile akaweka msamaha ukikosea unasamehewa, maana ukiingia peponi ujue umetaka wewe, kwa uhuru ambao ametupa.
 
Wakati anafanya hivyo, lengo lake si lilikuwa kuufanya ulimwengu uwe bora?
Na ndio maana imekuwa bora na akaufanya ni kituo Cha kuelezea katika hatima kuu.
Sasa kama aliweza kuona yatayojiri kabla hayajatokea maana yake aliona imperfections zote.
Huo ni ukamilifu wake na akaamua iwe hivyo, huo si kutokukamilika.
Na alikuwa na uwezo wa kubadili au kuboresha kuondoa hizo imperfections lakini akaziacha.

Maana yake huu ulimwengu wenye njaa, masunami, vimbunga, matetemeko, magonjwa, yanayoua mamilioni ya watu ikiwemo watoto wadogo wasiojua baya na zuri.
Unarudia nukta Ile Ile, ambayo nimeshaijobu.

Hilo hataki Wala Hana shida yoyote ndio maana amekupa uhuru wewe.

Na ahitaji sifa zako Wala umsifie.
 
So Mungu huyu ana inferiority haamini kwenye kupendwa bila kutengeneza drama, haamini kuwa anaweza kusifiwa bila kutengeneza tatizo ili umrejee kumlilia.

Ni Mungu wakijinga anayependa sifa za kishamba.
Bado hujaonyesha ujinga wake, bali umeonyesha ya kuwa ni kwa namna gani humjui.

Nasubiri hoja.
 
Tafuta katika kamusi zote za lugha zote hakuna maana ya uzembe hii au hiki unachokiita wewe ni uzembe si uzembe.
Mantiki yako ya kunikosoa maana ya uzembe ina lengo la kuthibitisha au kubadili nini kwenye hoja yangu?

Kwamba uzembe ni neno lenye maana ambayo ni positive na hivyo nimepotosha kulitumia kumuelezea negative Mungu?

Au ni sahihi kuwa neno hilo la uzembe haliwakilishi positive thing na hata ukikosoa kwa kuweka maana sahihi, halitaweza kuonesha ubora wa kitu?
 
Kama kila kitu kimepangiliwa na kinatokea kwasababu, maana yake hatuna uchaguzi. Tunafanya kile tulichoamuliwa tufanye.

Kama kila kitu kimepangiliwa na hutokea kwa sababu maalumu, kwanini kuwe na adhabu siku ya mwisho?

Kama kila kitu kimepangilia ni ipi nafasi ya kumlaumu binadamu kwa kufanya ndivyo sivyo?
 
Mungu alimuumba Adam kwa udongo.

Udongo alioutoa ardhini hapa duniani.

Sisi wote ni zao la Adam.

That means sisi asili yetu ni ulimwengu kupitia udongo.

Sasa ikiwa kama kweli akili yangu ina udhaifu, huoni nafasi ya ulimwengu kuwa na udhaifu pia kwasababu uli-generate udongo ambao ulitumika kuumba viumbe ambavyo vikizaliana miongoni mwao kuna viumbe vitakuwa na akili dhaifu?
 
Ubaya wake uko wapi ? Wakati huu ni utaratibu ameuweka ya kwamba ili ufikie hapa lazima upitie hapa.
Huko juu umesema kila kitu kimepangiliwa na kinafanyika kwasababu maalumu.

Kama kila kitu kimepangiliwa na kinafanyika kwasababu maalumu, huoni njia yeyeto atayopita binadamu ni sehemu ya mipangilio aliyowekewa na Mungu?
 
Mwanadamu ni dhaifu ila amewekewa mazingira ya kufikia ukamilifu ambayo yako wazi, kwamba akikosea akiomba msamaha anasamehewa, akifanya juhudi anapata akifanya wema analipwa wema na amepewa uhuru wa kuchagua, huu ndio ukamilifu wenyewe.
Katika thinking ya kiutu hilo jambo linaweza ku sound very reasonable.

Lakini katika perspective ya Mungu hilo jambo ni ridiculous.

Mungu mjuzi wa yote hawezi kufanya betting.

Alishajua kila kitu mapema hata kabla hajakuumba kuwa akikuumba na udhaifu bado hautaweza kufanya kile apendacho.

Alishajua mapema kuwa udhaifu huo anaotarajia kumuumbia mtu, utamfanya huyo kiumbe awe mkaidi hata pale atapoweka msamaha ili mtu huyo ajisalimishe kwake.

Kwa mantiki hiyo Mungu alikuwa na choice ya kuachana na mfumo huo kwasababu alikwisha ona out come yake yote.

Lakini aliamua kupitisha wazo hilo.

Maana yake alijiandaa na matokeo yake.

Maana yake Mungu ndio alipenda kuona watu wanaishi kwa mfumo huo.

Maana yake binadamu hawezi kulaumiwa kwa namna alivyokuwa kwasababu ni asili iliyopo ndani yake na hakuweza kuepuka.
 
ni kibri wakati ukiwa na afya!!!
 
Zingatia haya
 
Nakuuliza swali, kwani kufa ni kitu kibaya ? Mpaka useme watoto hawana hatia ? Hao wanao kufa ni muda wao umefika na rizki yao imekatika. Mafuriko ni sababu ya kifo Chao.

Unatumia nini kupima uzuri na ubaya wa kitu ?
Natumia empathy kupima ubaya au uzuri wa kitu

Kufa ndio nikitu kibaya na ndio maana ukiugua unaenda hospitalini kutibiwa ili usife.

Hauwezi kufurahia mwanao augue ili afe akamuone Allah.

Kufa ni kubaya na ndio maana hata modern Mosque ina fire extinguisher, emergency alarm nk.

Wanafanya hayo yote kwasababu watu hawapendi kufa, hivyo kifo kitokee tu kwasababu ni nje ya uwezo wao, watu wameshindwa kukidhibiti ila caution zote zilichukuliwa.

Kifo ni kibaya ndio maana unafanya kila kitu kuhakikisha unazuia mianya yote inayoweza kukuweka kwenye hatari ya kuweza kufa.

Kifo ni kibaya na ndio maana hauwezi kucheka au kufurahishwa na taarifa ya kifo cha mtu uliyekuwa unampenda sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…