Haiwezekani watu wanazurura duniani kuichafua Nchi yetu. Wamesoma kwa kodi za Watanzania
Wanaheshimika huko nje kwa siha njema ya Nchi yetu. Wakifika kule wanaanza kuitukana Nchi yetu
Hii Nchi yetu ipo kwa sababu kuna watu walijitolea maisha yao yote kuijenga hii Nchi
Kuna watu walimwaga damu.
Kuna watu walienda Uganda kuipigania Nchi wakarudi wamekatika miguu, wengine walirudi hawana mikono, wengine walirudi ni maiti.
Nchi hii ilikombolewa toka tukiwa tumboni mwa mama zetu
Anatokea mtu mmoja mropokaji, msaliti pengine hana hata dna na Tanzania yetu anaenda kwa Mabeberu kutukana Nchi yetu
Wanamtukana Rais wetu mpendwa Magufuli, Wanatukana Maendeleo anayotuletea
Wengine ni Wabunge wanaenda amerika kukutana na Mabeberu ati kuisema vibaya nchi yetu
Serkali watu kama hawa Kwanini mnawaacha huru? Kwanini wasihukumiwe kwa kusaliti wazee wetu waliopigania hii Nchi
Dawa ya usaliti hata huko kwa mabeberu inajulikana
Hao marikani haijawahi kucheka na msaliti wa Nchi adhabu yake inajulikana
China haijawahi kucheka na msaliti nenda popote msaliti wa Nchi zawadi yake inajulikana
Serkali acheni kuwachekea Wasaliti wa Nchi watatuharibia taifa letu
Kama kina kambona wenye heshima zao waliondolewa Uraia kwa manufaa ya Nchi Yetu mnaogopa nini kuwapokonya hawa wasio kuwa hata na historia ya ukombozi wa Nchi yetu!
Tumechoka kila siku Nchi yetu kutukanwa na wanasiasa wasaliti
Hatutaki tuwe kama Congo drc aliwachekea Wapinzani mwisho wake Wapinzani wakaiharibu Congo sasa ni machafuko kila siku huko Congo
Ni bora watu wawili au watatu waumie ili Watanzania milion 50 wawe salama
Tanzania tuna chama cha kizalendo kimoja tu ambacho ni Ccm na Tanu Hivi vyama vingine vimeletwa na Mabeberu kuja kuharibu Amani ya Nchi yetu
Naomba serkali ifutie uraia na kufunga wasaliti wa Nchi yote
Uingereza juzi imefutia uraia watu wengi kutokana na kusaliti Nchi yao
Serkali Kwanini inawaogopa hawa?