MKUU
Shayu!
Kila kiongozi katika CCM anaumwa saratani ya MISAADA. Nilishindwa kuamini masikio yangu siku ile Waziri wa Ujenzi Magufuli alivyo kuwa akimwambia Mkulu kwamba "ONGEZA SAFARI ZA NJE BABA KWANI NDIYO ZINAJENGA BARABARA".
Sasa ukiwa na viongozi kama hawa, ambao eti ndiyo viongozi wasomi ndani ya CCM halafu wamekosa mbinu za kugeuza fursa tulizonazo ili zilete maendeleo, inageuka kuwa JANGA.
Ni ukweli usio pingika kwamba, tumefikishwa hapa tulipo na uongozi wa CCM. wametanguliza UBINAFSI, UFISADI, KUTAFUTA MADARAKA KWA KUJIPENDEKEZA, UNAFIKI na mambo yote yanayo fanana na hayo.
Hivi inapofika kiwango cha hata waalimu kukosa chaki za kuandikia ubaoni, serikali hii itamudu kufanya kitu gani katika nchi hii? kila kiongozi amejaa uongo na ahadi zisizo tekelezwa.
Juzi sakata la Gesi, wazuri Mkuu na mawaziri wengine wanaelezea ahadi na mipango ya manufaa ya Gesi kwa wana Kusini. Muda kidogo anatoa taarifa kwamba wana Kusini wasitegemee kunufaika na Gesi katika muda mfupi ujao, hadi kati ya miaka 10 mpaka 20!!! Huyu ni kiongozi wa namna gani katika Tanganyika hii????
Na kwa vile wanajijuwa kwamba wameshindwa kazi tuliyo wapa kinacho fuata ni ubabe ndio unaotawala kwa sasa.
Hakuna njia nyingine ya kurekebisha haya zaidi ya kuiondoa CCM madarakani 2015. Kwani yeyote atakaye enda kinyume na sera zao za UFISADI huyo anakuwa ndiye adui yao mkubwa.