Asante kwa somo lako
Umeliongelea vizuri ila tatizo linakuja ni pale mzalendo kwetu anajulikana tofauti kabisa na ulivyoliezea kwani hakuna mafundisho hayo katika serikali nyingi duniani especially Africa
Wazungu wanaojitahidi sana na kujali wazawa kama wazalendo pia wapo wengi na hao ndio wanaopaswa kufuatwa.
UK kwa mfano, wamefundisha hili kwa sababu mfumo wao haubagui likija suala la uzalendo yaani ukizaliwa tu una haki zote bila kubaguliwa aidha unatoka Afghan au unatoka Lesotho origin.
Maadam umezaliwa hapo wewe ni mzawa na uzalendo unategemea na upendo wako wa nchi uliozaliwa
Kidogo wakenya wamefuata kanuni na sheria za Uingereza ambapo mpaka mawaziri wasomali wamejaa na kila sekta wapo na haijalishi rangi wala dini wala asili. Na huo ndio uzalendo kwani wanalitumikia taifa walilozaliwa na hawapajua mahali pengine zaidi ya hapo walipozaliwa.
Sasa sisi hilo darasa lilitupita na ndio maana akitokea mmoja aliesoma na kuingia siasa au kazi kubwa ataitwa majina ya kila aina.
Kwanini? Kwa sababu hatujafundishwa kuwa nao ni wazawa kama wewe.
Angalia USA wanajeshi weusi wamejaa na wanapigania nchi yao na haijalishi asili yake ni Guyana au Jamaica
UK mayor wa London ana asili ya Pakistan na Waziri wa mambo ya ndani ni mpakistan na ni wazawa na wazalendo haswa.
Mkubwa wa kitengo cha Scotland yard ana asili ya India sasa angalia kazi zote hizo nyeti zimeshikiliwa na hao bila kujali wana asili ya wapi.
Mkuu wa police Haringey ni mweusi pia na wengi tu
Sasa kwanza ni lazima tuwakubali watu wa aina zote kulijenga taifa bila kuwabagua la sivyo tutabaki na chuki na watu wengine wenye asili tofauti
Wengine huwa wanasema ooh hatutaki tuingiliwe maana watatuibia siri zetu what joke
Vipi hao kina Saddiq Khan?
Uzalendo hauna sura bali upendo wa nchi yako