Shayu,
Ni kweli CCM imehangia kwa wananchi wengi kutokuwa na uzalendo. CCM ilipopoteza mwelekeo na kutekwa na matajiri, mafisadi, wauza mihadarati, na kukumbatia rushwa na mishe town kama sehemu ya maisha ya Watanzania kila mtui alikata tamaa maana uzalendo ukawa haulipi. Hili hata CCM ikifanya vipi haiwezi kulikataa.
Pia ni kweli baada ya CCM kuwa na mwelekeo huo, maendeleo yalirudi nyuma saana maana rushwa, ufisadi, mihadarati na yote mabaya yalifanya bajeti yote inayotokana na pesa za ndani na nje kuliwa na miradi ypte kutotekelezwa hali iliyprudisha TZ nyuma. Pia TRA iliacha kukusanya kodi au ilikusanya kidgo huku walipaji wakubwa wakiwa hawalipi, matokeo yake tukapata mamilionea na tukashindwa kugharimia miradi ya maendeleo. Sijui kama kuna anayekumbuka "vitafunio na chai au takrima" kuwekwa kwenye bajeti.
Lakini pamoja na hayo yote awamu hii imerekebesha mambo. Bajeti yetu inafanya shughuli ilizopangiwa. Kodi inakusanywa, na miradi mingi inaonekana na kukamilika. Ambao wazembea hawaachiwi. Serkali inawawajibisha. Hii ime"restore" heshima. Najuwa uzalendo uliokuwa umeondoka hauwezi kurudi kwa siku moja. Itachukuwa muda serkali kuwafanya wananchi kubadilika na kuwa wazalendo kama zamani.
Pamoja kukubali kwangu kuwa CCM na srkali yake wamechangia kuondoa uzalendo, lakini upinzani nao wanechangia kuondo uzalendo. Kwanza viongozi wa upinzani ndiyo vinara wa wa wadio na uzalendo. Hebu chukulia mtu kama Zitto. Kwenye jimbo lake kuna wanafunzi hawana madeski. Ukiangalia Magufuli kaeleka miradi mikubwa kwenye jimbo lake, lakini anadiriki kuandika barua ya kuwanyima watoto wa TZ pesa zitakazoleta mabadiliko katika elimu yao.
Zitto anasemea watoto wanaopata mimba, mimi ninavyojuwa hiypo iko kwenye rasmi na sheria za TZ. Magufuli hakuanzisha. Hii ilkuwapo wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Mkwere. Sasa hii anaipigia na kujaribu kuzuia mabilioni ya maendeleo. Hivi hapa uzalendo wake upo wapi. Je hiyo pesa isingetumika Kigoma. Kama hili la mimba kwake ni muhimu kwa nini asianzishe shule zake ambazo atawaweka hao.
Kama hili la mimba anataka libadilike kwa nini asitumie njia ya bunge kulibadilisha kama inavyotaka demokrasia. Najuwa atasema bunge la CCM halitaipitisha hiyo sheria, ambayo ni kweli, lakini hivyo ndivyo ilivyo demokrasia. Kwani ninyi mnafikiru Raisi wa USA hakufanya makosa? Makosa kafanya, lakini masenata walio wengi wamesema hana kosa. Na sheria inasema wakimuachia basi. Na ameachiwa kwa sababu republicans ndiyo wengi, na hawawezi kumuondoa uraisi mwenzao.
Wakati mwingine tunafikiri maamuzi ya mabunge ni rational, ukweli ni kuwa chama hutangulizwa labda kuwe na jambo ambalo ni la "national interest/security" hapo huwa wote wanakuwa pamoja. Jambo kama ule mkopo wa elimu ni la "national interst/security" hakuna ambaye angetemea kuna mtu ataenda kuchongea eti tunyimwe. Kwanza, mikopo ya masharti kama hayo hatakiwi. Mkopo mashati yake yawe namna ya kurudisha, kwa miaka mingapi, na kwa interest gani na siyo usipokubali ushoga hatukupatii.