Nimeona niandike kipande kidogo kinachohusu uzalendo.
Mara nyingi unaweza kutana na mtu akisema uwe mzalendo, wengine hata wakidiriki kutumia neno hili kinyume kabisa.
Ipo hivi, uzalendo kwa kingereza ni "patriotism" mzalendo ni patriotic, uzalendo maana ya kiulimwengu (universal meaning) ni mapenzi ya mtu kwa taifa lake ,pamoja na jamii inayomzunguka yaani
*Patriotism is the feeling and expression of love for one’s home country, along with a feeling of unity with those who share those feelings*
Mapenzi kwa nchi au Taifa lako hutofautiani nchi na nchi ,Lawrence W.Reed katika andiko lake la *True meaning of patriotism* ,anasema mapenzi kwa nchi yako sio kupenda milima,mito,maziwa,misitu,hali ya hewa sababu hata nchi zingine zina milima na mabahari,mito na misitu.
Anasema Mapenzi ya nchi yako sio kutetea serikali sababu hata nchi zingine zina serikali ,na pia serikali huingia na kutoka, ni sawa leo uzalendo wako ni kusifu na kuamini katika serikali ya Bush ,siku Bush akitoka madarakani? Je na uzalendo wako utakuwa mwisho?
Uzalendo ni mapenzi kwa nchi au Taifa lako,huwezi kutokea kupenda kitu bila sifa (Sababu),merits zinazokufanya uwe (attached to ).
Ni sawa mapenzi katika familia yako (Marital fedelity),una mpenda mke wako sababu ya tabia zake,na historia yenu mlipotokea hivyo utaendelea kupambana muwe pamoja bila kuvurugwa na yeyote.
Mapenzi ya nchi yako ni tofauti na mapenzi ya mtu mwingine katika taifa lake sababu ya tofauti ya historia ya taifa hilo na watu wake, tamaduni,mila ,misingi na desturi mliyopokea kutoka kwa waasisi wa taifa lenu (national fathers).
Hivyo basi uzalendo ni kupenda nchi yako ,sio kwa sababu ya milima na bahari ,ni kwa sababu ya misingi hiyo,historia ya watu wa taifa hilo na nchi yenyewe na tamaduni yake na watu wake.Sio kuishia hapo tuu, kazi nyingi ni kulinda misingi hiyo ,storia hiyo ,watu hao na maslahi yao dhidi ya mtu yeyote anaye hatarisha kuivuruga awe wa nje au wa ndani.
Lawrence Reed anasema ,marekani ukitaja tuu misingi iliyopo katika azimio la Uhuru wa marekani (American declaration of Independence) ndio kitovu cha uzalendo wa watu wa marekani.Mule kuna storia ya taifa lao,watu wao,na misingi ya waasisi wao (Civic virtues)ambayo mingi imeingizwa katika katiba ambayo hulindwa kwa namna yeyote.
Tanzania sisi tuna misingi (Values na civic virtues) na tamaduni iliyoaminiwa na tuliyoachiwa na waasisi wetu (Nyerere na viongozi wengine).
Kama amani,umoja,usawa na haki, upendo na msingi mingine aliyotuachia ipo katika katiba ya TANU au Azimio la Arusha , Binadamu wote ni sawa,uhuru wa mawazo, kufanya kazi kwa bidii,heshima kwa kila mtu,usawa, Demokrasia , misingi mingine aliyoiamini waliyo iamini iliingia katika katiba , misingi hii ndiyo imekuwa ikitumiwa na watangulizi na viongozi wengine hadi hivi sasa katika kudumisha taifa letu na maendeleo yetu.
Hivyo uzalendo ni kupenda nchi kwa kuhakikisha misingi hii inadumishwa ,watu wake wanaishi vyema pia hata kujitolea kwa niaba ya watu ili waishi vyema kuwasaidia au kuwasemea na kuwasimamia.Mzalendo ni anayehakikisha misingi yote tuliyoachiwa ina dumishwa na kuheshimiwa ,stori ya uhuru wetu na huru tulio achiwa unaimarika bila kutikiswa na watu wa aina yeyote wa nje au wa ndani .
Ndio maana kuna uzalendo wa kikatiba unaitwa *Constitutional patriotism* uzalendo wa kuheshimu na kuilinda katiba, *Jurgen Habermas* ameelezea vyema sana dhana hii,hivyo yeyote atakaye heshimu na kuilinda katiba na sheria zingine huyo pia ni mzalendo.
Watu watakaotimiza misingi hii kwa kikamilifu hao watakuwa wazalendo wa taifa lao haswa na watakao timiza majukumu yao ya kutetea na kusifia serikali na mamlaka hao watakuwa wafuasi haswa.
Shukrani sana.
Abdul Nondo
abdulnondo10@gmail.com