Sema ukweli; taasisi nyingi ni Hospitali na Zahanati za serikali kwa wanafunzi wa vyuo vya afya vya Private ndiyo wahanga wakubwa wa kutozwa hela wakienda field.Ni tatizo kubwa tena na sugu hasa kwa miaka hii linazidi kukithiri. Ati, mwanafunzi anaomba afanye field (yaani anafanya kazi na kujifunza pia), ila wao wanamtoza pesa. Tena taasisi za serikali ndo zinaongoza, kiukweli ni tatizo na ushahidi upo. Ilhali hawa watu ni watanzania, wao au wazazi wao wanalipa kodi kuendesha taasisi hizo, ila taasisi zimejifanya ni chuo ama ni kamradi kao ati wanafunzi wataharibu vitu. How? Kwani wafanyakazi hawaharibu? Kwanini uconclude ataharibu kabla ya kuconclude atatengeneza?
Ni kweli kabisa aisee! Na imepewa baraka zote. Yani as long as mwanafunzi ametoka chuo cha private basi ni lazima alipie. This is very confusing.Sema ukweli; taasisi nyingi ni Hospitali na Zahanati za serikali kwa wanafunzi wa vyuo vya afya vya Private ndiyo wahanga wakubwa wa kutozwa hela wakienda field.
Ni utapeli, rushwa. Kama ushahidi upo, wahusika wachukuliwe hatua.Kumekuwa na utaratibu wa kutozwa fedha kwa wanafunzi wanaoenda kwenye taasisi mbalimbali za serikali kujifunza kwa vitendo. Hii ni sehemu ya kujifunza na pia kusaidia majukumu ya taasisi husika kwa kipindi fulani.
Badala yake, wanafunzi ndio wanaoombwa pesa nyingi ili kupata nafasi hiyo. Utaratibu wa kulipa ni kwa siku, wiki, na hata kwa mwezi. Mfano: mwanafunzi anaombwa kulipa elfu tano kwa siku kwa muda wa miezi mitatu na zaidi.
Je, serikali imezingatia hali za wanafunzi kama:
Sasa tujiulize sote: je, suala hili ni sahihi kwa kundi hili linalohitaji jicho la upekee sana ili kutimiza ndoto na malengo ya kuijenga kesho bora? Ikiwa kijana anasoma kwa mateso na gharama nyingi, na baada ya hapo anarudi kuungana na jamii inayohitaji ajiajiri, mtaji unatoka wapi ikiwa alimaliza fedha kutafuta nafasi ya kujifunza kwa vitendo?
- Kipato cha mwanafunzi, ikiwa hana chanzo kingine zaidi ya wazazi maskini.
- Jukumu la ulipaji ada chuoni, ambapo hulipa ada sawa akiwa darasani.
- Gharama za nauli na chakula.
- Majukumu anayopatiwa.
Ushahidi upo wa kutosha tu, sasa utashitaki vipi na wanakupa account kabisa za mamlaka husika? Humpi mtu mkononi. Mfano; wanakuambia ni mapato ya hospitali kufidia vifaa. Watoto wa masikini wanateseka ilhali ni walipa kodi.Ni utapeli, rushwa. Kama ushahidi upo, wahusika wachukuliwe hatua.
Mkuu mimi nilienda kufanya kazi Fulani kwenye Zahanati ya serikali, pale kulikuwa na WIFI ila walikataa kuniunganisha wakati nafanya Kazi hapo Kwa siku kadhaa. Hiyo ni haki kweli wakati ni Kodi zetu zinatumikaMkuu, ni ofisi gani ya serikali wamefanya ivyo?
Zipo kaka na ushahidi ninao. Wanafunzi wa vyuo vya afya wanateseka sana hasa private. Field unalipia? Nilikutana na madogo wanatia huruma hadi wanataka kulia yani. Na kamekua katabia sugu kwa waganga wakuu.Mkuu, ni ofisi gani ya serikali wamefanya ivyo?
Bora wifi huwezi jua imepatikanaje. Ila madogo wanalipishwa pesa ya fild asee, ni kituko😀 na waganga wakuu wamebariki! Means serikali imebariki?Mkuu mimi nilienda kufanya kazi Fulani kwenye Zahanati ya serikali, pale kulikuwa na WIFI ila walikataa kuniunganisha wakati nafanya Kazi hapo Kwa siku kadhaa. Hiyo ni haki kweli wakati ni Kodi zetu zinatumika
Fee zote za serikali zipo structured. Ni predetermined. Kama wahusika wameibuka na kutoza tozo ambazo hazijaidhinishwa popote mfano Bodi ya Hospitali au Waziri mwenye dhamana, hiyo tozo ni batili.Ushahidi upo wa kutosha tu, sasa utashitaki vipi na wanakupa account kabisa za mamlaka husika? Humpi mtu mkononi. Mfano; wanakuambia ni mapato ya hospitali kufidia vifaa. Watoto wa masikini wanateseka ilhali ni walipa kodi.
Asante Daktari kwa ufafanuzi.Pale hospitali wanafunzi hawa watapata huduma mbalimbali, mf. Kuna vifaa watatumia wakati wa mafunzo lakini pia kufundishwa na watumishi waliowakuta.
Hospitali husika huwa inatoa motisha mbali mbali kwa watumishi wake, hivyo lazima ikusanye mapato ili kufanikisha majukumu yake. Moja ya vyanzo vya mapato ni huduma kama hizi za field katika taasisi.
Kwa jicho hilohilo uliloona kama ni nongwa field practice kulipiwa, hoji umuhimu wa kulipa ada kwa vyuo vya serikali maana wanasoma watoto wa wananchi maskini (issue ya kiasi ni jambo jingine)
Hujajibu swali uliloulizwaMkuu mimi nilienda kufanya kazi Fulani kwenye Zahanati ya serikali, pale kulikuwa na WIFI ila walikataa kuniunganisha wakati nafanya Kazi hapo Kwa siku kadhaa. Hiyo ni haki kweli wakati ni Kodi zetu zinatumika
Naamini huu ujinga mtakuwa mmeanza kufanya baada ya Magufuli kufarikiPale hospitali wanafunzi hawa watapata huduma mbalimbali, mf. Kuna vifaa watatumia wakati wa mafunzo lakini pia kufundishwa na watumishi waliowakuta.
Hospitali husika huwa inatoa motisha mbali mbali kwa watumishi wake, hivyo lazima ikusanye mapato ili kufanikisha majukumu yake. Moja ya vyanzo vya mapato ni huduma kama hizi za field katika taasisi.
Kwa jicho hilohilo uliloona kama ni nongwa field practice kulipiwa, hoji umuhimu wa kulipa ada kwa vyuo vya serikali maana wanasoma watoto wa wananchi maskini (issue ya kiasi ni jambo jingine)
New members mnasapotiana bila kutueleza sisi expert members ni wapo mlitozwa pesa ili kufanya field,Mimi kama mwalimu,walimu wa field wakija shuleni kwetu Huwa tuna wasapoti kwa kuwapa makazi,chakula na fedha kidogo za kujikimu,sasa huko watozwako pesa ili kufanya field ni wapi?KamaNi tatizo kubwa tena na sugu hasa kwa miaka hii linazidi kukithiri. Ati, mwanafunzi anaomba afanye field (yaani anafanya kazi na kujifunza pia), ila wao wanamtoza pesa. Tena taasisi za serikali ndo zinaongoza, kiukweli ni tatizo na ushahidi upo. Ilhali hawa watu ni watanzania, wao au wazazi wao wanalipa kodi kuendesha taasisi hizo, ila taasisi zimejifanya ni chuo ama ni kamradi kao ati wanafunzi wataharibu vitu. How? Kwani wafanyakazi hawaharibu? Kwanini uconclude ataharibu kabla ya kuconclude atatengeneza?