KERO Kutozwa fedha kwa wanafunzi wanaohitaji kujifunza kwa vitendo katika taasisi za serikali ni sahihi na uungwana?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hivi hao wanaoenda field mtakuwa mnawapa gloves, au kama taasisi ina bajeti ya glove moja, itabidi wabadirishane na watoto wenu? Nani kawaambia kwamba ikiwa ni taasisi ya serikali basi yenyewe haina gharama za ziada?
Watu wanapenda sana mteremko. Wanadhani serikali inaweza shughulikia kila kitu.

Hii hapana na ni kitu kinakua kwa taifa letu kwa kasi mno watu wanajimilikisha ofisi za umma kama Mali zao. Ata kama tunachangamoto za kifadha na bajeti vitu kama mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi vipewe kipaombele. Wewe unaosema tunapenda " mteremko" ikitokea seminar ya malipo hizo hela zinapatikana unajilipa na unaenda. Shida ni uzalendo sifuri, ubinafsi, ufisadi na uchoyo
 
New members mnasapotiana bila kutueleza sisi expert members ni wapo mlitozwa pesa ili kufanya field,Mimi kama mwalimu,walimu wa field wakija shuleni kwetu Huwa tuna wasapoti kwa kuwapa makazi,chakula na fedha kidogo za kujikimu,sasa huko watozwako pesa ili kufanya field ni wapi?
Hospitalini; wanafunzi wa utabibu/udaktari, nurses, lab techs & scntsts
 
Kumtoza mwanafunzi kiasi cha fedha kinyume na utaratibu is unfair. Ada analipa mwanafunzi wa chuo cha serikali ni ndogo sana, pesa ya field ninkubwa kuliko ada. Unajua maana ya field? Usichanganye field na clinical rotation.
 
A
Naamini huu ujinga mtakuwa mmeanza kufanya baada ya Magufuli kufariki
Awapii huu utaratibu ni wakitambo mkuu 2018&2019 mimi na wenzamgu tulihangaika sana kufanya hizo Field hizo Hospitali hasa za mikoa wana utaratibu kabisa nafikiri ni Nchi nzims dakika za mwishon sana tukapata hospitali moja ya Private kubwa tu tuliombwa box moja la Gloves lenye Pieces 100 tu toka hapo sikufanya tena fields zangu hospital za GVT

Utaratibu upo na mnalipoa kwa Muhasibu kabisa
 
Sema ukweli; taasisi nyingi ni Hospitali na Zahanati za serikali kwa wanafunzi wa vyuo vya afya vya Private ndiyo wahanga wakubwa wa kutozwa hela wakienda field.
Mmmh mbona mimi kuna ndugu yangu na juzi alikuwa kwenye field kwenye hospitali ya serikali na wala hakutozwa hata senti tano?
 
Hivi hao wanaoenda field mtakuwa mnawapa gloves, au kama taasisi ina bajeti ya glove moja, itabidi wabadirishane na watoto wenu? Nani kawaambia kwamba ikiwa ni taasisi ya serikali basi yenyewe haina gharama za ziada?
Watu wanapenda sana mteremko. Wanadhani serikali inaweza shughulikia kila kitu.
Ni sawa kuchangia materials siyo tatizo, changamoto ni pale unapoombwa fedha nyingi unaweza kuta unaombwa mshahara wa mtu
Mfano mimi nimesoma psychology sihitaji hata sindano kufanya majukumu yangu ila nimeombwa 300k ili itumike wapi⁉️
 
New members mnasapotiana bila kutueleza sisi expert members ni wapo mlitozwa pesa ili kufanya field,Mimi kama mwalimu,walimu wa field wakija shuleni kwetu Huwa tuna wasapoti kwa kuwapa makazi,chakula na fedha kidogo za kujikimu,sasa huko watozwako pesa ili kufanya field ni wapi?
Zipo sehemu nyingi tu mfano hospital ya mkoa Iringa, mkoa wa mwanza pale sekoutoure
 
Mmmh mbona mimi kuna ndugu yangu na juzi alikuwa kwenye field kwenye hospitali ya serikali na wala hakutozwa hata senti tano?
Wewe hujui kitu! Alilipa kupitia chuo. Nitajie hospital nikueleze ni shs ngapi zinalipwa kwa idadi ya wanafunzi
 
New members mnasapotiana bila kutueleza sisi expert members ni wapo mlitozwa pesa ili kufanya field,Mimi kama mwalimu,walimu wa field wakija shuleni kwetu Huwa tuna wasapoti kwa kuwapa makazi,chakula na fedha kidogo za kujikimu,sasa huko watozwako pesa ili kufanya field ni wapi?
Hela zinazotozwa zinaambatanishwa katika Karo ya mwanafunzi. Lakini kila Chuo cha Private kinalipia field kuanzia Certificate, Diploma na Bachelor (MD).
 
Kumekuwa na utaratibu wa kutozwa fedha kwa wanafunzi wanaoenda kwenye taasisi mbalimbali za serikali kujifunza kwa vitendo. Hii ni sehemu ya kujifunza na pia kusaidia majukumu ya taasisi husika kwa kipindi fulani.

Badala yake, wanafunzi ndio wanaoombwa pesa nyingi ili kupata nafasi hiyo. Utaratibu wa kulipa ni kwa siku, wiki, na hata kwa mwezi. Mfano: mwanafunzi anaombwa kulipa elfu tano kwa siku kwa muda wa miezi mitatu na zaidi.

Je, serikali imezingatia hali za wanafunzi kama:
  • Kipato cha mwanafunzi, ikiwa hana chanzo kingine zaidi ya wazazi maskini.
  • Jukumu la ulipaji ada chuoni, ambapo hulipa ada sawa akiwa darasani.
  • Gharama za nauli na chakula.
  • Majukumu anayopatiwa.
Sasa tujiulize sote: je, suala hili ni sahihi kwa kundi hili linalohitaji jicho la upekee sana ili kutimiza ndoto na malengo ya kuijenga kesho bora? Ikiwa kijana anasoma kwa mateso na gharama nyingi, na baada ya hapo anarudi kuungana na jamii inayohitaji ajiajiri, mtaji unatoka wapi ikiwa alimaliza fedha kutafuta nafasi ya kujifunza kwa vitendo?
Unaweza taja ofisi inayofanya hivyo?
 
Hivi hao wanaoenda field mtakuwa mnawapa gloves, au kama taasisi ina bajeti ya glove moja, itabidi wabadirishane na watoto wenu? Nani kawaambia kwamba ikiwa ni taasisi ya serikali basi yenyewe haina gharama za ziada?
Watu wanapenda sana mteremko. Wanadhani serikali inaweza shughulikia kila kitu.
Kwani hizo gloves wanachezea?
 
Wewe hujui kitu! Alilipa kupitia chuo. Nitajie hospital nikueleze ni shs ngapi zinalipwa kwa idadi ya wanafunzi
Temeke Hospital. Pesa inayolipwa chuo ni kwa ajili costs mbalimbali ikiwemo usafiri wa kuwapeleka kwenye maeneo ya mafunzo/hospitali na kurudi chuo.
 
Inawezekana kukawa na gharama za field, ila zinatakiwa kuingizwa kwenye malipo ya chuo pamoja na gharama nyingine. Sio sahihi taasisi ya serikali kumlipisha mwanafunzi moja kwa moja.
 
Unafurahisha! Hujui Chuo kinalipa hata lawalawa ya MOI, katibu wa hospital, Head of Department etc. Na zinalipwa katika Account zao. Hujui kila mwanafunzi analipa hii kwa control number.

Kitu hujui ni bora kunyamaza. Tumehusika kulipa, kwa mantiki hiyo tuna uhakika na tunachozungumzia. Mwananyamala, Amana na hata Muhimbili uliza wanafunzi wa MD wa private hata CMT etc
 
Kumekuwa na utaratibu wa kutozwa fedha kwa wanafunzi wanaoenda kwenye taasisi mbalimbali za serikali kujifunza kwa vitendo. Hii ni sehemu ya kujifunza na pia kusaidia majukumu ya taasisi husika kwa kipindi fulani.

Badala yake, wanafunzi ndio wanaoombwa pesa nyingi ili kupata nafasi hiyo. Utaratibu wa kulipa ni kwa siku, wiki, na hata kwa mwezi. Mfano: mwanafunzi anaombwa kulipa elfu tano kwa siku kwa muda wa miezi mitatu na zaidi.

Je, serikali imezingatia hali za wanafunzi kama:
  • Kipato cha mwanafunzi, ikiwa hana chanzo kingine zaidi ya wazazi maskini.
  • Jukumu la ulipaji ada chuoni, ambapo hulipa ada sawa akiwa darasani.
  • Gharama za nauli na chakula.
  • Majukumu anayopatiwa.
Sasa tujiulize sote: je, suala hili ni sahihi kwa kundi hili linalohitaji jicho la upekee sana ili kutimiza ndoto na malengo ya kuijenga kesho bora? Ikiwa kijana anasoma kwa mateso na gharama nyingi, na baada ya hapo anarudi kuungana na jamii inayohitaji ajiajiri, mtaji unatoka wapi ikiwa alimaliza fedha kutafuta nafasi ya kujifunza kwa vitendo?
Taasisi gani hiyo, kataje
 
Inawezekana kukawa na gharama za field, ila zinatakiwa kuingizwa kwenye malipo ya chuo pamoja na gharama nyingine. Sio sahihi taasisi ya serikali kumlipisha mwanafunzi moja kwa moja.
Wanakidai chuo kwa idadi ya wanafunzi kilicho nacho. Na kwa taarifa yako, Chuo huwa hakina hela, hela hutoka kwa wanafunzi. Chuo ni mkusanyaji wa hela ya wanafunzi.
 
Unafurahisha! Hujui Chuo kinalipa hata lawalawa ya MOI, katibu wa hospital, Head of Department etc. Na zinalipwa katika Account zao. Hujui kila mwanafunzi analipa hii kwa control number.

Kitu hujui ni bora kunyamaza. Tumehusika kulipa, kwa mantiki hiyo tuna uhakika na tunachozungumzia. Mwananyamala, Amana na hata Muhimbili uliza wanafunzi wa MD wa private hata CMT etc
Chuo kipi hicho?
 
Back
Top Bottom