Uchaguzi 2020 Kutulazimisha wabunge tusiowachagua: Magufuli haogopi 'karma'?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Sio kila mtanzania ni CCM. Watanzania wasio na vyama bi wengi kuliko Wana CCM au wenye vyama vingine.

Kutulazimisha wote kumpitisha mbunge ambae hatujampigia kura sababu Tu ya kumuondoa mpinzani wake Kwa hila ni kutudharau na kutotuheshimu sisi ambao sio wananchama wa wa vyama.

Kutunyima haki ya kuchagua tunao wataka na kutubambikia wabunge ambao sio tuliowataka wala kuwachagua haki ya mtu haiendi bure mbinu zote za hila zinazofanywa bado mwisho kabisa kuna 'karma' karma haiangalii nafasi ya mtu ..kila dhuluma huwa inajibu ni suala la mda tu.

Magufuli kama Rais kazi yake ya kwanza ni kusimamia haki Kwa Taifa kugeuka na kusimamia dhuluma badala ya haki moja Kwa moja ni kutaka 'karma' ifanye kazi..

Je, yeye Magufuli haogopi karma?
 
Magufuli akiwa mbunge alikuwa anapita kwa mfumo huu ambao kwa sasa ameutambulisha nchi nzima.

Na kama tukiendelea kumchekea chekea akafanikiwa kuutekeleza basi wapinzani hatutapata nafasi tena kuchagua wagombea tunaowataka.

Tunatakiwa kuungana kuukomesha huu uhuni wa Chatoboy unaojaribu kupandikizwa nchini.
 
Kwani mwenye mamlaka ya kupitisha majina ni JPM au NEC, ??
Na pili sheria na taratibu si zinataka wajitokeze wengi kwa kazi yao, ili mradi wafuate sharia??
 
Kuielewa karma inahitaji kukua na sio kimwili ni kukua ki ufahamu na hapo ndo shida ilipo, maana kwenye Karma ndo kuna kanuni na sheria mama za maumbile hazijawahi athirika na muda wala ukuu wowote toka mwanzo, ni ku zi tii tu kadri ya uwezo wetu hakuna wa kukaa juu yake na wala hakuna siri isio ‘uchi’ kwenye Karma, na hauwezi ondoka ktk uso wa ardhi bila kusimama mbele yake‘be humble always’
 
TUKUTANE OCTOBER 28,ACHENI LONGOLONGO [emoji116]
 

Attachments

  • 20200829163552_IMG_0674.JPG
    130.7 KB · Views: 2
Kama haki hakuna tuilaumu NEC na sio JPM??
Wewe unaonaje ???
Na zaidi ya hapo kama haki imekosekana si kuna taratibu za kuidai kisheria na sio kisiasa na kwa vitisho kwani huko hakuthibitishi kanyimwa kwa hiyo haki
 
Hadi wewe umeandika haya??!!

Kweli kuna jambo litatokea mwaka huu!!! Hadi wana CCM mnahoji hili suala??? Kweli ukombozi umekaribia!
Alichoandika kina ukweli mkubwa sana, nami naongeza kitu kimoja alichokiacha mleta mada. Katiba yetu inatambua Wabunge wa aina 3 tu,
1.Wa kuchaguliwa
2.Wa viti Maalum
3.Wa kuteuliwa na Rais (10)
Sasa hawa Wabunge wanaotokana na mapingamizi wako kundi gani?
1.Wamechaguliwa - HAPANA
2.Ni viti maalum - HAPANA
3.Wametuliwa na Rais - HAPANA.
Sasa hawa wanawekwa kundi gani?
 
Mkuu nakubaliana na wewe, watawala waelewe kuwa wanasababisha watu wapoteze imani na mfumo tulionao wa kupata viongozi, unapowadharau watu kiasi hiki unawalazimisha watafute utaratibu mwingine wa kupata viongozi wanaowataka, kilicho kibaya zaidi matendo ya watawala yanahatarisha sio tu amani ya nchi bali pia mustakabali wa umoja na ustawi wa vizazi vijavyo na kama hatua stahiki hazitachukuliwa sasa hivi, itakuja kutulazimu kutumia muda na rasilimali nyingine kurekebisha makosa
 

Wamepitishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…