Kutumia dini kama kichaka cha kukwepa wajibu hakutotusaidia

Kutumia dini kama kichaka cha kukwepa wajibu hakutotusaidia

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Mwalimu Nyerere alisema kuwaasa viongozi kuwa kwa kiongozi kuwa aware na mambo ya dini nchini mwake ni jambo zuri lakini asijisahau na kuzama huko.

Imezuka Tabia sasa nchini mwetu, viongozi wanakwepa wajibu wa kutoa uongozi sahihi katika masuala mbalimbali na kutokana na kutowajibika huko athari zinapoanza kujitokeza wanakimbilia madhabahuni kutafuta huruma ya watu wa dini.

Tumeshuhudia mkuu wa mkoa mmoja nchini anakwenda redioni kabisa kuendesha misa, na si mara moja ni mara kadhaa ameonekana akienda katika madhabahu mbalimbali kwa minajili hiyo. Lakini ukitazama kwa makini kabisa timing, set up na vitu anavyoviongea vya kuchomekea siasa mtu mwenye akili unang'amua wazi kuwa madhabahu hapa yanatumika kutafuta sympathy ya umma kwa makosa ya kiuongozi na kisiasa. Kiufupi mtu anakua anataka kutumia dini kutafuta ushawishi na uungwaji mkono

Pia tatizo hili limejitokeza kipindi hiki cha Korona, Miongoni mwa hotuba za mwanzo za rais kulizungumzia suala hili la Korona ilikuwa ni madhabahuni huko kanisani, Katika hotuba hii ndipo alipoweka tone au muelekeo wa namna gani atapambana na hii korona. Huko. madhabahuni Raisi alisema Korona ni kagonjwa kadogo, "Kakorona", akasema kuwa korona ni shetani na atashindwa kwa damu ya Yesu. Maneno haya yaliplay down uzito wa tatizo, yakaresonate vizuri mno na mashabiki wa kidini (religious fundamentalist) wa makanisa ya kinabii, tukaona nao kwenye misa zilizofuata wakianza kushambulia baadhi ya vyama vya siasa na watu waliopinga namna rais na serikali yake inavyopambana na hii korona.

Tanzania ni Taifa la wenye kuamini uwepo wa Mungu, na ni Taifa linalompenda Mungu lakini kwa bahati mbaya Viongozi wetu wa kisiasa wanamanipulate tunu hii ya watanzania kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa na kupenyeza misimamo yao ambayo wanajua ni vigumu kwao kukubalika wakisimama na kuyasemea hayo kwenye majukwaa ya kisiasa. Yaani yale wanayoshindwa kuyatamka kwenye majukwaa ya kisiasa wanakwenda kuyatamka madhabahuni ili kutafuta huruma ya waumini pindi mambo yakiback fire.

Inashangaza sana, rais kusimama madhabahuni na kukejeli matumizi ya barokoa, Raisi anawasifu wasiovaa barakoa na wote kwa pamoja wanashangilia kwa vifijo.
Huko awali rais amewahi kusikika tena akisema kuwa tusitegemee haya mavitambaa kutusaidia bali tumtegemee Mungu!. Hivi Rais leo ameacha kazi ya uraisi na kugeuka muinjilisti?, amesahau kuwa yeye ni raisi wa wenye dini na wasio na dini?,Ok mathalani keshawaambia raia wake wenye kuamini uwepo wa Mungu kuwa wasitegemee mavitambaa je wale ambao wanaabudu mizimu au wanaoabudu ng'ombe au wasioabudu kabisa nao wategemee nani au nini kiwasaidie?.

Rais ajikite kwenye kazi ya uraisi, kutangaza dini awaachie wenye dini wenyewe

Jana nimemsikia kuwa yeye anampenda Yesu na Yesu ataishinda korona, lakini asichokielewa ni kwamba kuna Asilimia kubwa ya raia wake wanaamini huyo Yesu wake wala hana nguvu hizo anazifikiria yeye, wanamuona ni nabii tu aliyepewa uwezo mkubwa na Mungu miaka 2000 iliyopita na sasa yuko kwa Mungu na hayuko incharge ya maisha ya mtu yeyote hapa duniani kwa sasa. Sasa rais asidhani kuwa Imani yake ni imani ya watanzania wote, sisi tunachotaka ni atuongoze kwa misingi inayoresonate kwa wote, siyo kila Mtanzania ni Mkiristo, Siyo kila Mtanzania anaamini Yesu anaweza kuishinda Korona na kiufupi siyo kila mtanzania ni mlokole, Ulokole liwe jambo la mtu binafsi tusililete kwenye dira za kitaifa za kuongoza maamuzi ya kiserikali.

Tuliona Rais aliitisha maombi ya kumuomba Mungu siku tatu

Kisha Waziri mkuu akaitisha ya kwake

Ummy Mwalimu naye akaitisha yake

Jana tena rais anaitisha maombi ya kumshukuru Mungu

Tunaitisha haya maombi mbona basi namna mnavyotenda mambo yenu, maamuzi yenu haziakisi ukweli wa Mungu?.

Taarifa zenu juu ya takwimu za korona zina ukakasi, Measures zenu juu ya kupunguza usambaaji wa korona zina ukakasi, Namna mnavyofanya huko bungeni ubabe wa kutoheshimu katiba na sheria za nchi kwenye maamuzi yenu vina ukakasi. Je kweli nyinyi mnamtegemea Mungu kama mnavyotaka tuamini au mnataka kutumia Jina lake kutafuta cover ya kufeli kwenu ili hasira ya umma isiwaangukie?
Mungu hadhihakiwi, nyie chezeeni jina lake mje muone mwisho wake.

Nimalizie kwa kusema, hatukupiga kura kumchagua rais ili akawe askofu mwenye kutufundisha tufanye nini kwenye mambo ya dini zetu, tulichagua kiongozi wa kisiasa ili akatumie mamlaka aliyopewa akaongoze nchi kwa kufuata misingi ya sheria na katiba.

Kwenye ugonjwa huu wa Korona tunahitaji uongozi sahihi wa namna ya kupambana, tusimshirikishe Mungu kucover uzembe wetu
 
Tanzania ni Taifa la wenye kuamini uwepo wa Mungu, na ni Taifa linalompenda Mungu lakini kwa bahati mbaya Viongozi wetu wa kisiasa wanamanipulate tunu hii ya watanzania kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa na kupenyeza misimamo yao ambayo wanajua ni vigumu kwao kukubalika wakisimama kwenye majukwaa ya kisiasa. Yaani yale wanayoshindwa kuyatamka kwenye majukwaa ya kisiasa wanakwenda kuyatamka madhabahuni ili kutafuta huruma ya waumini pindi mambo yakiback fire.
Na anajua kuwa watanzania by 98% ni malofa wa dini! He can manipulate them the way he likes!
 
Kama kipindi Iddi Amini Raisi angekuwa ni huyu wala asingehangaika sana

Angewaita Maaskofu na Mashehe na kuwaambia waliombee Taifa kwa siku tatu mfululizo

Kwakweli Iddi Amini angecheka sana
 
Kama kipindi Iddi Amini Raisi angekuwa ni huyu wala asingehangaika sana

Angewaita Maaskofu na Mashehe na kuwaambia waliombee Taifa kwa siku tatu mfululizo

Kwakweli Iddi Amini angecheka sana
Hahah leo M7 ataongea ngoja tuone atasemaje.
 
Mwalimu Nyerere alisema kuwaasa viongozi kuwa kwa kiongozi kuwa aware na mambo ya dini nchini mwake lakini asijisahau na kuzama huko.
Hilo neno Nyerere alilisemea wapi na lini? tuwekee ushahidi mwongo mkubwa wewe unasingizia hadi marehemu
 
Magufuli talks about God but he doesn't live in God spirit at all.
Kwanza hatendi haki katika nchi, haheshimu kiapo chake cha kulinda na kutetea katiba maana anaivunjavunja kila anapojisikia.

Sasa akija kipindi hiki cha Korona na kujifanya mcha Mungu tunajua tu kuwa anataka kulitumia jina la Mungu kisiasa, hana dhati wala kweli yoyote moyoni wala fikra zake

Sisi hatudanganyiki hata kidogo
 
Hawa Viongozi wanaojifanya kukimbilia Makanisani na Mabulungutu ya fedha mchana

Usiku unawakuta wakigawa mabulungutu kwa waganga wa kienyeji huku wakitoa shukurani zao za dhati kwa kupigwa chale
 
Anaacha kutenga bajeti maalum bungeni kwa ajili ya kupambana na Korona nchini anakwenda kugawa fedha madhabahuni, kama hii siyo rushwa ya kuwanyamazisha watu wa dini wasiongee ni nini?

Nategemea hata siku ya Iddi kufanya mchezo huohuo wa kugawa fedha kwa BAKWATA ili aonekane mwema na kutafuta kununua uungwaji mkono kwa waislamu ili kupunguza lawama na shutuma za jinsi anavyohandle suala hii la Korona.
Korona inaua watu jamani huku mitaani tuache utani!
 
Kama RC angekuwa Muislamu na kufanya yale aliyofanya Makonda, hali ingekuwaje?

Loh, loh, loh ingekuwa kelele nchi nzima, humu JF watu wangeponda sana.

Kuna vitu humu nchini Christians wanaweza kufanya na wakago away easily bila lawama, lakini if the same thing ingefanywa na muislamu inakuwa nongwa isiyosemekana.

Just Imagine rais angekuwa Muislam kisha aseme "Allah ataondoa Korona msitegemee vitambaa hivi (barakoa)" kisha uje uone shughuli au response yake

Mfano mwingine ni rahisi nchini kiongozi wa Kikristo kutoa hotuba ya kisiasa na kuanza kunukuu biblia kama Zaburi etc mara nyinginyingi tu katika hotuba yake, but Muislamu akitoa hotuba akinukuu quran basi hulazimika kunukuuu kidogo na siyo mara kwa mara na pia at the same time inabidi anukuu na biblia in the same set up ili kubalance la sivyo watu huanza kumuona kama analeta udini hivi.
 
pia mashehe wenu wakuu wana matatzo pia ustolee mfno wakristo tu ingawa na wenyewe siwakubali

Ila story usiiweke biased

Mkulima wa mahindi
 
Back
Top Bottom