Kutumia dini kama kichaka cha kukwepa wajibu hakutotusaidia

Kutumia dini kama kichaka cha kukwepa wajibu hakutotusaidia

Magufuli talks about God but he doesn't live in God spirit at all.
Kwanza hatendi haki katika nchi, haheshimu kiapo chake cha kulinda na kutetea katiba maana anaivunjavunja kila anapojisikia.

Sasa akija kipindi hiki cha Korona na kujifanya mcha Mungu tunajua tu kuwa anataka kulitumia jina la Mungu kisiasa, hana dhati wala kweli yoyote moyoni wala fikra zake

Sisi hatudanganyiki hata kidogo
Swali ni je hao viongozi wa dini hili limewashinda vipi kuling'amua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaacha kutenga bajeti maalum bungeni kwa ajili ya kupambana na Korona nchini anakwenda kugawa fedha madhabahuni, kama hii siyo rushwa ya kuwanyamazisha watu wa dini wasiongee ni nini?

Nategemea hata siku ya Iddi kufanya mchezo huohuo wa kugawa fedha kwa BAKWATA ili aonekane mwema na kutafuta kununua uungwaji mkono kwa waislamu ili kupunguza lawama na shutuma za jinsi anavyohandle suala hii la Korona.
Korona inaua watu jamani huku mitaani tuache utani!
I wonder if the word ethics is known to our beloved leaders.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Opium of the people - Wikipedia
IMG_20200518_083027_672.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaacha kutenga bajeti maalum bungeni kwa ajili ya kupambana na Korona nchini anakwenda kugawa fedha madhabahuni, kama hii siyo rushwa ya kuwanyamazisha watu wa dini wasiongee ni nini?
Sisi mtaani kwetu toka corona ianze hakuna mgonjwa hata mmoja wa corona na hakuna anaayeumwa corona wala aliyekufa kwa corona hiyo bajeti hatuiihitaji

unataka aitenge kwa ajili ya mtoto wa Mbowe aliyeumwa corona au? maana yake mbowe kwa kukuza mambo hajambo .Mwanawe kuumwa tu Corona ikawa nongwa akataka wabunge wote wa chadema wawekwe lockdown watake wasitake kisa mwanawe kaumwa!! na mibunge mingi ya Chadema ilivyo mijinga ikakubali ikawekwa lockdown ikapoteza mamilioni ya pesa za vikao na perdiem walizotakiwa kurudisha bungeni!!!

mtaani kwetu hatuhitaji hiyo bajeti ya nini wakati barakoa zinauzwa hadi mia tano na majani ya kujifukizia yako kibao kila kona tena bure ni wewe tu kuchuma kuchemsha na kujifukiza uwe huumwi au unaumwa ukijilia tangawizi yako na malimao umemaliza
 
yaani mmekaa mnaombea mabaya ili utabiri wenu wa miezi kadhaa nyuma utimie lakini waapi.

sasa matako yanawatetemeka hamjui mshike lipi.kwa saa hizi kila nyumbu ni mwana falsafa.

wakati ambao dunia nzima imeaua kupambana na huu ugonjwa na natokeo kuwa mabaya kabisa,mnampangia mtu silaha ya kutumia???
 
Sisi mtaani kwetu toka corona ianze hakuna mgonjwa hata mmoja wa corona na hakuna anaayeumwa corona wala aliyekufa kwa corona hiyo bajeti hatuiihitaji

unataka aitenge kwa ajili ya mtoto wa Mbowe aliyeumwa corona au? maana yake mbowe kwa kukuza mambo hajambo .Mwanawe kuumwa tu Corona ikawa nongwa anata wabunge wote wa chadema wawekwe lockdown watake wasitake kisa mwanawe kaumwa!! na mibunge mingi ya Chadema ilivyo mijinga ikakubali ikawekwa lockdown ikapoteza mamilioni ya pesa za vikao na perdiem walizotakiwa kurudisha bungeni!!!

mtaani kwetu hatuhitaji hiyo bajeti ya nini wakati barakoa zinauzwa hadi mia tano na majani ya kujifukizia yako kibao kila kona tena bure ni wewe tu kuchuma kuchemsha na kujifukiza uwe huumwi au unaumwa ukijilia tangawizi yako na malimao umemaliza
haya ndio mafisi yamekaa widharani yakiuangalia huu ugonjwa kama fulsa.

ndio maana mengi yao,WHO ilipokosa kutoa mkopo wa mapambano TZ, yakapanick.

jitu limekaa linaombea lockdown,na wakati huo huo pesa ya bajeti itengwe lianze kukata fungu kama keki yake ya harusi[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1],magu akaona hiyooooo.
 
yaani mmekaa mnaombea mabaya ili utabiri wenu wa miezi kadhaa nyuma utimie lakini waapi.

sasa matako yanawatetemeka hamjui mshike lipi.kwa saa hizi kila nyumbu ni mwana falsafa.

wakati ambao dunia nzima imeaua kupambana na huu ugonjwa na natokeo kuwa mabaya kabisa,mnampangia mtu silaha ya kutumia???
Vipi hapajachanganywa siasa na dini hapo.Au Hadi upinzani ndio utamuona msajili
 
Huwezi kuanza sentensi na herufi ndogo, nobody will take you seriously.

Sent using Jamii Forums mobile app
who can you put their names here? have you done a research on all people in the world to prove your conclusion?

mpambavu wa takwimu wewe sema some dont say anybody!!! when yo say some it includes you but if you say nobody it includes all bodied beings including americans,europeans,all africans,Asiasians ,cows,goats,pigs because all have bodies according to bioloogy subject!!! so goats and pigs know how to read and write ? so they know the difference between capital letter and small letter mjinga mkubwa wewe
 
who can you put their names here? have you done a research on all people in the world to prove your conclusion?

mpambavu wa takwimu wewe sema some dont say anybody!!! when yo say some it includes you but if you say nobody it includes all bodied beings including americans,europeans,all africans,Asiasians ,cows,goats,pigs because all have bodies according to bioloogy subject!!! so goats and pigs know how to read and write ? so they know the difference between capital letter and small letter mjinga mkubwa wewe

Yehodaya, unaunga mkono suala la Raisi kufurahishwa na kuwapongeza waumininkutovaa barakoa katika mkusanyiko ule?
 
Yehodaya, unaunga mkono suala la Raisi kufurahishwa na kuwapongeza waumini kutovaa barakoa katika mkusanyiko ule?
Ndio nafurahishwa na kumpongeza sababu naamini Mungu sio kirusi cha corona hawezi kuwagawia waumini kanisani corona wakiwa wanamwabudu.
 
Mwalimu Nyerere alisema kuwaasa viongozi kuwa kwa kiongozi kuwa aware na mambo ya dini nchini mwake ni jambo zuri lakini asijisahau na kuzama huko.

Imezuka Tabia sasa nchini mwetu, viongozi wanakwepa wajibu wa kutoa uongozi sahihi katika masuala mbalimbali na kutokana na kutowajibika huko athari zinapoanza kujitokeza wanakimbilia madhabahuni kutafuta huruma ya watu wa dini.

Tumeshuhudia mkuu wa mkoa mmoja nchini anakwenda redioni kabisa kuendesha misa, na si mara moja ni mara kadhaa ameonekana akienda katika madhabahu mbalimbali kwa minajili hiyo. Lakini ukitazama kwa makini kabisa timing, set up na vitu anavyoviongea vya kuchomekea siasa mtu mwenye akili unang'amua wazi kuwa madhabahu hapa yanatumika kutafuta sympathy ya umma kwa makosa ya kiuongozi na kisiasa. Kiufupi mtu anakua anataka kutumia dini kutafuta ushawishi na uungwaji mkono

Pia tatizo hili limejitokeza kipindi hiki cha Korona, Miongoni mwa hotuba za mwanzo za rais kulizungumzia suala hili la Korona ilikuwa ni madhabahuni huko kanisani, Katika hotuba hii ndipo alipoweka tone au muelekeo wa namna gani atapambana na hii korona. Huko. madhabahuni Raisi alisema Korona ni kagonjwa kadogo, "Kakorona", akasema kuwa korona ni shetani na atashindwa kwa damu ya Yesu. Maneno haya yaliplay down uzito wa tatizo, yakaresonate vizuri mno na mashabiki wa kidini (religious fundamentalist) wa makanisa ya kinabii, tukaona nao kwenye misa zilizofuata wakianza kushambulia baadhi ya vyama vya siasa na watu waliopinga namna rais na serikali yake inavyopambana na hii korona.

Tanzania ni Taifa la wenye kuamini uwepo wa Mungu, na ni Taifa linalompenda Mungu lakini kwa bahati mbaya Viongozi wetu wa kisiasa wanamanipulate tunu hii ya watanzania kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa na kupenyeza misimamo yao ambayo wanajua ni vigumu kwao kukubalika wakisimama na kuyasemea hayo kwenye majukwaa ya kisiasa. Yaani yale wanayoshindwa kuyatamka kwenye majukwaa ya kisiasa wanakwenda kuyatamka madhabahuni ili kutafuta huruma ya waumini pindi mambo yakiback fire.

Inashangaza sana, rais kusimama madhabahuni na kukejeli matumizi ya barokoa, Raisi anawasifu wasiovaa barakoa na wote kwa pamoja wanashangilia kwa vifijo.
Huko awali rais amewahi kusikika tena akisema kuwa tusitegemee haya mavitambaa kutusaidia bali tumtegemee Mungu!. Hivi Rais leo ameacha kazi ya uraisi na kugeuka muinjilisti?, amesahau kuwa yeye ni raisi wa wenye dini na wasio na dini?,Ok mathalani keshawaambia raia wake wenye kuamini uwepo wa Mungu kuwa wasitegemee mavitambaa je wale ambao wanaabudu mizimu au wanaoabudu ng'ombe au wasioabudu kabisa nao wategemee nani au nini kiwasaidie?.

Rais ajikite kwenye kazi ya uraisi, kutangaza dini awaachie wenye dini wenyewe

Jana nimemsikia kuwa yeye anampenda Yesu na Yesu ataishinda korona, lakini asichokielewa ni kwamba kuna Asilimia kubwa ya raia wake wanaamini huyo Yesu wake wala hana nguvu hizo anazifikiria yeye, wanamuona ni nabii tu aliyepewa uwezo mkubwa na Mungu miaka 2000 iliyopita na sasa yuko kwa Mungu na hayuko incharge ya maisha ya mtu yeyote hapa duniani kwa sasa. Sasa rais asidhani kuwa Imani yake ni imani ya watanzania wote, sisi tunachotaka ni atuongoze kwa misingi inayoresonate kwa wote, siyo kila Mtanzania ni Mkiristo, Siyo kila Mtanzania anaamini Yesu anaweza kuishinda Korona na kiufupi siyo kila mtanzania ni mlokole, Ulokole liwe jambo la mtu binafsi tusililete kwenye dira za kitaifa za kuongoza maamuzi ya kiserikali.

Tuliona Rais aliitisha maombi ya kumuomba Mungu siku tatu

Kisha Waziri mkuu akaitisha ya kwake

Ummy Mwalimu naye akaitisha yake

Jana tena rais anaitisha maombi ya kumshukuru Mungu

Tunaitisha haya maombi mbona basi namna mnavyotenda mambo yenu, maamuzi yenu haziakisi ukweli wa Mungu?.

Taarifa zenu juu ya takwimu za korona zina ukakasi, Measures zenu juu ya kupunguza usambaaji wa korona zina ukakasi, Namna mnavyofanya huko bungeni ubabe wa kutoheshimu katiba na sheria za nchi kwenye maamuzi yenu vina ukakasi. Je kweli nyinyi mnamtegemea Mungu kama mnavyotaka tuamini au mnataka kutumia Jina lake kutafuta cover ya kufeli kwenu ili hasira ya umma isiwaangukie?
Mungu hadhihakiwi, nyie chezeeni jina lake mje muone mwisho wake.

Ninalizie kwa kusema, hatukupiga kura kumchagua rais ili akawe askofu mwenye kutufundisha tufanye nini kwenye mambo ya dini zetu, tulichagua kiongozi wa kisiasa ili akatumie mamlaka aliyopewa akaongoze nchi kwa kufuata misingi ya sheria na katiba.

Kwenye ugonjwa huu wa Korona tunahitaji uongozi sahihi wa namna ya kupambana, tusimshirikishe Mungu kucover uzembe wetu
Aisee mnapata taabu Sana.....come October JPM atashinda kwa zaidi ya asilimia 95 ...Chadema haitapata zaidi ya viti vitano...
 
Ndio nafurahishwa na kumpongeza sababu naamini Mungu sio kirusi cha corona hawezi kuwagawia waumini kanisani corona wakiwa wanamwabudu.
Img-1589782284895.jpg



Coronavirus: South Korea church leader apologises for virus spread

The head of the religious sect that has been at the centre of the coronavirus outbreak in South Korea has apologised to the nation for the disease's spread.

Lee Man-hee, the leader of the Shincheonji Church of Jesus, got on his knees and bowed at a news conference.

About 60% of the country's more than 4,000 confirmed cases are sect members. Deaths nationwide now stand at 28.

Fatalities globally have now passed the 3,000 mark, although the vast majority are in China, where the outbreak began.

Worldwide, there have been almost 90,000 confirmed cases, with the numbers outside China now growing faster than inside China

Prosecutors in South Korea have been asked to investigate Mr Lee on possible charges of gross negligence.

"Although it was not intentional, many people have been infected," said the 88-year-old leader. "We put our utmost efforts, but were unable to prevent it all."

Of the confirmed cases, about 75% are from the southern city of Daegu and 73% of those have been linked to the Shincheonji Church.

In the capital, Seoul, the mayor urged the city's 10 million residents to work from home and to avoid crowded places.

Source: S Korea sect leader apologises for virus spread
 
Vipi hapajachanganywa siasa na dini hapo.Au Hadi upinzani ndio utamuona msajili
inabidi uwe specific kuchanganya siasa na dini ni kufanya nini na nini.rais kuingia kanisani na kuhutubia ni kuchanganya siasa na dini!!!!
 
Tanzania naona sasa tunarudi kwenye enzi za mawe, kudharau Sayansi na kujikita kwenye kutatua matatizo yetu kwa njia walizotumia mababu zetu katika karne ya 15, 16, 17 na 18 - is this the right way of doing things?

Tujiulize kwa umoja wetu, maana kupanga ni kuchagua.
 
Kwenye makanisa wamejaa wajinga wengi sn, ndiyo maana ukiangalia hao mitume ni matajiri wa kupindukia lakini waumini wao ni mafukara haswa. 2020 kuna uchaguzi hivyo kuna kura nyingi sana makanisani.
 
Kwanini makanisa kila kukicha yanakuwa sehemu ya siasa? je wapinzani wakianza kupewa nafasi nao kuongea makanisani najua watawala watanuna sana na kuwashughulikia
 
Back
Top Bottom