Kutumia Msalaba kama ishara ya ukristo na kanisa si sahihi

Kutumia Msalaba kama ishara ya ukristo na kanisa si sahihi

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Msalaba ni zana ya kunyongea wahalifu ya utawala wa Warumi (weapon of execution) kama ilivyo kamba ya kunyogea, kiti cha umeme, sindano ya sumu au jambia la kuchinjia.

Kama Yesu angechinjwa kwa jambia je tungekuwa tunaweka alama ya ya upanga/jambia juu ya jengo la kanisa au kuivaa kifuani?
 
Kwa hiyo ulitaka watumie ishara gani? Huoni ni kupitia huo msalaba Wakristo wengi ndiyo wametambua Masiya wao aliteswa na kuuwawa kikatili juu ya huo msalaba?
Nakuheshimu sana mkuu lakini waliosulibiwa kwenye msalaba siyo Yesu peke yake. Maelfu walinyongwa kwa njia hiyo kwa hiyo hiyo siyo alama ya Yesu Kristo
 
Kwa uelewa wangu msalaba huwa unatumika kama ukumbusho wa Yesu kufa msalabani,Sioni ww una tatizo gani hapo?
Na wale majambazi na wauaji na wahaini waliotundikwa kwenye misalaba ya wakoloni wa Kirumi je??
 
Kwa uelewa wangu msalaba huwa unatumika kama ukumbusho wa Yesu kufa msalabani,Sioni ww una tatizo gani hapo?
Yesu hakuwa wa kwanza kusulibiwa. Soma hata secular history tu. Ilikuwa adhabu ya wakoloni Warumi for anyone who messes with the authority. Ukileta za kuleta unatundikwa msalabani mahali ambapo watu wengi wanapita ili wakiona suluba unayopata wasijaribu kucheza na mkoloni
 
Kwa hiyo ulitaka watumie ishara gani? Huoni ni kupitia huo msalaba Wakristo wengi ndiyo wametambua Masiya wao aliteswa na kuuwawa kikatili juu ya huo msalaba?
Kanisa lilianza kutumia msalaba kama alama yake, miaka mia nne baada ya yesu kuondoka
 
Kwahiyo kilawalichotumia warumi wakristo hawafai kutumia?
Mbona sisi tuna tamaduni nyingi za kiarabu lakini zinaingiliana na uislam
Sijasema hakiruhusiwi kutumia. Nimesema msalaba haumuwakilishi Yesu Kristo. Ni zana ya kunyogea wahalifu
 
Yesu hakuwa wa kwanza kusulibiwa. Soma hata secular history tu. Ilikuwa adhabu ya wakoloni Warumi for anyone who messes with the authority. Ukileta za kuleta unatundikwa msalabani mahali ambapo watu wengi wanapita ili wakiona suluba unayopata wasijaribu kucheza na mkoloni
Ukiangalia documentary ya Jesus:his life,utagundua mengi, ilikua pure politics,wakitupiana mipira mtawala wa galilaya na huyo aliyemsulubu,niliiona channel ya history, DStv
 
Na wale majambazi na wauaji na wahaini waliotundikwa kwenye misalaba ya wakoloni wa Kirumi je??
Halafu wanadanganya watu na kujidanganya wenyewe ukiutishia uchawi/jini msalaba basi uchawi/jini unaondoka
 
Msalaba ni zana ya kunyongea wahalifu ya utawala wa Warumi (weapon of execution) kama ilivyo kamba ya kunyogea, kiti cha umeme, sindano ya sumu au jambia la kuchinjia. Kama Yesu angechinjwa kwa jambia je tungekuwa tunaweka alama ya ya upanga/jambia juu ya jengo la kanisa au kuivaa kifuani???
Imani ni kitu huru sana. Ukiona watu ulionao wanaenda tofauti na unavyowaza, hauna haja ya kuwasumbua watu kuwalazimisha wakusikilize, ni kiasi tu cha wewe kujitoa hapo na wewe uanzishe dhehebu lako, ukalisajili serikalini
 
Kwahiyo kilawalichotumia warumi wakristo hawafai kutumia?
Mbona sisi tuna tamaduni nyingi za kiarabu lakini zinaingiliana na uislam
Na ukumbuke pia siyo madhehebu yote ya kikristo wala secular history inakubaliana na structure ya huo msalaba. Wengine huamini it it was a single straight pole. Yaani nguzo moja tu iliyonyooka. Inawezekana ile ya Yesu ilikuwa na kipande cha begani au ile aliyoichukua mabegani akitoka pale kwa Pilato ndiyo hiyo tu maaskari walimpigilia humo. Miti ni kitu adimu kule Israeli na kutumia miti mingi kuua wahalifu ni jambo lisilofikirika!
 
Back
Top Bottom