Kutumia Msalaba kama ishara ya ukristo na kanisa si sahihi

Ukiangalia documentary ya Jesus:his life,utagundua mengi, ilikua pure politics,wakitupiana mipira mtawala wa galilaya na huyo aliyemsulubu,niliiona channel ya history, DStv
Sijawahi kuiona. Ngoja nitaiangalia
 
Msalaba ni zana ya kunyongea wahalifu ya utawala wa Warumi (weapon of execution) kama ilivyo kamba ya kunyogea, kiti cha umeme, sindano ya sumu au jambia la kuchinjia. Kama Yesu angechinjwa kwa jambia je tungekuwa tunaweka alama ya ya upanga/jambia juu ya jengo la kanisa au kuivaa kifuani???
Kwahiyo unashauri tutumie mfuko wa cement
 
Msalaba ni zana ya kunyongea wahalifu ya utawala wa Warumi (weapon of execution) kama ilivyo kamba ya kunyogea, kiti cha umeme, sindano ya sumu au jambia la kuchinjia. Kama Yesu angechinjwa kwa jambia je tungekuwa tunaweka alama ya ya upanga/jambia juu ya jengo la kanisa au kuivaa kifuani???
Shida iko wapi? mbona hiyo ni alama tu, dini zingine zina alama ya michoro na maumbile tofauti ni sawa tu, hata ingekuwa panga ni sawa tu, mbona kuna dini za asia zina alama ya jambia
 
Kanisa lilianza kutumia msalaba kama alama yake, miaka mia nne baada ya yesu kuondoka
Angalau wewe una uelewa wa historia ya ukristo. Asante
Lengo la hii mada yako ni kutaka kujua historia ya lini Kanisa lilianza kutumia alama ya msalaba, au ni kutaka kufahamu kama ni sahihi kwa Ukristo/Wakristo kutumia alama ya msalaba Kanisani?

Mimi nimekujibu kulingana na ulivyo uliza. Ya kwamba matumizi ya alama msalaba yanatumiwa na Wakristo kama kumbukumbu ya Masiya wao kuteswa na kuuwawa kwa kutumia msalaba! Ni kupitia alama ya msalaba kila Mkristo anatumbua Yesu aliteswa na kufa msalabani. Shida iko wapo ukiendelea kutumika kama ukumbusho kwa vizazi na vizazi?

Kwa hiyo siyo vizuri kuleta mada jukwaani, huku ukiwa tayari na mtazamo/majibu yako.
 
Shida iko wapi? mbona hiyo ni alama tu, dini zingine zina alama ya michoro na maumbile tofauti ni sawa tu, hata ingekuwa panga ni sawa tu, mbona kuna dini za asia zina alama ya jambia
Mkuu nimeongelelea imani ya kikristo. Theolojia (Tauhid) yetu ni tofauti kabisa na hizo imani zingine ila kwa suala hili ndio maana niewaalika maaskofu,mapadri, wachungaji, maprofesa wa Theology tulijadili
 
Lengo la hii mada yako ni kutaka kujua historia ya lini Kanisa lilianza kutumia alama ya msalaba, au ni kutaka kufahamu kama ni sahihi kwa Ukristo/Wakristo kutumia alama ya msalaba Kanisani?

Mimi nimekujibu kulingana na ulivyo uliza. Ya kwamba matumizi ya alama msalaba yanatumiwa na Wakristo kama kumbukumbu ya Masiya wao kuteswa na kuuwawa kwa kutumia msalaba! Ni kupitia alama ya msalaba kila Mkristo anatumbua Yesu aliteswa na kufa msalabani. Shida iko wapo ukiendelea kutumika kama ukumbusho kwa vizazi na vizazi?

Kwa hiyo siyo vizuri kuleta mada jukwaani, huku ukiwa tayari na mtazamo/majibu yako.
Mkuu, everything can be debated. Sasa nikija kwenye debate bila kuwa na mtazamo wangu hiyo siyo debate tena. Nimeleta hoja na ijibiwe kwa hoja.
 
We watu wanamuita binadamu mungu, na Mama yake wanamuita mama wa mungu hao watu akili watatoa wapi
 
Lengo la hii mada yako ni kutaka kujua historia ya lini Kanisa lilianza kutumia alama ya msalaba, au ni kutaka kufahamu kama ni sahihi kwa Ukristo/Wakristo kutumia alama ya msalaba Kanisani?

Mimi nimekujibu kulingana na ulivyo uliza. Ya kwamba matumizi ya alama msalaba yanatumiwa na Wakristo kama kumbukumbu ya Masiya wao kuteswa na kuuwawa kwa kutumia msalaba! Ni kupitia alama ya msalaba kila Mkristo anatumbua Yesu aliteswa na kufa msalabani. Shida iko wapo ukiendelea kutumika kama ukumbusho kwa vizazi na vizazi?

Kwa hiyo siyo vizuri kuleta mada jukwaani, huku ukiwa tayari na mtazamo/majibu yako.
Pia naomba unipe uhakika kama huo msalaba una structure hiyo inayotumiwa na wakristo. Maana injili inasema aliondoka pale mahakamani AKIJUCHUKULIA MSALABA WAKE. Unataka kuniambia alibeba magogo yote mawili baaada ya ile mijeledi 40 ambayo lengo ni kummaliza mhalifu nguvu akitundikwa afe upesi??
 
We watu wanamuita binadamu mungu, na Mama yake wanamuita mama wa mungu hao watu akili watatoa wapi
Kuna shida ya ufahamu. Mimi ni mkristo lakini nikiona mahali pamepotoka lazima tuwekane sawa. I am not a conservative Christian!
 
Nakuheshimu sana mkuu lakini waliosulibiwa kwenye msalaba siyo Yesu peke yake. Maelfu walinyongwa kwa njia hiyo kwa hiyo hiyo siyo alama ya Yesu Kristo
Toa mapendekezo itumike ishara gani. Kama haitakiwi kabisa, anzisha kanisa au huduma yako, tutatoa sadaka
 
Lile gogo moja tu alilibeba lilimwelemea ikabidi askari wamlazimishe mzee mmoja alikuwa anatoka shambani huko Kirene ( (Cyrene) amsaidie kulibeba. Kile kipigo cha mijeledi kilikuwa ni hatari. Zile kamba walikuwa wanaweka vitu vyenye ncha kali kama vyuma au mifupa. Akipiga moja akitoa inatoka na nyama yako. Sasa fikiri vipigo arobaini!
 
Toa mapendekezo itumike ishara gani. Kama haitakiwi kabisa, anzisha kanisa au huduma yako, tutatoa sadaka
Sadaka tena? Sina njaa hiyo mkuu. Nchi tajiri hii nikose akili nianze kuhubiria watu utapeli wa kiroho? Nimesema hata kwenye hilo la msalaba hakuna mwenye uhakika structure yake iliyotumika kumuua Yesu ilikuwaje. Ilikuwa ngozo moja au nguzo na kipande cha mabegani that is a matter of debate. . Kwa kile kipigo cha pale mahakamani kubeba magogo mawili ni jambo lisililofikirika!
 
Kwa akili ya kawaida tu huwezi kumning’iniza shingoni akiwa uchi unayemuheshimu,chukuliani mfano baba yako mzazi unaweza mvaashingoni akiwa uchi!!!.
 
Msalaba ni zana ya kunyongea wahalifu ya utawala wa Warumi (weapon of execution) kama ilivyo kamba ya kunyogea, kiti cha umeme, sindano ya sumu au jambia la kuchinjia. Kama Yesu angechinjwa kwa jambia je tungekuwa tunaweka alama ya ya upanga/jambia juu ya jengo la kanisa au kuivaa kifuani???
Ndio, kama Yesu angeuwawa kwa bunduki tungeweka bunduki kuwa ishara ya Kanisa au Ukristo! Yesu mwenyewe anasema hakuja kwa ajili ya wenye afya, amekuja kwa ajili ya wagonjwa ili wapate afya. Yesu na Ukristo ni mwanamapinduzi. Kuna vitu vingi sana mwanzoni vilikuwa ishara ya mabaya lakini Yesu amekuja na kuvibadilisha kuwa ishara ya wema. Na hakuna ushindi kama kutumia kilichokuwa kinatumiwa kwa uovu na sasa kuwa ndio zana ya kutendea mema! Hiyo ndio inammaliza kabisa shetani. Msalaba ni mojawapo tu ya mifano hiyo, ipo mingi.
 
Back
Top Bottom