Mimi sifahamu Mungu anaongea lugha gani.Pia naamini Mungu haongei kiarabu.Wewe unaweza kuniambia Mungu anaongea lugha gani??
Unasahau hata ulichoandika mwanzo,ulidhihaki waislam kutumia kiarabu,ukauliza huyo Mungu anaongea kiarabu tu,nikakuuliza Mungu anaongea lugha gani,so unapaswa kujibu, kusema hujui Mungu anaongea lugha gani siyo jibu
Nimekuambia vazi kuu la waarabu ni vazi gani,waislamu vazi kuu ni vazi gani?? Wewe umeelezea jinsi ya kuvaa hilo vazi
Waislam hawana vazi kuu, isipokua hijabu kwa wanawake,na hijab ni amri ya Quran, waarabu hawakuvaa hijab kabla ya uislam,kama unadhani kanzu ni vazi kuu la waarabu basi kumbuka yesu na warumi walivaa kabla muhammad hajazaliwa
.
Ndoa za mitala ilikuwa sehemu ya utamaduni wa kiarabu, uislamu haukulikataza.Wewe umeelezea taratibu za ndoa.
Mitala mfalme selemani alikua nayo kule israel,ulaya walikua nayo, africa kwa wingi,mitala siyo utamaduni wa kiarabu
Unaweza kuelezea taratibu za ndoa za utamaduni wa kiarabu??
Hili inabidi ueleze wewe unayezijua taratibu za ndoa za kiarabu kabla ya uislam,maana umedai uislam umeiga huko
Dini haiwezi kuwa mfumo wa maisha, dini ni sehemu ya utamaduni.
Wewe kwa kutumia akili yako, kipi ni kikubwa kati ya utamaduni na dini??
Uelewa wako wa dini ndiyo upo hivyo,lakini uislam unasimamia/elekeza mambo yote ya maisha kuanzia ndoa,mavazi,kula, biashara,mahusiano baina ya jamii,utasemaje siyo mfumo wa maisha,mfumo wa maisha ni nini?
Quran imeuweka utamaduni wa kiarabu kwa njia ya maandishi.
Humo ndani kuna mambo mengi.
Nb: Tamaduni huwa zinaingiliana na kumezwa pia.
Unarudiarudia vitu visivyo na msingi,sisi wenye Quran tunaijua yote na iliyoelekeza,hakuna utamaduni wa kiarabu, maelekezo hayo wakipewa waarabu awali kabla ya walimwengu, waarabu wakiambiwa waache tamaduni zao wafuate Quran
Acha kumeza propaganda,Quran haijashuswa na haijakamilika.
Maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yaliyoletwa hapa duniani unahisi yaliletwa kwa kusoma Quran?
Quran kushushwa na kukamilika kunahusiana nini na binaadam kuunda roketi,simu na magari!?..hivi unaelewa hata Quran ni kitu gani!?
?
Nafikiri umetumia jazba na hisia zaidi kuliko uhalisia.Nimekuambia tumia akili yako vizuri.Toka nje ya boksi.
Huwezi kuutenganisha utamaduni wa kiarabu na uislamu kwa namna moja ama nyingine.
Nadhani umeamua kukaza fuvu,hutaki kuelewa, waarabu wa makkah walimpiga vita mtume na kumfukuza kwa kuharibu tamaduni zao