Kutunza kwa kutupa pesa chini ni kosa, waweza kukamatwa - Profesa Kabudi

Kutunza kwa kutupa pesa chini ni kosa, waweza kukamatwa - Profesa Kabudi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wale wenzangu na miye wa Tandika, Mwananyamala, Tandale na Mbagala waliozoea kutunzana pesa kwenye vigodoro vya HAKIKA, UBATIZO, KUMTOA MWALI au Kipaimara, watambue kwamba ni makosa makubwa kumtunza mtu fedha kwa kuzitupa chini, iwe kwenye mkeka, kitambaa au sakafuni.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Sheria na Katiba Mh Kabudi, ambapo imeelezwa kwamba atakayekutwa akifanya hivyo atakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kudharau pesa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Video hii hapa



1634968007525.png
 
Ametaja kifungu gani Cha sheria au naye Ni kwa maoni yake Kama yule mtoa hukumu alivyotuthibitishia??
 
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Kabudi amesema kuanzia sasa mtu yoyote atakayetunza kwenye sherehe kwa kutupa hela chini atashtakiwa mahakamani.

Source: Eatv!
Hajatumia neno "Kwa sasa" kasema hamjui tu ila kutupa hela chini ni kosa, inaonekana sheria hipo tangia zamani! Pia kaendelea kusema wekeni kitu kama kikapu muwe mnaweka.
 
Back
Top Bottom