Kutunza kwa kutupa pesa chini ni kosa, waweza kukamatwa - Profesa Kabudi

Kutunza kwa kutupa pesa chini ni kosa, waweza kukamatwa - Profesa Kabudi

Badala ya sheria za kipumbavu za kuweka ndani bila ushahidi anaongelea visivyo tija
 
Angeweka wazi kuwa anaongelea hela ya madafu. Sidhani kama ana mamlaka na dolari. Hawa watu wamepoteza muelekeo kabisa. Wanajisemea na kujifanyia lolote linalowajia kichwani kwa wakati huo. Si walimkamata Maua Sama, nini kiliendelea baada ya pale, mbona watu waliendelea kurusha pesa?
 
Bora hao wanaotunza kwa kutupa..

Yeye atueleze pesa zetu zilitumika kwa manufaa gani kufuata Juice Madagascar akaishia kunywa mwenyewe na mwenzie huku akihadaa watanzania kuwa shehena iliyobaki inaenda kufanyiwa tafiti.

Je hakutupa pesa yetu kwa safari hiyo isiyokua na umuhimu?
 
Kufuatilia wanaotunza fedha kwa kutupa chini ili uwafunge ni kukosa kazi..utawafanya wasizalishe,utawapa chakula,maji na dawa jela
 
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Kabudi amesema kuanzia sasa mtu yoyote atakayetunza kwenye sherehe kwa kutupa hela chini atashtakiwa mahakamani.

Source: Eatv!
Aisee Tz ina watu hupenda shughulika na vitu vidogo, Kama sio kutafuta sifa , kwani kutunza mtu pesa ikaanguka chini ina shida GANI ? au nayo inasaidia mzunguko wa pesa kua chini?
 
Back
Top Bottom