Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hili liwe angalizo kwa Watekaji na Wauaji na Viongozi wa Nchi ya Tanzania Wanaowatuma kuteka na kuua, Kwamba CHADEMA haitavunjika Moyo kutokana na Mauaji ya Mohamed Kibao, hizi mbinu za vitisho kwenye zama za sasa ni mbinu zilizopitwa na Wakati.
Mzee Kibao alipokuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga hakuna aliyemgusa, kumtisha wala kumteka, Kuhamia CHADEMA tu limekuwa kosa la hukumu ya Kifo!
Hizi siasa za kishamba zinazoletwa na viongozi wa sasa wakiongozwa na Samia Suluhu Hassan, hazina tija yeyote kwenye Nchi na wala hazitoikatisha tamaa CHADEMA, zaidi sana zinaidhalilisha Nchi kwenye Jumuiya ya Kimataifa.
Pia soma: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Bali Ifahamike Kwamba Chadema itaendelea kuhakikisha Nchi na Wananchi wanakombolewa, hii ni kwa sababu Hakuna mahali popote kwenye Dunia hii ambako Shetani aliwahi kumshinda Mungu
Hata wewe Mwanaccm hupaswi kufurahia jambo hili, hii ni kwa vile Shetani hajawahi kuwa na Rafiki, akichoka kushughulika na Chadema atashughulikia Wanaccm Wenzake, Mifano ni Mingi Mno, Nape Nnauye, Edward Lowassa na Phillipo Mangula iwe sehemu ya Mafunzo kwenu.