Pre GE2025 Kuuawa kwa Mzee Ali Kibao hakutafifisha jitihada za CHADEMA kuikomboa nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jinga tu nyie
 
Haya mambo ya kuuana sio issue kabisa. Serikali ilichukulie hili swala kwa uzito sana maana hii chuki inayo pandikizwa ni mbaya sana inaweza kudumu kwa vizazi kazaa mbeleni.
Na kama ni watu wa serikali wana husika wajue madaraka sio kitu cha kudumu wasitengeneze mazingira mabaya kwa vizazi vyao vijavyo.
Kila mtu ana haki ya kuishi mpaka pale mwenyezi Mungu atakapo mhitaji
 
Mzee Kibao alipokuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga hakuna aliyemgusa, kumtisha wala kumteka, Kuhamia CHADEMA tu limekuwa kosa la hukumu ya Kifo!
Kuna mengi zaidi ya kutambua katika tukio hili.
Kwanza, huyu anatumika kama mfano kwa aina fulani ya watu ambao hawatakiwi kuwa ndani ya CHADEMA. Huo ni ujumbe tosha kwao.

Inawezekana sasa kuanza kujenga nadharia ya aina fulani kuhusu kinacho endelea nchini. Kuna kundi linalomshikiria mama na kuhakikisha atabaki madarakani kwa manufaa ya kundi hilo maalum. Kwa sasa sitataja sifa kuu ya kundi hili; lakini viashiria vya wazi vipo na vinaanza kujitokeza waziwazi. Pengine kufikia kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, kundi hili litakuwa lime jibainisha zaidi kuliko ilivyo sasa.

Ule mgawanyiko tulio dhani tulisha vuka ngazi hiyo salama, inawezekana sana wakati huu ndio ukawa tatizo kubwa kwa Tanzania.
Hizi siasa za kishamba zinazoletwa na viongozi wa sasa wakiongozwa na Samia Suluhu Hassan, hazina tija yeyote kwenye Nchi na wala hazitoikatisha tamaa CHADEMA, zaidi sana zinaidhalilisha Nchi kwenye Jumuiya ya Kimataifa.
Huyu mwanamke alisha jitambulisha toka zamani kuhusu mambo haya, lakini watu hawakujuwa tu na kujifanya kupuuza. Sasa watamwona alivyo kiuhalisia wake.

Kawapanga watu wake sehemu zote husika huku watu wakipuuza upangaji wake huo. Sasa kazi ndio imeanza.
 
Nape Nnauye alipotekwa alikuja kwetu kutulilia, tunaamini na wewe siku yako ikifika utakuja
Punguani.baada ya msiba nawaangalia chadema wanawasha magari yao ya kifahar wanaondoka.
Nikaangalia na wanaFamilia nikasikitika sana
 
Ndivyo akili madhubuti iliyojaa utu na ubinadamu inanifanya niwe na tafakari ya namna hio, kama una maswali tukutane kwenye comments.

Chief Wadiz
 
Mungu ipokee roho ya Ally Kibao, Amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…