Kuna kitu sijaelewa
--- Kila ukipita kwenye post za watu ( hata mimi nimeuliza ) wanaouliza kuhusu Samia yuko wapi, unakutana na Team ya Waziri Rajabu inatoa matusi ya nguoni kwa wanaouliza Rais wa Nchi Yuko wapi
--- Kwa kipi rahisi? Kuajili Team kutukana watu mtandaoni au Samia kujitokeza tu na kupoza hii hali ambayo imeendelea kwa wiki mbili sasa?
-- Watu wanahoji sababu wanajua sheria za nchi zinasemaje, Lakini pia haiwezekana Rais wa Nchi akaondoka na kwenda nchi kama Marekani kisha akapotea tu kama upepo na kusiwe na Mswali
-- Kwa nini Gharama kubwa inatumika kutuma watu kutukana badala ya kuja na HOJA
Hii inaacha maswali makubwa zaidi, sababu haiwezekana serikali ikatumia gharama kubwa kulipa wahuni badala badala ya ku address suala muhimu la Samia yuko wapi
Mwisho serikali inatakiwa kujifunza wakati wa Magufuli alipopotea serikali ilikuja kwa namna inavyokuja sasa na kuna baadhi ya watu walikamatwa mwisho wa siku tukamzika Magufuli, Mpaka leo serikali imekaa kimya awakuomba radhi
Samia YUKO wapi, hii ndio hoja ijibiwe