Kuuliza alipo raisi Samia ni kiherehere

🤣🤣🤣 Chuo cha kukera watu ulisomea wapi Mkuu?.Huu uandishi kibokooo🤣🤣🤣
 
Kikwete alivyokwenda Marekani kufanyiwa upasuwaji wa tezi dume alitangaza atakuwa Marekani kwa matibabu kwa wiki mbili.

Sionagi logic yoyote ya kufichaficha mambo ambayo wala siyo ya siri.
 
Kwani Zaidi ya Wizara ya mambo ya nje, chombo gani kingine cha habari cha Canada kilitaarifu kuhusu kutokea kwa Kimbunga Rafael tarehe 6-7?
 
Sio kila aulizae hajui....hao wanaolizauliza wanashaka na nini?
 
Rais ni mtumishi wa umma.

Kachaguliwa na umma, analipwa na umma, anawajibika kwa umma.

Hivyo, watu wakitaka kujua alipo mtumishi wao wanaomlipa, wana haki hiyo, ni haki ya kikatiba.

Tatizo inaonekana una uelewa mdogo sana wa haki za kikatiba na kiraia.
 
Hilo bandiko sio la mtu mwenye uelewa mdogo wa Haki za kiraia Mkuu. Soma tena!
 
Hilo bandiko sio la mtu mwenye uelewa mdogo wa Haki za kiraia Mkuu. Soma tena!
Ni la mtu mwenye uelewa mdogo wa haki za kiraia, ndiyo maana anaona ajabu wananchi kuuliza rais yuko wapi.

Haelewi kuwa rais ni mtumishi wa raia.

Haelewi kuwa raia wana haki ya kikatiba ya kujua rais yuko wapi.

Kutoelewa mambo hayo ya msingi kabisa katika haki za kiraia ni kuwa na uelewa ndogo wa haki za kiraia.

Na inawezekana hana ueleea hata mdogo, hajali kabisa mambo ya uelewa wa haki za uraia anajali mambo ya ujingaujinga tu ya "huyo mwanamke damu inachemka".
 
Huyu katumia Lugha ya kinyumenyume Mkuu🤣🤣🤣
 
Nimeona maandiko kadhaa humu toka kwa wadau mbalimbali wakihoji kuhusu kutoonekana hadharani kwa Rais Samia a.k.a Nani kama mama.
Wengine wanafika mbali wanasema amerudi akiwa kwenye Sanduku na kuahirishwa Safari ya Cuba ni kutuandalia mazingira ya kututangazia kilichojiri kwa hio anaandaliwa wa kuisogelea maiki wengine wanamuulizia Maja yupo?
 
Cuba wapo vizuri kwenye mbinu za kivita ingawa hawavumi saana ila wanaoenda kusoma Cuba wengi hugeuka kua wana Mapinduzi
Cuba ilisifika miaka ile 1950s, nyakati za ujamaa, Cuba ipo nyuma sana hata kwa muonekano wa miji yao.

Ni nchi masikini, huwezi kuwa na mbinu bora za kivita halafu huna pesa.
 
Cuba ilisifika miaka ile 1950s, Cuba ipo nyuma sana hata kwa muonekano wa miji yao.

Ni nchi masikini, huwezi kuwa na mbinu bora za kivita halafu huna pesa.
Walioenda kusoma Cuba wanaelewa Mimi sina la kuongeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…