Kuuliza si ujinga: Katika ugo wa kisiasa hapa Tanzania, 'Mabeberu' ni akina nani hasa?

Kuuliza si ujinga: Katika ugo wa kisiasa hapa Tanzania, 'Mabeberu' ni akina nani hasa?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
  • Inasemwa kuwa nchi yetu iko kwenye vita ya kiuchumi na maadui wakuu vitani humo ni 'mabeberu'.
  • Wapo watanzania na wasio watanzania wanaotajwa kutumiwa na 'Mabeberu' kutukwamisha kwenye vita ya kiuchumi tuipiganayo Kama taifa.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' hawafurahii kuiona Tanzania ikipiga hatua za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' wako macho na bize na mipango yao ya kutukwamisha. Kuwa karibu yao ni 'usaliti' kwa Tanzania, husemwa.
Ni akina nani hasa ndio 'Mabeberu' ili nami kama mtanzania mzalendo nijiweke kando na mbali nao?
 
Hizi ni siasa za kuiita mizimu ya siasa ya Ujamaa na kujitegemea. Huwezi kuwa na mabeberu kwenye uchumi wa soko huria kama wetu uliochanganyika na ubepari uchwara.

Enzi zile tunaanza kujenga nchi yetu juu ya dhana ya Ujamaa na kujitegemea, ili kuhalalisha utaifishaji wa mali za watu (Nationalization) tulitumia neno ":mabeberu" kuonesha kwamba wale waliotaifishiwa mali zao wanatetewa na watu wa nchi za Ulaya Magharibi (Zama hizo) dhidi ya maslahi ya nchi yetu!!
 
Mabeberu ni neno la enzi za mwalimu. Wote ambao hawakua wanaunga mkono sera za kijamaa waliitwa mabeberu, wanyonyaji, wasiotutakia mema na mambo kama hayo.

Watu wote waliokua wanahoji utendaji kazi wa mwalimu aliwaita mabeberu. Ukimpinga mwalimu unakua beberu.

Mabeberu kwa ujumla ni wazungu. Wazungu hao wakituchangia kwenye bajeti na miradi wanaitwa wahisani na washirika wetu wa maendeleo. Wakihoji matumizi ya pesa walizotupatia kama msaada wa maendeleo na kusaidia bajeti wanakua mabeberu.
 
  • Inasemwa kuwa nchi yetu iko kwenye vita ya kiuchumi na maadui wakuu vitani humo ni 'mabeberu'.
  • Wapo watanzania na wasio watanzania wanaotajwa kutumiwa na 'Mabeberu' kutukwamisha kwenye vita ya kiuchumi tuipiganayo Kama taifa.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' hawsfurahii kuiona Tanzania ikipiga hatua za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' wako macho na bize na mipango yao ya kutukwamisha. Kuwa karibu yao I 'usaliti' kwa Tanzania, husemwa.
Ni akina nani hasa ndio 'Mabeberu' ili nami kama mtanzania mzalendo nijiweke kando na mbali nao?
Mimi naiona tofauti . Mabeberu ni hawa wanaong'ang'ania madaraka hata pale uwezo wao wa kuongoza nchi unapokuwa umefikia ukomo. Hawa walio tayari kuuwa wananchi wa Tanzania mradi wabaki madarakani. Mbinu hizi hata makaburu wa SA na pote duniani walizitumia.

Kama hata ajira zimekuwa mpaka uwe mtoto wa kada ?! Ni nini hicho kama si ubeberu dhidi ya waTz wengine ?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali zuri na fikirishi katika kutafuta hawa wanaoitwa 'mabeberu' kama kweli wapo au ni dhana tu isiyo na ukweli nia ni kudanganya umma wa waTanzania kuwa wanaharakati ni mawakala wa 'mabeberu' walio maruhani / wasiokuwepo.

Hii hapa chini ni clip muhimu ya historia ya wanaharakati Tanzania na changamoto walizopitia ambazo vijana wa zamani wanatuelezea sisi wa leo. Kubwa ni kujijengea tabia ya kuuliza bila kuchoka ili kupata majibu ya kweli.

Source : wanazuoni
 
Mabeberu ni neno la enzi za mwalimu. Wote ambao hawakua wanaunga mkono sera za kijamaa waliitwa mabeberu, wanyonyaji, wasiotutakia mema na mambo mama hayo.

Watu wote waliokua wanahoji utendaji kazi wa mwalimu aliwaita mabeberu. Ukimpinga mwalimu unakua beberu.

Mabeberu kwa ujumla ni wazungu. Wazungu hao wakituchangia kwenye bajeti na miradi wanaitwa wahisani na washirika wetu wa maendeleo. Wakihoji matumizi ya pesa walizotupatia kama msaada wa maendeleo na kusaidia bajeti wanakua mabeberu.

Ha ha ha ha. Wewe kama GuDume.
 
Hizo hoja mnazotaka zijibiwe ni zipi, hakuba lolote la maana analolizungumza, ila kilio cha maafa yaliyomkuta, na habari za kuokotwa na kuletewa na washabiki wake.

Huyo ni a wolf cryer
Hakuna cha mabeberu wala maajuza, ni kwamba pumzi imekwisha! Yote hayo yametokana na kuwa hoja za Lissu hazijibiki!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom