Kuuliza si ujinga: Katika ugo wa kisiasa hapa Tanzania, 'Mabeberu' ni akina nani hasa?

Kuuliza si ujinga: Katika ugo wa kisiasa hapa Tanzania, 'Mabeberu' ni akina nani hasa?

  • Inasemwa kuwa nchi yetu iko kwenye vita ya kiuchumi na maadui wakuu vitani humo ni 'mabeberu'.
  • Wapo watanzania na wasio watanzania wanaotajwa kutumiwa na 'Mabeberu' kutukwamisha kwenye vita ya kiuchumi tuipiganayo Kama taifa.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' hawsfurahii kuiona Tanzania ikipiga hatua za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' wako macho na bize na mipango yao ya kutukwamisha. Kuwa karibu yao I 'usaliti' kwa Tanzania, husemwa.
Ni akina nani hasa ndio 'Mabeberu' ili nami kama mtanzania mzalendo nijiweke kando na mbali nao?
Both Mabeberu na Mafisadi are the mythical creatures. Ni viumbe wa kufikirika... These are technical jargon Used for political purpose only...
 
HOJA YA BEBERUNADHANI SASA INATAKIWA IFE, TUJIKITE KATIKA KUMUUNGA MKONO MH. JPM KATIKA KULETA MAENDELEO,..

1550677325399.png
 
Samahani mkuu na Mimi sielewi Mzalendo maana yake Nini, hebu fafanua maana ya Mzalendo/Uzalendo hasa hii ambayo imekuwa ikongelewa Sana siku hizi kuwa vijana kuweni wazalendo au watu wasio wazalendo [emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
Someone who is patriotic loves their country and feels very loyal towards it.
Mzalendo ni mtu ambae ana upendo wa kweli juu ya nchi yake na ni mwaminifu kwa nchi yake.

My thinking, mara kwa mara wakubwa huwa wanatuhamisisha wananchi tuwe wazalendo. Ila mara nyingi viongozi huwa wanapungukiwa sana na uzalendo.

With exceptional ya kiongozi ambae ni"Jiwe", kajipambanua kuwa mzalendo wa kweli sio wa maneno. Kuna mengi anayafanya kwa kuhakikisha anakuwa mwaminifu kwa nchi yake kwa kuhakikisha nchi anafaidika na rasilimali zetu. Amekomaa na mikataba mibovu, amekaba mianya ya shekels zilizokuwa zinavuja kwenye mifuko ya wajanja wachache.

By works is very is to know nani mzalendo na nani anaongea tu bila kutenda
 
  • Inasemwa kuwa nchi yetu iko kwenye vita ya kiuchumi na maadui wakuu vitani humo ni 'mabeberu'.
  • Wapo watanzania na wasio watanzania wanaotajwa kutumiwa na 'Mabeberu' kutukwamisha kwenye vita ya kiuchumi tuipiganayo Kama taifa.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' hawsfurahii kuiona Tanzania ikipiga hatua za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' wako macho na bize na mipango yao ya kutukwamisha. Kuwa karibu yao I 'usaliti' kwa Tanzania, husemwa.
Ni akina nani hasa ndio 'Mabeberu' ili nami kama mtanzania mzalendo nijiweke kando na mbali nao?
UKWELI MCHUNGU: Ukikuta nchi/utawala u/i/mepoteza dira na mwelekeo jua kutakuwa na MAADUI WASIOJULIKANA WAKITAJWA.
TUJIULIZE NA KUJITAFAKARI:
1. UHURU NA KAZI
2. KILIMO NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA
3. AFRIKA LAZIMA IWE HURU (NCHI ZA MSTARI WA MBELE
KUMNG'OA NDULI
USIPOWAJIBIKA OLE WAKO
UKWELI NA UWAZI
KILIMO KWANZA
LEO TUNAWAZA VIWANDA!!!!!
 
Mabeberu ni kichaka cha kujifichia maovu ambayo CCM imeitendea nchi hii. Wakiiba, wakifisidi, wakidhulumu, wakiharibu, wakiishiwa hoja hukimbilia kuwatuhumu wanaowaambia ukweli kuwa wametumwa na mabeberu.
 
Februari 20, 2019

Kongamano la "Wenye Nchi ni wananchi'

Katika kongamano la "Wenye Nchi ni wananchi' lililoandaliwa na Jukwaa la Change Tanzania.

Source : MCL Digital
 
BARRICK GOLD MINE ni moja ya MABEBERU wanaoongelewa na Serikali Elewa hivyo.
 
  • Inasemwa kuwa nchi yetu iko kwenye vita ya kiuchumi na maadui wakuu vitani humo ni 'mabeberu'.
  • Wapo watanzania na wasio watanzania wanaotajwa kutumiwa na 'Mabeberu' kutukwamisha kwenye vita ya kiuchumi tuipiganayo Kama taifa.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' hawafurahii kuiona Tanzania ikipiga hatua za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' wako macho na bize na mipango yao ya kutukwamisha. Kuwa karibu yao ni 'usaliti' kwa Tanzania, husemwa.
Ni akina nani hasa ndio 'Mabeberu' ili nami kama mtanzania mzalendo nijiweke kando na mbali nao?

Ni CHADOMO
 
Mabeberu ni neno la enzi za mwalimu. Wote ambao hawakua wanaunga mkono sera za kijamaa waliitwa mabeberu, wanyonyaji, wasiotutakia mema na mambo kama hayo.

Watu wote waliokua wanahoji utendaji kazi wa mwalimu aliwaita mabeberu. Ukimpinga mwalimu unakua beberu.

Mabeberu kwa ujumla ni wazungu. Wazungu hao wakituchangia kwenye bajeti na miradi wanaitwa wahisani na washirika wetu wa maendeleo. Wakihoji matumizi ya pesa walizotupatia kama msaada wa maendeleo na kusaidia bajeti wanakua mabeberu.
Daah kweli kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Inasemwa kuwa nchi yetu iko kwenye vita ya kiuchumi na maadui wakuu vitani humo ni 'mabeberu'.
  • Wapo watanzania na wasio watanzania wanaotajwa kutumiwa na 'Mabeberu' kutukwamisha kwenye vita ya kiuchumi tuipiganayo Kama taifa.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' hawafurahii kuiona Tanzania ikipiga hatua za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' wako macho na bize na mipango yao ya kutukwamisha. Kuwa karibu yao ni 'usaliti' kwa Tanzania, husemwa.
Ni akina nani hasa ndio 'Mabeberu' ili nami kama mtanzania mzalendo nijiweke kando na mbali nao?
Ukiwajua, nistue.

World Bank wanaweza kuwa marafiki zetu wa dhati leo (mkopo wa flyover Ubungo). Kesho wakawa mabeberu (mkopo wa elimu hadi mabinti waja wazito warudi shule).
 
Jenerali Ulimwengu akijibu maswali na hoja za vijana kuhusu Haki na Wajibu wa raia ktk Kongamano Wananchi wenye Nchi

  • Inasemwa kuwa nchi yetu iko kwenye vita ya kiuchumi na maadui wakuu vitani humo ni 'mabeberu'.
  • Wapo watanzania na wasio watanzania wanaotajwa kutumiwa na 'Mabeberu' kutukwamisha kwenye vita ya kiuchumi tuipiganayo Kama taifa.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' hawafurahii kuiona Tanzania ikipiga hatua za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  • Inasemwa kuwa 'Mabeberu' wako macho na bize na mipango yao ya kutukwamisha. Kuwa karibu yao ni 'usaliti' kwa Tanzania, husemwa.
Ni akina nani hasa ndio 'Mabeberu' ili nami kama mtanzania mzalendo nijiweke kando na mbali nao?

Beberu ni mzungu fisadi. si wazungu wote ni mafisadi na hivyo si wazungu wote ni mabeberu. Kitaliano mabeberu wanawaita Mafioso. Kwahiyo si wazungu wote ni mafioso, bali mafioso ni ka group fulani ka ma mafioso wa kuibia nchi zingine kimafioso ndo mabeberu.
 
Mabeberu ni ideal tu hawapo sijui nani karudisha fikra hizi Karne hii ya 21.

Sent using Jamii Forums mobile app
Toleo jipya la Kamusi ya zamani ya Lumumba (revised CCM dictionary). Toleo la zamani la miaka ya 70 na 80 ilikuwa imesheheni msamiati wa 'mabeberu', 'mabepari', 'makabaila', 'mirija', 'kupe' nk kama propoganda ya kutukuza itikadi ya ujamaa. Toleo la miaka ya 90 hadi majuzi (pre-Magufulization) 'mabeberu/mabepari/makabaila' wakageuka kuwa 'waekezaji', 'wahisani' na 'wadau wetu wa maendeleo'. Kama Jenerali alivyotudokeza kuwa katika awamu ya 5 zinapandwa mbegu za kuturudisha nyuma miaka 50, Magufulization haiwezi kufikia malengo bila kuibua 'kamusi' ya ujamaa, na ndio sababu za ufufuko wa "mabeberu". Ukiunda utopian goals, ni lazima pia uunde na Mnyamwezi wa kubebesha lawama (= adui). Kwa hivyo tutawasikia sana 'mabeberu' katika awamu hii ya Magufulization!
 
Back
Top Bottom