Waungwana salamu kwanza.
Katika utawala huu wa awamu ya tano neno "Mabeberu" limetumiwa zaidi kuliko awamu ya nne na ya tatu, siwezi kuzungumzia awamu ya kwanza na ya pili. Neno hili ambalo mara nyingi limekuwa likitumika sana kuonssha kwamba "Mabeberu" ni watu wabaya mno na wasioitakia mema nchi yetu.
Hebu basi tushughulishe akili zetu tujiulize Mabeberu ni akina nani? Je Tanzania inaweza kuendesha mambo yake bila Mabeberu?
Mabeberu ni akina nani?
Neno Mabeberu ni neno la kiswahili ambapo kwa kiingereza huita "imperialist".
Imperialism is a policy of extending a country's power and influence through colonization, use of military force, or other means. Hii ni kwa mujibu wa Merriam Webster dictionary. Ikiwa na maana kwamba ubeberu ni sera za kutanua ushawishi wa nchi kwenye nchi nyingine kwa njia za kivita au njia ya ukoloni/ ukoloni mamboleo, au njia nyingine yoyote ile.
Kwa maana hiyo ni sawa kwamba nchi nyingi za ulaya, marekani na Asia zinaweza zikawa ni Mabeberu kwani mara nyingi huwa zinapambana kuongeza ushawishi kwenye nchi za kiafrika. Ushawishi huo huwa wa kiuchumi, kisiasa, kijamii na zaidi kiuchumi.
Ni njia gani hutumiwa na Mabeberu?
Mabeberu hutanua ushawishi wao kwa nchi za kiafrika kupitia ukoloni mamboleo. Marekani au uingereza hahitaji kuja kutawala hapa Tanzania sijui kuleta jeshi nakadhalika ili aitawale Tanzania. By the way sababu kubwa ya nchi za ulaya kuzipa Uhuru nchi za afrika ni kwa sababu ukoloni ule wa mwanzo baada ya mkutano wa Berlin ulikuwa ni gharama mno. Yaani Uingereza anakuja kutawala Tanganyika anagharamia kila kitu, anajenga miundombinu analeta staff kutoka uingereza pamoja na jeshi. Ni kutokana na gharama hizo za ukoloni ndipo walipoamua kuachia makoloni yao ili yajiendeshe na matokeo yake wakaja na ukoloni mamboleo.
Kupitia ukoloni mambo leo sasa haihitajiki gharama kubwa kama awali kuchota madini na maliasili za waafrika. Malkia anavuna dhahabu za Tanzania akiwa London bila kutumia jeshi wala nguvu. Mabeberu hutumia Makampuni makubwa, Benki ya Dunia, IMF nk kueneza ubeberu katika nchi za kiafrika.
Je Tanzania inaweza kuondokana na ubeberu?
Ndiyo inaweza,
kama tu itaacha kutegemea misaada,
kama itaacha kutegemea makampuni makubwa kama Barrick yaje kuwekeza badala ya kuyapa nguvu makampuni ya ndani.
Kama tu tutaacha kutegemea mikopo kutoka World Bank na IMF.
Je Tanzania inaweza kuendesha mambo yake bila Mabeberu?
Ni swali gumu naogopa jibu linaweza likawa hapana au ndiyo yaani kutokutegemea IMF? WB? USAID? EU? China? nk wakati hao ndiyo tunaowaita wadau wa maendeleo?
SERIKALI YA AWAMU YA TANO NA MABEBERU
Serikali ya Magufuli haina tatizo na mabeberu wala ubeberu wao, naam haina nia ya dhati ya kupambana na Mabeberu, Serikali inayopambana na Mabeberu haiwezi ikawa inabembeleza misaada na mikopo kutoka WB, IMF, Marekani, EU nk
Kiufupi hii ni Serikali ya kinafiki Mabeberu wakiingilia siasa ndiyo wanakuwa wakali lakini wakiwapa misaada wanawaita wahisani na wabia wa maendeleo. Wasichokijua ni kwamba jinsi wanavyopokea misaada yao ndivyo wanavyowapa nguvu ya kuingilia mambo yetu ya ndani ya nchi. Huwezi ukamwambia Marekani asikuingilie wakati unamtegemea, Uchina inaweza ikamwambia uingereza asimwingilie lakini Tanzania haiwezi maana hiyo ni mbia wa maendeleo.
Wakatabahu