Kuuliza si ujinga: Tunapokopa kama Taifa, dhamana yetu huwa ni nini?

Baba au mama akikopa pale nyumbani wewe kama mtoto unashirikishwaga?

Ok, utasema mimi ni mwananchi natakiwa kujua kinacho endelea, swali nikwamba kwanzia umezaliwa mpaka sasa kuna maamuzi yoyote uliyotoa wewe kama mwananchi yakasikilizwa ma kufanyiwa kazi?

Hayo maswali nliulizwa jana kwenye banda la mpira, baada ya kuliza swali kwanini tz tunakopa bila taadhari
 
Sasa hivi iko chini ya Chief Hangaya.
 
China imechukua bandari ya Hambantota huko Sri Lanka kwa miaka 99 baada ya nchi hiyo kushindwa kulipa deni lake lililokuwa linadaiwa na China.
 
Tulipinga kodi ya Kichwa tukajibiwa positively na Serikali ya awamu ya tatu chini ya Uongozi mahiri wa Mheshimiwa Benjamin Mkapa.Na tulipigania Mfumo wa Vyama Vingi kwa nguvu zote tukajibiwa na Mzee wa viwango Ndugu Ali Hassan Mwinyi Rais wa Awamu ya Pili.
 
Wewe ni mwanasheria nafkiri unapaswa kufanya mapitio na kutupa usahihi au maadirio kuwa huu mkopo tunaweza kuwa tumeweka rehani hiki na hiki. Pia, uko resourceful kupata details ukatusaidia sisi maamuma
 
na kibaya zaidi tunakopa kama serikali lkn hiyo fedha wanachukuwa watu binafsi, rostamu is 8 billion dollars worth jiulize hiyo fedha kaitoa wapi? kujibu swali lako dhamana ni kodi wanazotozwa wananchi mpaka mafao ya uzeeni ndiyo maana ya tozo, usisahau raisi wa tanzagiza halipi kodi hivyo haimuhusu …
 
CCM ni Chama cha Matapeli.
 
Kuna nchi ilikopa china alafu ikashindwa kulipa, walichofanya wachina walichukua bandari ya hiyo nchi.

NB: nna wasiwasi hata DP world ikawa tuliweka rehani bandari tukashindwa lipa mkopo ndio ikabidi dp world wapewe bandari.
 
Kuna nchi ilikopa china alafu ikashindwa kulipa, walichofanya wachina walichukua bandari ya hiyo nchi.

NB: nna wasiwasi hata DP world ikawa tuliweka rehani bandari tukashindwa lipa mkopo ndio ikabidi dp world wapewe bandari.
Inaweza kuwa hivyo.
 

Mm navyojua hata uweke dhamana pia ukikopa lazima wazingatie kile kifungu cha ability to pay. Sasa hawa wanaotukopesha huwa wanazingatia nini hasa ili hali wanasema sisi ni masikini?
 
Taifa haliendeshwi kwa mfumo wa familia wa baba, mama na watoto wao. Taifa linaendeshwa kwa mfumo wa katiba na social contract. Hao waliouliza hayo maswali kwenye banda la mpira ni vilaza majuha wasiojua chochote kuhusu raia na haki zao kama walipa kodi na wenye nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…