Takribani mikopo yote inayotolewa kwa watu binafsi, taasisi au nchi huwa na masharti. Pamoja na kwamba masharti hayo kukubaliwa na pande zote za mkopo husika (Mkopeshaji na Mkopaji), masharti hayo huandaliwa na Mkopeshaji kwa ajili ya kulinda maslahi yake-urejeshwaji wa mkopo pamoja na faida.
Kati ya masharti ya mkopo ambayo yasioepukika ni kuhusiana na dhamana ya mkopo (security/securities). Hapa Mkopaji huweka rehani mali yake fulani kama dhamana au hakikisho la kulipwa kwa mkopo. Pale ambapo Mkopaji anaposhindwa kulipa mkopo huo, Mkopeshwaji hushughulika na dhamana hiyo kwa njia mbalimbali ikiwemo ya kuiuza.
Dhamana za mikopo ni vitu kama ardhi, mishahara, magari, mitambo, hisa na kadhalika. Hizi zimekuwa za kawaida na maarufu kwenye mikopo itolewayo na taasisi za kifedha kwa watu binafsi, taasisi na kadhalika. Kwa ngazi za kinchi (pale ambapo nchi moja inaikopesha nchi nyingine) dhamana ya nchi mkopaji huwa ni nini hasa? Najua masharti mengineyo kama muda wa kulipa huwepo pia.
Mfano, Tanzania inapokopa kutoka mfano Benki ya Dunia au nchi nyingine, dhamana ya mkopo husika huwa ni nini?
Wewe ni mwanasheria kitaaluma kama sijakosea.
Inashangaza kuwa unauliza kama mtu wa kawaida tu asiye na idea yoyote ya mambo haya ambayo basically ni maswala ya kisheria.
Mimi nafikiri ulipaswa tu ufahamu kuwa, nchi inapokopa au inapotoa udhamini ktk mikopo iwe kwa mtu binafsi au taasisi au kampuni kwenye taasisi za kifedha za kimataifa kama WB, IMF, au nchi nyingine nk maana yake na kwa ufahamu wa haraka haraka tu ni kuwa dhamana itakuwa ni nchi (ardhi ya nchi husika) na watu wake.
Nchi maana yake: Vyote vilivyomo ktk ardhi ya taifa hilo i.e natural resources (ardhi yenyewe, madini, misitu, maji, bahari nk).
Watu (citizens) na walivyo navyo: Raia, majengo yao yaliyo nje ya nchi, international bonds, nk
Je, huwa Kuna clauses ktk mikataba hiyo kuweka bayana haya?
Hili swali ndilo linanishangaza zaidi toka kwako Mwanasheria by professional Mr
Petro E. Mselewa.
Hivi unategemea nchi yako ipewe mkopo wa over 6trl halafu kusiwe na masharti ya hakikisho kuwa waliotukopesha watarudisha pesa zao?
KWA HIYO: Jibu la swali lako ni obvious NDIYO kuwa lazima zipo clauses zinazotoa hakikisho hili iwe ni directly au indirectly.
Mfano mdogo tu ni mkataba wa Bandari zetu ambao kila mtu aliuona ukiwemo wewe.
Angalia masharti yake. Hayako direct lakini mtu akisoma ataelewa kuwa, tumetoa mali yetu bure kwa mataifa ya nje kwa sababu ya ujinga na upumbavu wa viongozi wetu!
Ndivyo ilivyo kwenye mikataba ya mikopo hii.
Laiti ukipata nafasi ya kuiona mikataba ya mikopo hii, nakuambia unaweza kutoa machozi kiasi cha kujiuliza hawa viongozi walikuwa wamepofushwa na nini hata kukubali masharti haya? Jibu ni RUSHWA maana rushwa hupofusha ufahamu wa mtu!!
Lakini utafanyeje maana viongozi wetu hawa wanaiona leo tu na sio kesho ya taifa hili na watu wake? Ni kwa sababu pia wanakuwa wameshavuta cha kwao ku - sustain matumbo yao na familia zao, basi.